Makapuku Forum

Makapuku Forum

20201217_153528.jpg
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amefanya mabadiliko katika jeshi la Uganda (UPDF)na kumrejesha mwanae Lt.Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais yaani Special Force Command(SFC)


Mabadiliko hayo yamefanyika wakati wanasisa wa upinzani wakilaumu jeshi la polisi kwa kuwasumbua katika kampeni zao za uchaguzi zinazoendelea nchini. Jenerali Mhoozi amerudishwa kwenye cheo ambacho aliwahi kukitumikia kabla ya kubadilishwa kuwa mshauri wa rais Museveni katika masuala ya ulinzi.Na kitengo hicho ndicho kina husika na kumulinda rais wa Uganda.


Mabadiliko haya yamefanyika wakati zikiendelea kampeni za uchaguzi mkuu wa rais ambapo wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakituhumu jeshi la polisi kuwatatiza kwenye kampeni zao,lakini Msemaji wa jeshi amesema ni mabadiliko ya kawaida tu.
.
.
20201217_165440.jpg
 
Wewe unaoga mara ngapi kwa siku?


"Ninajihisi vizuri kabisa ," " Unazowea tu" dokta James Hamblin alipoulizwa anajihisi vipi baada ya kuishi bila kuoga kwa kipindi cha miaka mitano !


Hamblin 37, ni mtaalamu aliyesomea taaluma yake katika chuo kikuu cha Yale University kitengo cha huduma ya afya ya umma na ni daktari bingwa wa tiba ya kuzuia magonjwa.


"Unapooga kwa sabuni ya nguvu kila wakati, unaharibu bayoanuwai ya mwili wako.
Vimelea huongezeka haraka, lakini bayoanuwai hii haiwiani na ile asili ambao hutengeneza harufu ya mwili ,"alielezea katika taarifa yake.


Je mwili hautanuka mtu asipooga?



"Ninafahamu watu wengi ambao wanaoga mara chache sana. Nilifahamu kuwa inawezekana , lakini nilitaka kujaribu ili nione kutooga kutakuwa na athari gani ."

'' Baada ya kutooga muda mrefu mwili unazoea zaidi na zaidi kwahiyo haunuki vibaya usipotumia sabuni au manukato ."

"Na mwili wako haupati mafuta unapoacha kutumia sabuni kali ."

"Lakini la kubwa la kuelewa ni kwamba inachukua muda kuona athari hizi, hazijitokezi haraka, sio mara moja ."



Haya wangwana, Swali.....

Kama kuoga ndio usafi
kwanini taulo huchafuka?
.
.
20201217_165730.jpg
 
Katika hatua inaonekana kuikera Somalia,
Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itafungua ubalozi mdogo katika eneo linalojitawala lenyewe la Somaliland mwakani.


Tangazo hilo la pamoja limetolewa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somaliland Muse Bihi Abdi mwisho wa ziara yake nchini Kenya.


Somaliland ilijitenga na Somalia 1991, lakini juhudi zake za kutaka kutambuliwa kimataifa kama taifa huru hazijafanikiwa huku Somalia ikisisitiza kuwa bado ni sehemu ya eneo lake.


Somalia imetangaza kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya.


Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema kamati imebuniwa kutatua mzozo kati ya nchi hizo, kwani zina uhusiano wa muda mrefu ambao unastahili kulindwa.


Jeshi la Kenya ni sehemu ya majeshi ya Umoja wa Afrika yanayolinda serikali ya Somalia dhidi ya wapiganaji wa Al Shaabab.
.
.
20201217_170117.jpg
 
Netflix Inc. imemteua bilionea wa Zimbabwe, Strive Masiyiwa kuwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi, ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kupanua soko la Afrika.

Masiyiwa ni muanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya mawasiliano ya simu, Econet Global inayotoa huduma Afrika, Asia, Ulaya na Latini Amerika.
20201217_170424.jpg
 
Wanafunzi 759,706 (91.1%) kati ya wanafunzi 759,737 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2021.

Kati ya waliochaguliwa, wavulana ni 368,174 na wasichana ni 391,532. Wanafunzi 4,169 watajiunga na shule za bweni, wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi.

Aidha, wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi na wanafunzi 1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.
20201217_170553.jpg
 
Umoja wa Ulaya (EU) umesitisha msaada wa takribani TZS bilioni 255 kwa Ethiopia kutokana na mgogoro wa Tigray.

EU imetoa masharti ya kuachia fedha hizo ambayo ni pamoja kukoma kwa mapigano na hotuba za chuki, kurejeshwa mawasiliano ya simu na redio Tigray, misaada ya kubinadamu iruhusiwe kuwafikia wahitaji, uchunguzi wa ukiukwaji haki za binadamu na raia wanaotaka kuondoka waruhusiwe kuingia nchi jirani
20201217_170804.jpg
 
Pakistan imepitisha sheria mpya ya kukabiliana na vitendo vya ubakaji ambayo pamoja na mambo mengine imeruhusu matumizi ya kemikali kiwahasi wabakaji. Sheria hiyo pia italinda utambulisho wa waathiriwa na inataka kesi za ubakaji kukamilika ndani ya miezi minne.
20201217_170945.jpg
 
Edinson Cavani ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu na Shirikisho la Soka England [FA] juu ya chapisho lake katika ukirasa wake Instagram mwezi uliopita.

Mchezaji huyo atakabiliwa na kufungiwa baadhi ya michezo na amepewa muda hadi kufikia Jumatatu ya tarehe 4 Januari 2021 kutoa utetezi wake.

Basi utopolo wanatamani haya yangemkuta Morrison
20201217_171330.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom