Makapuku Forum

Asante ubarikiwe mamaa
 
Bandiko zuri sana mdau, asante lakini unajua ni kwanini wengine hatuna huo muda wa kukaa tunasoma au kutafuta maarifa mapya kila wakati? Tumeanza majukumu ya familia tukiwa wadogo na hadi tumeweza kununua simu na laptop kuingia JF ni kwa sababu tumeajiriwa na muda wote mwajiri anatutumia hatupi nafasi ya kufanya yale tunayopenda. Kikubwa tunafanya kazi kuhaklikisha watoto wetu waka sawa, hawawi kama sisi. Mungu kumtanguliza ni sawa, lakini si hata kwa Mungu kuna madaraja? bahati mbaya ukiniangalia mtu kama mimi, nyumba zuri zote mjini nilikuwa kibarua, mkono wangu upo kweli kila tofari la pembeni, nilitamani kuweka jina langu lakini mpiga plasta akasema hataki uchafu. Mpiga rangi naye akasema plasta ina harara hivyo akapiga rangi kuondoa harara, hawa wote kama mimi tu nao hawatambuliki na sadaka wanatoa.

Haka katoto ka imam wangu nakaangalia kila siku kanavyotoka chuo kikuu kanakuja na maneno makubwa makubwa, kanachosha akili yangu ambayo matofari na misumali imeichosha, na kakianza kuongelea kuondokana na umaskini nakatizama maana najua kabisa zaka zangu ndo zinakafanya katambe, kanasema kana homuweki wakati mmi na wenzangu homuweki yetu ni kitandani nikirudi home namkuta wifi yako ananisubiri kuniongezea uchovu.

siandiki haya kujitetea na kupotosha lakini natamani uandike wengine ninaowafanyia kazi na wananilipa wanithamini, watambue kabisa nyasi nikifyeka nawaepusha na nyoka.

Sasa umeziona akili zangu za week days
 
Hivi tunataka kufanya biashara gani vile ebu ninong'oneze

...biashara ya simu sijawahi kufanya kwa kweli labda unifundishe. sasa fanya fasta kutuma namba ili nishiriki fursa. Afu unaonekana wewe ni mtu makini sana maana unaongea biashara, sasa mimi nimevuana korosho hapa unaweza kuniunganisha na wafanyabiashara wanunue, mimi narudisha mtaji faida unakula wewe 96 percent
 
Hapa ndo maana ulimwqmbiaa kimodo wako akaee pembeni wala asikugusee ushusheee nondooo...

Huyu ndo anko binamu akiwa hajatekwaa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…