Makapuku Forum

Makapuku Forum

3a20de6693afe93e646962f54f1fe961.jpg
f6ddaffac1d3bbaa0866cd02d4aa349d.jpg
 
Moja ya anguko kubwa sana la kibiashara kuwahi kutokea Duniani, ni kutoka Kampuni ya Nokia. .
.
Jifunze kitu, Mwaka 1998 Nokia alitajwa kuwa kampuni kubwa ya Simu za mkononi Duniani.
.
.
Mwaka 2003,Walitoa simu ya "Nokia 1100" ambayo ilitajwa kuja kuleta mapinduzi makubwa katika Ulimwengu wa Simu na kweli ilinunuliwa Haswa (SWIPE KUIONA) na mpaka sasa ndio Brand ya Nokia ambayo imenunuliwa zaidi kuzidi zingine... Lakini hapa ndipo matatizo yalianzia...Kivipi?
.
.
Ni hivi... Wakati Apple wanatoa simu ya iPhone toleo la kwanza mwaka 2007, asilimia 95 ya simu zote duniani zilizokuwa zikitumiwa na watu zilikua ni Nokia. .
.
Lakini Chaajabu ni baada ya Miaka 5 mbele Thamani ya Nokia ilishuka kwa takribani asilimia 90, na mwaka 2013 Microsoft waliinunua Nokia hapo ndio Wakazidi kujizika zaidi. .
.
Kuna kitu Tujifunze, Kilichowaangusha Nokia ni Kubweteka na Sifa kemkem Walizokuwa wakipewa, Walijiona wao ndio bora na hakuna Kampuni yoyote ingeweza Kuwapindua hivyo Walikosa kuendana na Soko Kwa kushindwa kuleta Ubunifu mzuri kwa Haraka Na Chaajabu zaidi katika Kampuni ambayo hata hawakuifikiria au Haikufikiriwa ingeweza kufanya Maajabu katika Upande wa Simu ni Apple. .
.
Sababu wao walionekana kuwa wapo upande zaidi wa computers na iPod.. Lakini kilichowatokea hawatokaa Kuamini mpaka sasa. .
.
Wakati wanastuka kutoka Usingizini, ilikua tayari hali imebadilika licha ya kujitahidi kufanya mabadiriko kadhaa Bado hali kwao imekuwa ngumu. .
.
Mambo yanaweza kubadirika kwa haraka sana zaidi hata unavyofikiria, Hakuna Muda wa kupoteza. Hakikisha Unapambana kikamilifu kwa nguvu sana, Sababu Wakati wewe unafurahia Mafanikio yako, Kuna mtu yupo Chini Anapambana Afikie Mafanikio tena katika Jambo ambalo wewe Pia Unafanya. .
.
Acha Kuutumia UBONGO wako katika mambo yasiyofaa, Hakikisha kila siku unakuwa mtu mpya. .
04b177fbeb3b143d3cfaa30d1644a0a8.jpg
520aed194fb43c0a5332998ec8a4adc4.jpg
 
Mwaka 1501-1504 Mchongaji maarufu wa sanamu wa Italia Michelangelo alipewa kazi ya kuchonga sanamu ya Daudi nchini Italia katika mji wa Florence.

Kwa kuwa Michelangelo alikuwa maarufu kwa kazi hizo kitendo hicho kilivutia wengi kutaka kuona atakavyoichonga.

Kwa miaka miwili mizima alizunguka huku na kule akitafuta jiwe litakalofaa aina ya sanamu aliyotaka kuchonga.

Siku moja pembeni mwa Barabara moja aliona jiwe lililokuwa limeotewa na magugu na lilikuwa na uchafu.
Alipolikwangua kidogo akagundua ni jiwe aina ya Marble.

Akawaagiza vijana wake waliviringishe hadi kwenye karakana yake.

Akatumia miaka miwili kulipiga nyundo na kuchonga ili kupata picha rough ya Daudi.

Kisha akatumia miaka miwili tena kulipiga msasa na kusawazisha vizuri ili kupata sanamu kamili. Yenye urefu wa mita 5 na nchi17.

Kazi ilipomalizika sanamu ile ilipelekwa kwenye Town square Florence ili kuzinduliwa.

Mara ilipofunguliwa watu waliokuwa wametoka kila pembe ya Italia kuja kuangalia sanamu hii walipigwa na butwaa na baadhi ya wanawake walizimia kwa ustadi iliochongwa na uzuri wake.

Baadaye walipomuuliza Michelangelo amewezaje kuchonga sanamu nzuri vile jibu lake lilikuwa "Mimi nilimuona Daudi akiwa amekamilika ndani ya lile jiwe, kazi yangu ilikuwa ni kuondoa kile ambacho sio Daudi." Leo unaweza ukawa ni Daudi ambaye umejificha ndani ya magugu ya mashaka, hofu, uvivu, na kutokujiamini.

Mwaka 2019 uutumie kuondoa kile ambacho sio we we ili ubaki wewe. Ndani yako Mungu ameweka MTU mkubwa sana lakini bado hujamwona. .
.
Elekeza nguvu zako katika KUJITAMBUA.
9f450273f5cd368e3f90ba502a2a3030.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom