Kizazi na Uzao: Macho Tofauti Kuangalia Jambo Moja
Wakati anaulizwa kuhusu namna utawala wake ulivyokuwa, baada ya kuwa amestaafu, rais alhaji Ali Hassan Mwinyi (mwalimu huyu) alisema kila zama na kitabu chake. Kuna ukweli katika hili, kila zama na kitabu chake. Nchi yetu kwa sasa, upande wa idadi ya watu unashuhudia kiwango kikubwa cha ongezeko la watu na la kuvutia zaidi ni idadi kubwa ya vijana ambao hawazalishi (chini ya miaka 15), hawa wanaunda asilimia 45 ya watanzania. Asilimia hii inatekutegemea wewe ulete, yenyewe ikae chini ile na kushiba na uhakikishe umeandaa mazingira mazuri ya kizazi hiki (kizazi cha milenia na kizazi cha uzao Z- kuanzia mwaka 1981 na 1995).
Kuna mammbo ya msingi kujadili sasa, nyumba bora hujengwa kwa ramani na msingi. Tunajiandaa vipi kuhakikisha kizazi hiki kinafurahia kuwepo kwetu sasa (BTW, mimi ni kizazi cha milenia FYI)
Tunaliangaliaje hili suala? Huu ni mjadala unaohitaji utulivu kuujadili na hasa kama tunaona kabisa tunakabiliwa na changamoto za utoaji wa huduma za afya, elimu na ajira. Majuzi tu tumesoma na kuona kuwa bajeti inayotengwa kwa ajili ya huduma ya afya haifiki kikamilifu, inafika kwa chini ya asilimia 40.
Makapuku ni sehemu nzuri kuwepo maana mabadiliko hayaletwi na wapiga kelele bali watu wa uzao tofauti wanaoleta tofauti zao pamoja na kuamua kuzitatua kuliko uzao mmoja unaodhani mawazo yake ndiyo suluhu ya changamoto tunazoziona sasa. This is the beauty of diversity, bringing differences together such that the whole is greater than the sum of its parts. Tunaweza kuwa na uono tofauti wa masuala (different optic) lakini hii haimaanishi kuwa kizazi fulani ni sahihi dhidi ya kingine. na hapa ndipo tunapohitaji kukaa kama taifa bila kujali wewe ni wa uzao gani ili kuja na suluhu ya changamoto za leo, kesho na kesho kutwa.
Kama kuna jipya, unaweza kuchangia chochote nikijiaminisha kabisa wewe ni wa kizazi kinachoiangalia juzi kuiona jana na kikishaiona jana kinaifanyia kazi leo kuiboresha kesho na kesho kutwa salama kwa wote na si wachache wenye kufaidika kwa jasho la wengi kesho kutwa.