Manchester United wamewasiliana na Fulham juu ya uwezekano wa kusaini mkataba na mlinzi Ryan Sessegnon, mwenye umri wa miaka 19 siku ya Jumapili, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akilengwa na Tottenham. (Sky Sports)
Everton wanapanga dau la £35m kwa ajili ya mshambuliaji wa Bournemouth Muimngereza Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 27, lakini hawakutaka kulazimishwa kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29, kwa mkataba wa pesa. (Sun)
Juventus wamewasiliana na meneja wa Chelsea Maurizio Sarri baada ya kutangazwa kwa taarifa ya kuondoka kwa Massimiliano Allegri hivi karibuni. (SNAI, via Express)
Sarri watashinikiza uamuzi kutoka kwa Chelsea kuhusu msimamo wao baada ya fainali ya Ligi ya Ulaya kwani mikataba ya wakufunzi wake wote inamalizika na iwanahitaji kujua wazi hatma zao. (Times
Newcastle na Rafa Benitez wako tayari kuendelea na mazungumzo juu ya hali ya baadae ya meneja wikendi hii, huku, wakiwa pande hizo mbili zikiwa bado hazijafikia makubaliano. (Newcastle Chronicle)
Griezmann ataondoka Atletico Madrid msimu huu lakini Manchester City na Paris St-Germain wameachaachana na mpango wa kumchukua mshambuliaji huyo (independent)
Wakili wa mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, anatarajia kukutana na maafisa wa klabu ya Barcelona ili kukamilisha mpango wake wa kuhamia timu hiyo . (Marca)
Duru kutoka Newcastle zimesisitiza kuwa mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Uingereza Sean Longstaff, anahamia Manchester United, hayuko katika mpango wao wa mauzo msimu huu. (Newcastle Chronicle)