Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,112
- 1,249,267
Usiabudu mtu, jiabudu mwenyewe. Kuna kasumba za watu ambao wana tabia ya kuwaabudu matajiri. Kwa mfano, wafanyakazi wengi hasa wale wa sekta binafsi kama vile wahudumu hotelini na wengine wanapoteza uwezo wao halisi wa kufanya kazi kwa kuwa mkurugenzi yupo karibu yao na hivyo wafanyakazi wanakuwa waoga ambao unatokana na kuamini kuwa mkurugenzi huyo anao uwezo wote juu ya maisha yao hivyo kusahau kuwa nao wanaweza kumiliki mradi kama huo na mkurugenzi pia ni mtafutaji kama wao na siku moja wanaweza kumuajiri katika miradi yao.
