Makapuku Forum

Makapuku Forum

KARUDI BABA MMOJA

Karudi baba mmoja
Toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja
Na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja
Ili kumtaka hali
Wakataka na kauli
Iwafae maishani

Akatamka mgonjwa
Ninaumwa kwelikweli
Hata kana nikichanjwa
Haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa
Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Yakawatoka kinywani
Maneno yenye adili
Baba yetu wa thamani
Sisi tunataka mali
Urithi tunatamani
Mali yetu ya halali
Sema ipo wapi mali
Itufae maishani

Baba aliye kufani
Akajibu lile swali
Ninakufa masikini
Baba yenu sina mali
Neno moja lishikeni
Kama mnataka mali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakazidi kumchimba
Baba mwenye homa kali
Baba yetu watufumba
Hatujui fumbo hili
Akili zetu nyembamba
Hazijajua methali
Kama tunataka mali
Tutaipataje shambani

Kwanza shirikianeni
Nawapa hiyo kauli
Fanyeni kazi shambani
Mwisho mtapata mali
Haya sasa buriani
Kifo kimeniwasili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Alipokwisha kutaja
Fumbo hili la akili
Mauti nayo yakaja
Roho ikaacha mwili
Na watoto kwa umoja
Wakakumbuka kauli
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Fumbo wakatafakari
Watoto wale wawili
Wakakata na shauri
Baada ya siku mbili
Wote wakawa tayari
Pori nene kukabili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakazipanda shambani
Mbegu nyingi mbalimbali
Tangu zile za mibuni
Hata zitupazo wali
Na mvua ikaja chini
Wakaona na dalili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Shamba wakapalilia
Bila kupata ajali
Mavuno yakawajia
Wakafaidi ugali
Wote wakashangilia
Usemi wakakubali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakanunua na n'gombe
Majike kwa mafahali
Wakapata na vikombe
Mavazi na baiskeli
Hawakuitaka pombe
Sababu pombe si mali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakaongeza mazao
Na nyumba za matofali
Pale penye shamba lao
Wakaihubiri mali
Wakaweka na kibao
Wakaandika kauli
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani
 
KARUDI BABA MMOJA

Karudi baba mmoja
Toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja
Na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja
Ili kumtaka hali
Wakataka na kauli
Iwafae maishani

Akatamka mgonjwa
Ninaumwa kwelikweli
Hata kana nikichanjwa
Haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa
Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Yakawatoka kinywani
Maneno yenye adili
Baba yetu wa thamani
Sisi tunataka mali
Urithi tunatamani
Mali yetu ya halali
Sema ipo wapi mali
Itufae maishani

Baba aliye kufani
Akajibu lile swali
Ninakufa masikini
Baba yenu sina mali
Neno moja lishikeni
Kama mnataka mali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakazidi kumchimba
Baba mwenye homa kali
Baba yetu watufumba
Hatujui fumbo hili
Akili zetu nyembamba
Hazijajua methali
Kama tunataka mali
Tutaipataje shambani

Kwanza shirikianeni
Nawapa hiyo kauli
Fanyeni kazi shambani
Mwisho mtapata mali
Haya sasa buriani
Kifo kimeniwasili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Alipokwisha kutaja
Fumbo hili la akili
Mauti nayo yakaja
Roho ikaacha mwili
Na watoto kwa umoja
Wakakumbuka kauli
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Fumbo wakatafakari
Watoto wale wawili
Wakakata na shauri
Baada ya siku mbili
Wote wakawa tayari
Pori nene kukabili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakazipanda shambani
Mbegu nyingi mbalimbali
Tangu zile za mibuni
Hata zitupazo wali
Na mvua ikaja chini
Wakaona na dalili
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Shamba wakapalilia
Bila kupata ajali
Mavuno yakawajia
Wakafaidi ugali
Wote wakashangilia
Usemi wakakubali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakanunua na n'gombe
Majike kwa mafahali
Wakapata na vikombe
Mavazi na baiskeli
Hawakuitaka pombe
Sababu pombe si mali
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani

Wakaongeza mazao
Na nyumba za matofali
Pale penye shamba lao
Wakaihubiri mali
Wakaweka na kibao
Wakaandika kauli
Kama mnataka mali
Mtaipata shambani
Aisee ndo mambo yenyewe hayo.?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom