Makapuku Forum

Makapuku Forum

20201217_153937.jpg
 
DUNIANI wapo wahalifu wengi wa matukio mbalimbali lakini Afrika Kusini haiwezi kumsahau jamaa huyu anayeitwa Andre Stander ambaye alikuwa askari mpelelezi na wakati huohuo alikuwa jambazi sugu na wa kuogopeka.



Stander wakati mwingine alitumia muda wa mapumziko ya mchana kazini na kuaga kuwa anakwenda kula chakula cha mchana, lakini alitumia mwanya huo na kwenda kutekeleza uhalifu kwa kufanya uvamizi katika mabenki.



Stander alifanya uhalifu huo akiwa amevaa kinyago (mask) usoni ili asifahamike na kuiba mamilioni ya pesa kisha kurudi ofisini kama kawaida lakini cha kushangaza zaidi alikuwa anarudi tena kwenye benki hiyohiyo aliyoiba kama polisi mpelelezi akichunguza wizi alioufanya bila watu kumjua kama mhalifu aliyetekeleza tukio hilo ni yeye.



Hata hivyo, za mwizi ni 40, siku moja askari wenzake walimuotea akifanya uhalifu wakamnasa, na alifunguliwa kesi za kuiba pesa kwenye mabenki zaidi ya 20.



Baada ya hapo alifungwa lakini cha kushangaza zaidi alitoroka gerezani, jambo lililowatia hasira wananchi wa Afrika Kusini na serikali kwa jumla, kwani walianza kumsaka na mnamo Februari 13, 1984, Stander aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati akijaribu kuwakimbia.

20201217_153541.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom