Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu mzee unayemuona alivamia benki moja na bastola, akaiba dola 1 ambayo ni sawa na 2200 tu.

Alipofanikiwa, hapohapo benki akakaa chini na kuwasubiri polisi wamkamate.
Alipohojiwa sababu akasema yeye ni mgonjwa, hapati huduma ya afya na anaishi mitaani ila akipelekwa gerezani basi huduma zote atazipata bure.View attachment 932809
hatariii
 
RIP Jembe Stan Lee.

Unapomuona Spiderman, Ironman, Black Panther, Ironman na superheroes wengi kutoka Marvel...huyu mzee ndiye aliwatengeneza miaka hiyo kupitia michoro iitwayo Comic.

Leo ameafariki. Ni pengo kubwa sana. Ameigiza filamu zote za Marvel...swip kuona baadhi ya vipande alivyoigiza japokuwa naamini wengi hawakumfahamu.

Screenshot_20181114-151118.jpeg
Screenshot_20181114-151138.jpeg
 
Stan Lee, mwanaume shupavu ambaye alihakikisha dunia inafurahia matunda yake ameondoka siku chache zilizopita. Ni pigo kwa kila mtu anayependa muvi, ni pigo kwangu, kwa yule na dunia nzima.

Maisha yake ni ya mapambano sana, kila siku amekuwa mtu wa kuamini kwenye vitu vyake anavyovifanya, amekuwa muumini mzuri wa kuamini kile alichokuwa akikitengeneza. Katika miaka ya 1930, jamaa alikuwa na wazo lake la kutengeneza vitabu vya vikatuni (comic). Hakukaa na wazo hilo kichwani mwake na kuliacha kwani aliamini kwamba kama asingefanya yeye, kuna siku jamaa fulani angekuja kufanya na kujuta maisha yake yote kwani kipindi hicho, yeye akiwa na kampuni ya Marvel ambayo ipo chini ya Disney, upande wa pili kulikuwa na watu walioitwa DC.

Hawa ndiyo waliomtengeneza Superman, Batman, Wonder Woman na wengine wengi. So wazo lake lilikuwa ni kutengeneza hivyo vitabu na kweli akafanikiwa. Alitengeneza vingi vikiwemo vya Ironman, Spiderman, Dr. Strange, Captain America na wengine wengi.

Baadaye, miaka ya 2000 akaja na wazo jingine kwamba kwa nini badala ya kuendelea kutengeneza vitabu vya vikatuni asihamie kwenye muvi? Wazo lake hilo akalipa nafasi kwani tayari DC walikuwa wamekwishaanza kitambo.
Hakuwa akijiamini kabisa lakini mwisho wa siku akajiamini na kusema kwamba nitaweza, hivyo akathubutu. Kwenye mafaili yake yote ya vikatuni, akasema ngoja nianze na Spiderman, akatoa muvi, ikafanya vizuri, huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuandaa filamu nyingine kupitia vilevile vitabu alivyovitengeneza katika maisha yake.

Akatengeneza pesa nyingi, si jambo geni kuona filamu yake ikitengeneza dola bilioni moja ama mbili. Amefanya hivyo kwa The Avengers, Black Panther na nyinginezo nyingi. Hivyo basi, kama kweli tutahitaji kutengeneza mamilioni ya shilingi, tuwe kama huyu jamaa.

Ni kweli hakujiamini mwanzo, alijua atashindwa lakini baadaye akafumba macho, akajitoa na kuthubutu, dunia ikamuamini, ikampenda na kumpa pesa.
Leo usipojiamini, ukabaki ulivyo, utaendelea kuwa hivyo milele. Thubutu kama Stan Lee.
R.I.P Legend.
Screenshot_20181114-151350.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom