Badili fikra zako, epuka kuwaza kushindwa na waza mafanikio. Utakuta mtu hata bado hajaanza kazi fulani anasema, hawezi wakati hajafanya akashindwa kwa mfano, suala la ujasiriamali, ukimwambia mtu aanze kujishughulisha na ujasiriamali, jambo la kwanza atasema, hawezi kutengeneza bidhaa kama sabuni na mafuta ya kupaka. Wengine watasema, hawawezi kwani hawana mtaji, hebu jiulize, ukiambiwa kuna gari jipya aina ya Noah au Toyota linauzwa shilingi za kitanzania laki moja na nusu (150,000/=) hutazipata?
Ukweli ni kwamba, mjasiriamali wa kawaida huanza na mtaji chini ya laki na nusu na faida na mtaji huongezeka kadri anavyoendelea kufanya biashara na hatimaye kumiliki biashara kubwa. Hivyo ondoa ile fikra ya kushindwa na jiamini kuwa unaweza.