Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mlio single jamani ujumbe wenu huo
Kuwa single ni kuwa mkamilifu, lakini watu wengi wanafikiri kuwa ni laana au kukosa bahati. Wanawake na wanaume wengi wanaishi kwa masikitiko wakifikiri kuwa hawana ngekewa ya kupata wenza.

Nataka nikupe mbinu mbalimbali za kukusaidia kufahamu upekee wako wakati ukiwa single. Kumbuka kupoteza muda ni kupoteza maisha. Ukiwa unafikiria kwa nini uko peke yako kama wengine ambao wako wawili wawili, utapoteza muda mwingi . Wekeza muda wako ili uwe na maisha mazuri. Fanya kazi kwa bidii , usipoteze muda wako kufikiri au kutaka kupata mtu wa kuishi nae kama muda bado haujafika , huwezi kulazimisha.

Msingi pekee wa kukusaidia wewe wakati ukiwa single ni Mungu peke yake. tafuta mahusiano na Mungu. Mahusiano ya mwanadamu yana mwisho , lakini ya Mungu yanadumu, hata siku moja hayajawahi kushindwa.

Ukweli ni kwamba ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu, Yatareflect mahusiano yako na watu wengine. jinsi ambavyo utawafanyia watu vizuri, utakuwa unamfanyia Mungu, Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi na wao waupendao watakula matunda yake. Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema.

Kwa hio kuwa single sio ugonjwa wala laana , ni wakati wa kujifunza mambo mengi, kujifunza kupika, kufua, kuwapenda watu, kujipenda mwenyewe na kumpenda Mungu. kujifunza kuwa na ujasiri, kuondoa woga.

Jinsi ya Kuwa Karibu na Mungu.

1.Soma neno la Mungu. tafuta maarifa mbalimbali, maarifa sahihi utayapata ndani ya neno la Mungu. Yapo maarifa mengi , lakini sio yote yanayofaa. kuwa makini na taarifa unazotafuta.

2.Uwe na silaha za kukulinda, kama kufanya maombi, kufunga kwa kumpenda Mungu sio kwa kutaka kitu au kwa sababu fulani.

3.Tumia Muda wako vizuri. ukomboe wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. tumia akili ipasavyo, usiwe kama mjinga asiyependa kujifunza. kujifunza hakuna mwisho. nenda semina mbalimbali, sikiliza CD mbalimbali za watumishi wa Mungu .

Kanuni iliyo kubwa sana katika maisha ya mwanadamu , itakayokufanikisha wewe mtu uliye Single ni Hii , Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. na ya pili ni hii, mpende jirani yako kama nafsi yako.
 
Nimeguswa na hii makala mm biblia haitoki chini ya mto kitandani nikiamka au nikilala lazima niifungue nisome mistari kadhaa

Asante sana numbii
Watu wengi wanafikiri kwamba maisha hayana fomula , sio kweli.

Maisha yana fomula yake. Ukitaka uwe tofauti na ulivyo sasa, ni lazima uifahamu fomula ya maisha.

Neno la Mungu liko wazi kabisa , Mpende Bwana Mungu wako Kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, kwa nguvu zako zote na kwa roho yako yote. Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Hakuna fomula inayopita hii. Ukikosa fomula hii utapoteza muda mwingi na kupoteza maisha yako yote.

Ukinunua simu utapata na kitabu chake, yaani menu yake. Mwanadamu pia ana kitabu chake, menu yake ni neno la Mungu, Biblia.

Watu wanalazimisha maisha bila fomula. Watu wajinga wasiotaka kujifunza hawana fomula. Mtu asijidanganye mwenyewe kuwa ni mwenye hekima Dunia hii kwa kufuata Elimu ya Dunia peke yake. Bora awe mpumbavu ili apate kuwa mwenye Hekima ya Mungu. Maana hekima ya Dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu.

Mungu hawezi kumpa mtu mjinga pesa, kwa kuwa pesa hio itamuua. Pesa ambayo umewahi kuishika inalingana na kiwango cha akili yako .

Sasa jiulize leo hii, unawezaje kuongezeka kama hauna fomula ya maisha?

Anza kuangalia mazingira yako , unamiliki gari nzuri, nyumba nzuri, smartphone, mke au mume mzuri, watoto au watoto na vitu vingine vingi tu, lakini huna kitabu chako cha Imani. Huna dayari, huandiki mafundisho ya neno la Mungu , Unakutana na changamoto kadhaa katikati ya maisha yako. Mungu hapo atakusaidiaje?

Umeoa umelipia gharama mwanamke milioni na zaidi , lakini umeshindwa kununua Biblia shilingi 25. Ndoa inaenda hovyo. Hapo Mungu atakusaidia vipi?

Stuka basi, anza kufikiri ili kiwango chako cha akili kiongezeke. Unaenda kwenye mafunzo huandiki, wakati wewe ni mjinga, na unafahamu kabisa kuwa ujinga wako uko wapi. Husomi vitabu na huendi semina, utatokaje?

Ndio maana Yesu alilia kwa ajili ya watu wasio na akili, watu wajinga. Akasema laiti hawa watu wangejua kuwa hawana maarifa ya neno la Mungu. Ndicho ulichokosa. Maarifa ya neno la Mungu. Fomula ya maisha umeikosa. Watu wangu wameangamizwa kwa kukosa maarifa.

Kanuni nyingine kubwa ni hii. Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo. Maana hio ndio torati na manabii.

Ukiona watu wanakufanyia vibaya wewe ndio uliyewafanyia hivyo, hapo unavuna ulichopanda, umekaribisha mwenyewe. Msidanganyike Mungu hazihakiwi , kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Kanuni ni Kumpenda Mungu. Weka thamani yako kwa Mungu, Kipaumbele chako kiwe ni Mungu kwanza. Maisha yanafuata baada. Fomula ya kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na Haki yake.

Iko hivi.

Ukimpenda Mungu utatumia muda wako vizuri katika kufanya kazi za imani. Kazi za imani ni kama zifuatazo.

Kazi za Yesu ni kuhusiana na watu, injili, kwenda kwa watoto yatima , wajane wafungwa, wazee na kuwatembelea wagonjwa na kuwaombea. Kufanya usafi na kuwafulia nguo watoto yatima na kuwasaidia kama unao uwezo wa kununua chochote, chakula, nguo, mahitaji yote ya mahali wanapoishi. Kama huna pesa toa muda wako tu. Utampendeza Mungu. Hii ni fomula.

Kazi ya Adamu ni usafi wa mazingira. Safisha bustani yako ya Edeni ili ikupatie Baraka. Edeni yako ni mahali ulipo sasa, kama ni Mwanza, Arusha, Dar, Dodoma, Nairobi, Kampala, , Kigali na kwingine kote ulipo unayesoma makala hii. Usitupe takataka ovyo, wala usiwe mmoja wa watu wanaokojoa kila mahali, hasa wanaume, msichafue ardhi, unachafua akili na ufahamu wako. Funguka kwa kufanya usafi.

Unganisha imani yako na neno la Mungu

Yakobo 1:27 neno linasema, Dini iliyo safi mbele za Mungu baba ni hii,kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao,na kujilinda na Dunia pasipo mawaa.

Mathayo 25:35-46 Neno linasema kwa maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula,nalikuwa na kiu mkaninywesha,nalikuwa mgeni mkanikaribisha,nalikuwa uchi mkanivika, nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia.,

Mwanzo 2:15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu , akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza.

Mathayo 28:16-20. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba na mwana na Roho mtakatifu…

Mungu atakupa Kazi, Ndoto yako, Maono yako, Biashara Yako, Maisha yatakuwa mazuri.

Lazima ujipange mapema, hujachelewa maadamu bado uko hai. Fuata kanuni hii utaona matokeo mazuri. Usiwe kama watu wasio na hekima bali kama mwenye hekima ukiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Anza kumthamini Mungu. Mpe Mungu kipaumbele kwenye kila kitu chako. Mshukuru Mungu kwa kila kitu. Usiwe mtu wa kulalamika, kunyoshea watu vidole, kusema serikali , kumsema raisi, acha!!.

Weka akili yako mezani. Usipende kuweka ugali tu mezani kwako. Hakikisha akili yako inatokwa jasho sio mwili utoe jasho kila siku.

Fuata fomula ya maisha utafanikiwa.
 
Chelsea 4
Cardiff 1
Chelsea-vs-Cardiff-City-Highlights.jpg
Screenshot_20180915-203438.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom