Makapuku Forum

Makapuku Forum

Binamu shikamoo
Asante sana Tumosa kwa kuonesha namna wapishi wanaume tunavyokuwaga makini katika upishi, hasa kwenye kukaangakaanga na vitunguu.

Nimekuja na ninafurahi kuona wadau wamejaa tele.

Vipi, kuna jipya?
 
Jioya lipo binamu Da vinci kapata mbebez
 
Tafasiri Unavyoweza: Vibarua Pekee Hawaendeleze Miradi, Elimisha

...miaka michache iliyopita Sugu, mbunge wa Mbeya Mjini alishauri, kama utani kuwa ingekuwa sawa sana kama rais wetu angepata nafasi ajipe muda wa kutembea kidogo kwa jirani na marafiki wa nchi yetu. Baadhi ya watu walimshambualia na kujisifu kuwa rais wetu ana kazi ya kunyoosha nchi na marafiki na majirani wao ndo watakuwa wanamfuata maana ni rais 'bora' aliyetrend mtandanoni kiasi kwamba TBC ikanukuu khabari feki ya kumsifu rais wetu. Hatuko kisiwani, ni lazima tushirikiane na kushindana na nchi nyingine (a need to cooperate while competing at the same time).

Ushindani na ushirikiano ndo mtindo wa maisha wa nchi na dunia ya sasa, mataifa yanashirikiana na kushindana katika kuvutia wawekezaji, kupata mikopo na misaada mingine ya kuwaletea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi. Dunia ya sasa siyo ya kuwaandaa wananchi wako kuwa vibarua kwenye miradi ya ujenzi. Hili la vibarua sijalitunga mimi, ninamnukuu rais akisema kuwa wapo vibarua wa kutosha kukamilisha ujenzi wa daraja na miradi mingine. Huu no moja ya 'upuuzi' ambao ukiachwa bila kuongelwa utaleta madhara huko mbele.

Sitaki kuamini kama rais anataka sisi tuwe taifa la vibarua, miradi mikubwa anayojinasibisha nayo haitakuwa na maana kama waliyoijenga na kuikamilisha wataondoka na kutuachia sisi. Hakutakuwa na mtu wa kuisimamia na kuiendeleza, itakufa na hivyo ni wakati sahihi kwa rais na utawala wa sasa kuhakikisha vibarua wanageuzwa na kuwa wataalamu kwa kupewa utaalam na elimu ya kuendeleza yaliyopo na kuja na mawazo mapya. Dunia ya sasa ushindani ni wa akili (ideas) kwani miundombinu si kusimika majengo na madaraja au kununua ndege bali ni namna ya kuendeleza miradi hii na kesho ikawepo. Tafasiri unavyoweza
 
Asante binamu

Muziki: Utulivu Kama Talaka

....sijui hata nataka kuandika nini, nilipolalia leo nikirudi nitapaangalia tena maana kila nikiandika nafuta, well, sio mbaya labda nianze kwa kukusalimia wewe Kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Napapenda hapa kwa sababu yako wewe na unalijua hilo na hata kama hutataka kujua hali yangu basi nitakueleza kuwa niko salama sana na nimekuja tena hapa muda huu. Hapa ni sehemu inayoniongezea maarifa, inayonifanya nijue watu na kujifunza mengi, najifunza mengi sababu kubwa ni wewe Kapuku.

Ni kutokana na sababu ya wewe kuwepo hapa ndiyo maana jukwaa hili litaendelea kuwepo maana wewe unaleta madini adimu hapa na hata ukiondoka basi anakuja mwingine na madini mengine sio makinikia. Nimesema hata sijui naandika nini sasa wacha nikuburudishe tu na muziki. BTW, hongera sana mdau Da'Vinci na sinyoritah kwa hatua mnayoianza, nawakumbusha tu kuna talaka tulivu, haina makeke wala vitimbwi mkifikia hatua ya kuitafuta

Similar Discussions

Back
Top Bottom