Sayari mpya yagunduliwa ndani ya mfumo wetu wa Jua. Sayari hiyo imepewa jina la 2018 VG18 au "Farout" ipo umbali wa takribani maili bilioni 11 au sawa na mara 100 ya umbali kati ya Dunia na Jua - au umbali sawa na Voyager 2, chombo ambacho kimeingia kwenye Intersteller hivi karibuni.
Kwa sasa mengi bado hayajafahamika kuhusu sayari hiyo ambayo imegunduliwa na wanasayansi wakati walipokuwa wakitafuta sayari ya 9 maarufu kama planet X.
Farout inakadiliwa kuwa na ukubwa wa kipenyo cha kilometa 500 na inatumia miaka 1,000 kukamilisha mzunguko wake mmoja kwenye Jua.
Ugunduzi wa sayari hii umewapa matumaini wanasayansi katika kuongeza juhudi za kuipata sayari ya 9 (Planet X) na hii imeonesha bado kuna sayari zingine nyingi tu zipo kwenye mfumo wetu wa Jua zikisubiri kugunduliwa.
Miongoni mwa watu maarufu waliowai kutaka ufanyike uchunguzi kuhusiana na ndege zisizotambulika - UFO ni milionea Laurence rockeffer ambaye kwa sasa ni marehemu mwaka 1993 hadi 1995 tajiri huyo alitoa kiasi cha fedha za kuanzisha na kuendesha kampeni ya kutaka serikali ya raisi bill Clinton nchini Marekan iueleze umma ukweli kuhusiana na UFO ingawa serikali hiyo ilikubaliana na matakwa hayo lakini baadaye ilielezwa kuwa uchunguzi haukubaini chanzo cha UFO.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.