Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wanasayansi wapo karibu kutuwezesha kutengeneza mapacha wetu (cloning). Cloning ni teknolojia ya kutengeneza pacha wako ambaye mnafanana kwa kila kitu pamoja na tabia, na hii imekuwa karibu sio kama sisi tulivyotegemea.

Mwaka 1997 upachishaji wa kwanza uliofanikiwa ulifanyika kwa kondoo aliyeitwa Dolly the sheep, hii ilipelekea raisi wa Marekani enzi hizo Bushi kutangaza teknolojia hiyo sio salama hivyo isitishwe mara moja na tafiti zisiendelee tena. Hata muigizaji wa filamu Arnold Schwarzenegger aliunga mkono usitishwaji wa teknolojia hiyo kwa kuigiza kwenye filamu inayoelezea jinsi pacha wake wa kutengenezwa alivyochukua nafasi ya maisha yake.

Kwa sasa watu wamekuwa wakitoa pesa kwenye makampuni yanayofanya cloning ili watengenezewe pacha wa wanyama wanaowapenda kama mbwa japo ni ghali sana. Kwa sasa imebaki tu kwa binadamu, muda sio mrefu kutokea sasa utakuwa na uwezo wa kutengeneza pacha wa mtu umpendaye hivyo hata akifa bado atabaki pacha wake anayefanana nae kwa kila kitu na tabia.
Screenshot_20181026-090858.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
CUP ndiyo kamera yenye nguvu zaidi Duniani kwa sasa. Kamera hii inauwezo wa kusimamisha muda hata kuweza kupiga picha mwanga katika mwendo wa taratibu sana
Screenshot_20181026-091254.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Wanasayansi wagundua sayari pweke (Rogue Planet) ambalo linaranda nje ya mfumo wetu wa Jua. Sayari hilo pweke ni kubwa mara 12 ya Sumbula (sayari kubwa zaidi kwenye mfumo wetu wa Jua), pia una uga sumaku wenye nguvu mara 200.

Hili dubwana lililopewa jina la SIMP J01365663+0933473 lipo umbali wa miaka 20 ya mwanga nje ya mfumo wetu wa Jua na utofauti wake na sayari zingine lenyewe ni sayari pweke kitaalam zinafahamika kama Rogue Planets - sayari ambazo hazizunguki nyota yoyote badala yake zipo tu zinaranda huko angani.

Kutokana na kuwa kubwa sana wanasayansi mwanzo walidhani ni Brown Dwarf: nyota iliyoshindwa kukua zaidi.
Screenshot_20181026-091552.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Watafiti kutoka chuo cha Minnesota nchini Marekani, wafanikiwa kutengeneza jicho bandia ambalo litawawezesha vipofu kuona tena au kumpa yule anayeona uwezo wa kuona vizuri zaidi.
Screenshot_20181026-091651.jpeg
 
"Hire Me" ni app ambayo kwa sasa inazaidi ya wasichana 1,000 ambao wapo tayari kukodishwa nchini China

Eti nyie wanaume ngoja niwaulize mm shunie kuna faida gani kama huyo mwanamke hamkulani mana hata madomo zege hii app haitawasaidia
Screenshot_20181026-091756.jpeg
 
Hii picha ni ya jeshi la maangamizi na moja kati ya vitu hatari na vyaajabu sana ulimwenguni vitu hivyo si vingine ni mashimo meusi. Hii picha imepigwa hivi karibuni na NASA na kwa mara ya kwanza wameweza kupata picha inayoonesha mashimo meusi mengi yakiwa sehemu moja.

Kiuhalisia si rahisi kwa sisi kuweza kuyaona mashimo meusi, ila kwa bahati nzuri eneo picha hii ilipopigwa kuna nyota, gesi, vumbi, ambavyo vyote ni vyakula vya mashimo meusi. Ili sisi tuweze kuyaona mashimo meusi ni lazima kuwe na nyota au maumbo mengine huko angani.

kila kidoti cheupe unachokiona hapo ni shimo jeusi na huo weupe unasababishwa na masalia ya nyota inayofyonzwa. Kundi hili la mashimo meusi lipo umbali wa mwaka mmoja wa mwanga kutoka Sagittarius A lilipo - hili ndiyo shimo jeusi kubwa zaidi ambalo lipo katikati ya galaksi yetu ya Milky Way. #andewsoft
Screenshot_20181026-092005.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Utafiti huo uliofanywa na NASA, vyuo vikuu pamoja na vituo mbali mbali vya sayansi unaonesha kwamba sababu kuu ya Dunia yetu kuanza kuzunguka hovyo ni sisi binadamu.

Watafiti hao walitumia takwimu zilizokusanywa kwa zaidi ya miaka 100 kutengeneza kiolezo cha kimahesabu ili kufahamu sababu ambazo zimepelekea Dunia yetu kuanza kuzunguka hovyo kitaalamu inafahamika kama "Polar motion".

Katika utafiti huo pia imeonekana kiasi gani gesi chafu tunazozalisha hapa Duniani kutoka kwenye magari, viwanda n.k zimepelekea ongezeko kubwa la joto lililosababisha zaidi ya gigatoni 7.500 za barafu kuyeyukia kwenye bahari. Uzito huo wote ndio umesababisha madhara kwenye mhimili wa Dunia yetu na jinsi inavyozunguka.

NASA wameshatoa tahadhari dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kama ikiendelea hivi inaweza ikaasili maisha yetu hapa Duniani pamoja na vifaa vya teknolojia kwa ujumla
Screenshot_20181026-092152.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Anatoli Bugorski, mwanasayansi kutoka nchini Urusi ambaye mwaka 1978 aliweka kichwa chake kwa bahati mbaya kwenye Hadron Collider - mashine inayotumika kuongeza mwendo wa atoms zenye umeme hadi kufikia kasi ya mwanga sawa na ile inayotumika na wanasayansi kwenye maabara za CERN leo hii.

Basi alipoweka kichwa chake muale wa protoni ulimpiga nyuma ya kichwa chake na kutokea puani, baade upande mmoja wa sura yake ulitanuka kama puto - jamaa aliwahishwa hospitali sio kwa matibabu bali kufanyiwa utafiti kwa sababu tatizo kama hilo yeye ndiye wa kwanza kuwa nalo na madaktari waliamini jamaa angekufa ndani ya siku kadhaa tu.

Jamaa mpaka leo yupo hai (2018) anamiaka 75 ila upande wake mmoja wa sura haujazeeka mpaka leo.
Screenshot_20181026-092324.jpeg
 
Uwezo wetu wa kutuma mawimbi ya sauti nje ya Dunia ni miaka 80 ya mwanga au sawa na kilometa trilioni 720 (maili trilioni 400) au sawa na asilimia 1% ya eneo la galaksi yetu ya Milky Way.

Kwa hiyo tusijali kuhusu uwepo wetu kwenye huu ulimwengu ndani ya miaka 1,500 tutapokea simu zao za kwanza.
Screenshot_20181026-092458.jpeg
 
Lifti hiyo itapunguza gharama na kurahisisha safari za anga za juu.
Screenshot_20181026-092643.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Watafiti hao watengeneza mfumo ambao watu watatu wanaweza kutumiana mawazo yao wanayofikiri.

Mfumo huo unatumia electroencephalograms kuchukua kile mtu anachowaza na transcranial magnetic stimulation kukituma kwa mtu mwingine.
Screenshot_20181026-092839.jpeg
 
Kama viatu vyako vinanuka hatimaye Panasonic wamekuletea MS-DS100 - kifaa kinachofyonza harufu mbaya kwenye viatu vyako.
Screenshot_20181026-092949.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Uanasheria ndiyo taaluma inayokuja kuchukuliwa na kompyuta. Kompyuta zenye weledi wa hali ya juu (AI) zimekuwa zikitupiwa lawama kwa kuchukua kazi za viwandani lakini hata kazi zinazohitaji ueledi nazo zipo hatarini kuchukuliwa na maroboti
Screenshot_20181026-093058.jpeg
 
Sayari hiyo ambayo inafanana kabisa na Dunia yetu ipo kwenye nyota ambayo ipo kwenye nyota inayoitwa Proxima Centauri ambayo ipo jirani na Jua letu na eneo ambalo inaizunguka ni salama kwa viumbe hai kuweza kuishi (habitable zone).
Screenshot_20181026-093204.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom