Makapuku Forum

Melania Trump kuzuru Afrika. "Hii itakuwa safari yangu ya kwanza barani Afrika kuondoa shauku yangu kubwa na kujifunza masuala yanayowahusu watoto na vilevile kujifunza juu ya utajiri na utamaduni na historia ya bara Afrika
 
Mawakili nchini Chad wamekwenda mahakamani, kupinga marufuku hii ya mitandao ya kijamii.

Imepita miezi 5 sasa tangu serikali ya Chad kuzima ghafla kwa matumizi ya mitandao ya kijamii nchini humo.

Mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Twitter na mitandao mingine, hazipatikani kabisa nchini humo.
 
Polisi nchini Uganda wamewakamata watu 45 kwa kufanya vurugu jijini Kampala.

Wafuasi wa Bobi Wine walijitokeza barabarani wakitaka serikali imuachie huru mbunge huyo wa Kyadondo anayedaiwa kuwa katika hali maututi
 
Watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuwa watoto wazazi wao walivuta sigara mbele yao,wana hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na maradhi ya mapafu.
 
Rais Vladimir Putin wa Urusi alihudhuria harusi ya waziri wa Austria
Ziara yake imeibua hisia kali miongoni mwa viongozi nchini Austria wakimlaumu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Austria bi Karin Kneissl kwa kuhujumu sera za kigeni za Ulaya kwa kumualika.
 
"Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu."

Methali 3: 24

Mungu awatunze usiku huu,Malaika walinzi waweke kituo kila nyumba,Damu Takatifu ya Yesu Kristo itufunike
Usiku Mwema
 
Hivi gharama ya kupata passport kwa sasa ni shilingi ngapi? Makapuku tujuzane

1. Nikijiaminisha unamaanisha hii hati ya kusafiria, basi gharama imepandishwa toka 50k hadi inasoma 150k


Hapo bado gharama za fomu ambazo ni kama 20k.

Tembelea web ya Uhamiaji wameifanya iwe poa sana

2. Kama unamaanisha hizi passport size bei yake ni tofauti tegemeana na studio. Hapa Mtwara unatoa 1k unapewa passport 6 kwa mpigo bahati mbaya hawakupi negative.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…