Makapuku Forum

Makapuku Forum

Marekani imeliwekea vikwazo jeshi la China kufuatia hatua zake za kununua ndege za jeshi kutoka Urusi pamoja na makombora ya kurushwa kutoka ardhini.

Inasema ununuzi kama huo unakiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi kujibu, tabia za Urusi nchini Ukraine na madai ya kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Majuzi China ilinunua ndege 10 za Sukhoi Su-35 na makombora ya S-400.
China haijajiunga kwenye vikwazo ilivyowekewa Urusi kutoka Marekani na washirika wake tangu mwaka 2014
Screenshot_20180922-144220.jpeg
 
Zaidi ya watu 100 wamefariki baada ya mkasa wa kuzama kwa kivuko cha mvnyerere.

Lakini mkasa wa aina hii umewahi kutokea mara kadhaa kwa miaka tofauti

Mungu awapumzishe mahali pema peponi na awatie nguvu sana waliopoteza ndugu zao.
Screenshot_20180922-144503.jpeg
 
Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Reggae Jah Kimbute amefariki.
Ras Kimbute ambaye ni gwiji wa “Roots Reggae” alifariki usiku wa kuamkia leo.

Jah Kimbute ambaye jina lake halisi ni Samuel Mleteni aliwatumbuiza wapenzi wa Reggae miaka ya themanini.
Screenshot_20180922-144713.jpeg
 
Benki ya CRDB imemtangaza rasmi Abdulmajid Musa Nsekela kuwa Mkurugenzi Mtendaji akichukua nafasi ya Dkt. Charles Kimei ambaye atastaafu Mei 2019.

Nsekela aliajiriwa mara ya kwanza CRDB mwaka 1997, mwaka 2008 alihamia NMB kabla ya kurudi tena CRDB.
Screenshot_20180922-145123.jpeg
 
Mwanamfalme wa Uingereza William anatarajia kukutana na Rais Dkt JP Magufuli wiki ijayo akiwa katika ziara isiyo ya kikazi ya siku 7 Afrika.

Watazungumza kuhusu juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama pori.

Baadaye, atatembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Screenshot_20180922-145244.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom