Koma kabisaaaa akusalimiee wewe...leo ni furahiday, kama huwezi kunipa Hi basi nipige mabusu ya kiarabu na kama umelewa basi nipige mabusu ya Kifaransa na usijali maana umeeleza kwenye Je Wajua kuwa ukipiga mambo yote hukumbuki, na sitakukumbushia.
Shikamoo msalimie anko wangu Lyon Lee
Nko poa binamu wkend vp...hellow sweetmoyo, hujambo mama JJ
...namba 8 ni muhimu, unakuta unaanzisha entity na unaipa jina Wamandavaku (unalikumbuka hili jjina la kina mandojo/Domokaya), utafanikiwa tu ikiwa utakuwa na upekee na mtaji wa maana usimame miaka mitatu mwenyewe ila kama ndo unaanza kutegemea 'watu' wadau basi kuwa na jina lenye mvuto, rahisi kutamkika kutakupa point nyingi za kukuweka kwenye biashara.USIANZISHE BIASHARA KABLA HUJAFANYA HAYA KUMI.
1.Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha sio tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla.
2.Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara.
3.Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha, usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine
4.Jitahidi kadri ya uwezo wako kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ambayo yatapelea kuharibu mtaji wako ulioanza nao.
5.Unapokuwa unafanya mpango mkakati wa fedha jitahidi matumizi yako uyawekee makadirio ya juu na kipato chako ukiwekee makadirio ya chini.
6.Kama unataka kufanya biashara na huduma ambayo kuna wengine wanafanya, hakikisha biashara yako iwe na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na watu wengine, na ujue wanakosea wapi na utafanya nini cha tofauti la sivyo utakuwa nyuma yao milele kwani kinachowavuta watu kuja kununa kwako ni utofauti kati yako na wapinzani wako na sio tu kwa kuwa bidhaa unayo.
7.Fanya utafiti sokoni kujua watu wanazichulia vipi bidhaa au huduma unayotaka kutoa ili kuweza kujua wapi unakosea na kujirekebisha mapema iwezekanavyo ili kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri na watu.
8.Hakikisha jina la biashara yako linamvuto na kukubalika katika jamii husika. Pia Jihusishe na watu mbalimbali walioendelea katika ujasiliamali ili uweze kupata mawazo mbalimbali na mbinu mpya za kuweza kufanikiwa katika ujasiliamali.
9.Andika! Mali bila daftari huisha bila habari. Daima tunza kumbukumbu zako katika maandishi
10.Tafuta kitu kitakachokuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa wakati huo katika eneo husika, ukitumie kama njia ya kujitangaza. ukifanikiwa katika hilo basi utajijengea channel kubwa na watu wengi watakujua na hiyo itakurahisishia safari ya kufahamika kwa biashara yako.
...kuna mtu alituma clip ya jamaa analisha nyoka (ni Whatsapp- simu yangu ina wasap-fyi) basi mwishoni lilikuja joka likajaa kwenye screen, sijawahi kutukana matusi kama siku hiyo.
Hata mm sijamuona kitambo,labda kabanwa na majukumu
acha kumkasirisha binamu bana
acha kumkasirisha binamu bana
Kwan hukuisoma ?Kikosi cha kisasi bwana aliweka season 1 akasema nyingine tulipie
Kwan hukuisoma ?
FAHAMU KONOKONO.
* Je wajua hakuna konokono dume wala jike ?
Konokono ni kiumbe hai asiye na uti wa mgongo, kama ilivyo kwa kobe, konokono pia huwa na gamba mgongoni kwake, gamba ambalo huuficha mwili wake pindi anapohisi mazingira ya hatari, kichwani kwake ana minara minne (antenna) ambapo Mbili za juu huwa ndefu kuliko za chini, pamoja kwamba konokono ana macho lakini ni dhaifu sana katika kuona, antena za juu ndio ambazo hubeba macho na za chini ni kwa ajili ya kuhisi kwani macho yake hutangulizwa mbele zaidi kuliko mwili, hivyo nafasi ambayo hubakia antena za chini ndio hufanya kazi ya kuepusha mwili kuingia katika tatizo.
Konokono ni viumbe wanaomiliki jinsia mbili yaani huyo huyo ni jike na huyo huyo ni dume, utajiuliza sasa inakuwaje kwenye nanii ! Maana najua niliposema tuu hivyo ubongo wako umepitiliza huko kwenye nanii ! Iko hivi si kwamba kwa umiliki wa jinsia hizo basi ndio hujitosheleza mwenyewe kimahaba, hapana konokono nao hukutana wawili na ambaye mwili wake utakuwa na joto ndiye atabeba jukumu la kutaga, kwa taarifa yako konokono hutaga mayai zaidi ya 70, chakula chao kikuu huwa majani hususani mboga mboga, matunda ikiwa ni pamoja na mimea iliyooza.
...kuna mtu alituma clip ya jamaa analisha nyoka (ni Whatsapp- simu yangu ina wasap-fyi) basi mwishoni lilikuja joka likajaa kwenye screen, sijawahi kutukana matusi kama siku hiyo.
Lakini si ni mkubwa jamani
Kwa mwendo konokono hutembea taratibu sana, na kutokana na mwili wake kuwa mlaini ili asiumie anapotembea hutanguliza ute ute chini, pindi anapouvuta mwili wake asipate kuumia, na ute ute huo hufanya kutengeneza alama ya njia aliyopita, konokono huwa na uzito wa gram zipatazo 5 na kuendelea, na urefu wao huwa inchi zipatazo 7 na kuendelea, ukiondoa hayo muujiza wa konokono ni kwamba ana maisha marefu huishi zaidi ya miaka 10.
Kimsingi konokono wapo wa aina tatu wapo wa nchi kavu, maji baridi na maji ya chumvi, maisha yao huathiriwa sana na viumbe wafuatao kwakuwa huwatumia kama chakula, viumbe hao ni pamoja na ndege,panya, Kobe,binadamu, mijusi nk.
Konokono mwendo wake ni taratibu sana mpaka sasa hakuna ushahidi wa kutosha kuonesha kwamba kuna konokono aliyewahi kuvuka salama barabara, mwendo wao ni wa kusua sua sana, utafiti unaonesha ya kwamba ili aweze kumaliza umbali wa kilometer moja anahitaji wiki moja na siku mbili.
SIFA ZA KONOKONO.
1. wana uwezo mzuri wa kutizama usiku kuliko mchana.
2. Ni ngumu sana kujua jike ni yupi na dume yupi hiyo yote ni kwa sababu jinsia zote kila konokono anazo.
3. Konokono anapotaga baada ya kutotoa, magamba ya mayai hula na ambayo hayatatotolewa huliwa na watoto wake.
4. Konokono hawasikii kabisa, hivyo hujiongoza kwa kunusa .
5. Ukimmwagia chumvi konokono anayeyuka kabisa na kupotea, hivyo kama wamevamia kwako mwaga maji ya chumvi tuu.
6.konokono huweza kutembea gamba lake akiweka juu au likiwa chini na akatembea pasina ya tatizo lolote.
7. Kiumbe huyu pengine ndiye mwenye meno mengi kuliko wengine, watafiti hudai ana meno yanayozidi elfu moja.
8. Konokono ni kiumbe asiyekula nyama kabisa, hivyo akikupanda mwilini kwa bahati mbaya mtoe kistaarabu hawezi kukuuma.
9. Konokono hupendelea mazingira machafu na yenye giza yenye unyevu nyevu.
10. Konokono huweza kuufupisha mwili wake ajifichapo katika gamba lake, na baada kilichosabisha ajihami kutoweka hutoa tena mwili wake.