Makapuku Forum

Makapuku Forum

Uvaaji soksi na utunzaji wake

Soksi ni vazi ambalo huvaliwa miguuni.
Miguu ni mmoja kati ya viungo ambavyo vinatoa jasho mwilini, huzalisha
zaidi jasho kila siku.
Soksi husaidia kuhakikisha kuwa unyevunyevu unahifadhiwa katika eneo
linalotakiwa na baadaye kutolewa nje kwa njia ya hewa.
Katika mazingira ya baridi soksi husaidia kupunguza uhakika wa kupata baridi.
Soksi hutengenezwa kwa pamba, sufu, nailon na aina nyingine za nyuzi.
Katika kuongeza kiasi cha ulaini, malighafi nyingine ambazo
hutengenezaa soksi hutumika.
Kuna aina mbalimbali za rangi za soksi ambazo hutengenezwa na pia
kuvaliwa kila siku.
 
Wengine huvaa soksi ili kuimarisha muonekano wao
Soksi za rangi ya kung’aa mara nyingi huwa ni sehemu ya vazi katika
michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutofautisha wachezaji pale
ambapo miguu pekee ndiyo inaonekana.
Mitindo ya soksi huvaliwa kulingana na matakwa ya mvaaji.
Wengine hupenda kuvaa soksi na viatu vya wazi huku wengine wakivaa na
viatu vilivyozibwa.
Soksi ndefu nyeupe huvaliwa kama sehemu ya sare za shule.
Wanamichezo wamekuwa wakitumia soksi kama sehemu ya vazi. Soksi hizi
huwa ndefu na mara nyingi huwa ni nzito.
Makundi mbalimbali yamekuwa yakivaa soksi hata wanawake ambao huvaa
soksi katika kuhakikisha wanakuwa na muonekano mzuri na mavazi
waliyovaa.
 
Kuna zile soksi nyepesi sana hizi mara nyingi huvaliwa na wanawake.
Soksi ni vazi ambalo huvaliwa kila siku hasa kwa wanaume ni vizuri
kama soksi zinakuwa safi muda wote ili kuondoa ile harufu mbaya ambayo
imekuwa kero kwa watu wengi.
Ni vizuri kama soksi zikafuliwa na kuanikwa juani na kukauka vizuri
kabla ya kuvaliwa. Pia wavaaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na
jozi nyingi za soksi ili kuweza kupunguza ugumu wa kuzitunza.
mwisho
 
Umaridadi wa wanaume uko mikononi mwa wanawake

LEO nataka tukumbushane kitu kimoja nacho ni jinsi ya kumfanya mwenzi
wako aonekane maridadi wakati wote. Hapa nazungumzia wale walio katika
mahusiano ya kudumu ambao wanaishi pamoja.
“Nikiamka asubuhi jambo la kwanza ni kumuandalia mume wangu maji ya
kuoga, nahakikisha nguo zake zimepigwa pasi, viatu vimeng’arishwa,
soksi ziko safi, na akivaa lazima nimfunge tai, na nguo za kazini mimi
ndiye nachagua siku hiyo avae nguo gani” anasema Mama mmoja mkazi wa
Kimara Jijini Dar es Salaam.
Sikiliza na hii “ Mimi mume wangu huwa anaandaa nguo zake mwenyewe
anafua, apige pasi au asipige shauri yake, aoge asioge atajijua, huo
muda sina kabisa siku hizi” anasema mwanamke mmoja Mkazi wa Buguruni
Jijini Dar es Salaam.
Siku zote tumekuwa tukisisitiza urembo kwa wanawake na utanashati kwa wanaume.
 
Mmoja ya jukumu la mwanamke ni kuhakikisha kuwa, mwanaume wake anakuwa
maridadi na mwenye kuvutia. Jaribu kuangalia ni nguo za aina gani mume
akivaa zinampendeza na hapo unaweza kumchagulia shati na suruali
ambazo rangi zake zinaendana na hata akivaa zitamfanya apendeze.
Pia suala zima la kufua na kupiga pasi vizuri ni moja ya njia ya
kuonyesha kuwa unamjali na unamjengea namna ya kujiamini
zaidi.Utunzaji wa soksi ikiwemo ufuaji wa nguo za ndani ni jambo
linalosisitizwa sana kwani wanaume wengi wanaonekana kutojali sana
vitu hivyo ama kutokana na muda au kwa kukosa ushirikiano wa wenzi wao
katika kutunza na kufanyia usafi aina hizo za nguo.
 
Jamani mwanaume akiwa maridadi au mtanashati huwa anamvutia kila mtu
na zaidi sifa zinakwenda kwa mkewe ambaye anaaminika kuwa ni chanzo
cha mwanaume kuwa msafi.
Jenga mazingira ya kujali usafi wa nguo za mwenzi wako ili kuhakikisha
kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
Pia kuna wanawake wengi ambao ni wajuzi wa kufunga tai, kama hilo bado
hulifahamu tafuta mtu ambaye atakufundisha namna bora ya kufunga tai
ili uweze kumpendezesha mume wako.
Kama unapita dukani au sehemu zinakouzwa nguo si vibaya kama unaona
kuna nguo inaweza kumfaa mwenzi wako mna ukahakikisha kuwa akivaa
anapendeza usisite kununua kwani itakuwa ni zawadi nzuri sana kwake.
Jaribu kuwa na tabia ya kumvika mwenzi wako, si kuacha kila kitu
afanye yeye kuanzia kufua, kupiga pasi na hata kung’arisha viatu.
 
Ni vizuri kama utaamua kuhakikisha kuwa, unamuaandaa mume wako kabla
ya kwenda kazini kisha na wewe kuendelea na shughuli zako.Hilo
litaongeza upendo na amani kwenye nyumba.
Wanawake wengi wamejisahau sana na kuacha wanaume wafanye kila kitu
wenyewe jambo ambalo husababisha wanaume wengine watoke nyumbani bila
kupiga pasi au kusahau kuchana nywele.
Jirekebishe kama una tabia za kutojali usafi wa mwenza wako,
utanashati ni muhimu kwa wanaume pia usiishie kwa wanawake kujipenda
na kujiremba kila wakati huku wakisahau waume zao
 
Onyoaji ndevu wenye raha

MOJA ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho
wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa.
Pengine hili ndilo linalowasumbua watu mpaka wanajisikia vibaya
kuzaliwa wanaume, halafu hataki ndevu na ndevu zinakuja kama
zimepaliliwa vile. Lakini haya ni maamuzi tu ya kimsingi kwani naamini
unyoaji ndevu unaweza kuwa laini na wenye raha kubwa kama utafuata
haya ambayo nataka kukueleza.
Nafahamu mwanamke wako hapendi ndevu anapenda kuwa na kidevu laini
chenye raha yake kukigusa ingawa najua vile vile wapo wanawake
wanaopenda kukwanguliwa kidogo kwa namna Fulani na kidevu chenye
ndevu.
 
Kwa wanaume wengi asubuhi ni siku ya matatizo makubwa. Ili kuondoa
matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka katika
aina Fulani ya raha kubwa.
1.Chagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi
yako. Kuna aina nyingi sana za mashine za kunyolea pamoja na nyembe
zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa kuzingatia mahitaji yako
hasa ya aina ya ndevu
2.Weka uso safi na usio uchafu. Safisha kabla ya kunyoa. Hii
inakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili
kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.
 
3. Usisahau kuloweka kidevu chako vyema. Hii inasaidia wenye kupita
kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana
kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.
4.Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia
sana kufungua vishimo vya vinyweleo. Pia unaweza kupata masaji ya
chapchap katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.
5.Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi
yako na chagua linalostahili unalotaka. Jipake kiasi cha kutosha
katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.
 
6.Unaponyoa chagua zinapoelekea ndevu. Usiendelee kunyoa sehemu
iliyokwisha kunyolewa. Italeta matatizo na ua uwasha na ukomavu wa
aina Fulani wa kidevu na mbaya zaidi unaweza kujikata.
7. Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote. Tumia
moistrurizer baada ya kunyoa.
Epeka kutumia after shave yenye pombe. Pombe inasababisha ngozi
kupoteza unyevunyevu wake kwa haraka.
 
Unatakiwa kuwa makini zaidi katika kutunza uso wako

WATU wengi wamekuwa wakichukulia suala la utunzaji wa ngozi ya uso kwa
umakini zaidi. Ngozi zina mahitaji maalum ikiwemo kuweka ngozi katika
hali ya usafi na pia kuikinga ngozi na miale ya jua na mabadiliko
mengine ya hali ya hewa.
Ngozi ya uso inahitaji umakini zaidi kwani uso ni utambulisho wa
jinsi ulivyo na imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu
uso umekuwa ukizalisha mafuta mengi hasa kwenye paji la uso, macho,
pua, na kidevu.
 
Hitaji muhimu ni kuhakikisha kuwa, ngozi yako inakuwa katika hali
nzuri na safi kuanzia asubuhi unapoamka hadi usiku unapokwenda
kulala.
Unatakiwa kuchukua dakika tano hadi 10 katika suala hili.
Utunzaji wa uso asubuhi
Wakati wa asubuhi unatakiwa kusafisha uso wako kwa maji ya vuguvugu.
Epuka kutumia sabuni ya mche (ya kufulia) kwani haikutengenezwa
maalum kwa ajili ya uso na imekuwa ikifanya ngozi ya uso kuwa
iliyokakamaa
Unatakiwa kuhakikisha kuwa, uynaosha uso wako vizuri wakati unaoga au
wakati unanawa uso kwenye sinki,
Unaweza kutumia tona kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu
ulioganda usoni. Baadaye unaweza kutumia moisturiza .
 
Utunzaji wa uso jioni
Jioni unaweza kusafisha uso wako kwa kutumia maji ya vuguvugu. Baada
ya mizunguko ya hapa na pale ngozi inakuwa imechoka na inahitaji
umakini zaidi katika suala la usafi.
Pia unapotumia tona jaribu kutumi pamba laini ili kuweza kulinda uso wako.
Unapotunza ngozi lengo ni ngozi kuwa na unyevunyevu, unatakiwa
kuhakikisha haina magamba.
Lakini pia unaweza kutoa magamba au ngozi iliyokufa ambayo hufanya
ngozi isiyokubalika.
Wakati mwingine ngozi isiyokubalka husababuisha uso kuwa na chunusi.
Angalizo
Usiende kulala bila kuondoa make -up usoni
 
Make-up zimekuwa
zikisababisha kuzina kwa vitundu vya kutolea hewa na hivyo kusababisha
tatizo la kuwa na ngozi isiyokubalika.
Pia unatakiwa kuacha kutumia vipodozi vyenye kemikali kwani hufanya
watu wengine kupata kansa za ngozi.Wakati mwingine sehemu za uso
hupata uvimbe .
Hizi ni moja ya changamoto zinazoweza kukutokea katika ngozi yako la
muhimu ni kuhakikisha kuwa, usafi unazingatiwa sana pamoja na kunywa
maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
 
Uvaaji wa mikufu na utunzaji wake

NI siku nyingine tena katika urembo na nimeona ni muhimu tukaangalia urembo katika shingo zetu.
Wanawake wengi wenye shingo fupi wana wasiwasi kama kuvaa mikufu kunaweza kufanya waonekane wenye shingo ndefu.
Wabunifu wa mitindo wanasema kuwa, kuvaa mkufu mrefu kunaweza kufanya shingo kuonekana kuwa ndefu.
Wanawake wenye shingo fupi wanashauriwa kuvaa mikufu ambayo inaendana na shingo zao.
 
Kama unataka muonekano mzuri wa shingo yako unashauriwa kuvaa mikufu ambayo ni inaendana na shingo yako.
Mikufu ya dhahabu imekuwa ikivaliwa sana na kuonekana kuwapendeza wengi Mikufu hii ni ya thamani kubwa ambapo mingine huwa na nakshi za kuvutia.
Lakini si kila mmoja anapenda kuvaa aina hiyo ya mikufu kutokana na kuwa ni ghali sana na wengi wamekuwa hawamudu gharama zake.
Mikufu inayotengenezwa kutokana na silver naye imekuwa ikipendwa na kuvaliwa na watu wengi wa rika zote.
Aina hii ya mikufu imekuwa ikivaliwa zaidi pia na wanaume ambao hupenda kuivaa ikiwa imetengenezwa mithiri ya minyororo midogo.
 
Uvaaji wa mikufu iunayotengenezwa na dhanga au vitu vya asili kama shamba, vifuu vya nazi na vitu vingine vya asili vimekuwavikivaliwa kwa wingi na wanawake kwa wanaume na kuonekana ni mfano mzuri kwa kutunza utamaduni wa Mtanzania.
Uvaaji wa mikufu hii ya asili huwapendeza zaidi wanawake hasa pale wanapovaa kwa nguo za vitenge huku sehemu kubwa a vazi hili shingoni likiwa wazi.
Mikufu hiyo ina aina ya utunzaji wake ili iweze kudumu zaidi na kuendelea kutunza thamani yake.
 
Tukianza na utunzaji wa mikufu ya dhahabu, hii inahitaji uangalifu wa hali ya juu ilinapokuja suala la wapi na kwa njia gani mikufu hii inaweza kutunzwa.
Mikufu ya dhahabu inapendeza sana kama ikitunzwa kwenye kasha dogo baada ya kulizungushia kitambaa laini hii husaidia vitu hivyo kutopoteza thamani yake kwa kuhifadhi mng’ao wake.
Hata katika uvaaji wake mikufu hii huitaji kuvaliwa vyema kwa uangalifu mkubwa ili isiweze kushikana na nguo na hatimaye kukatika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom