Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Elimu Ni Kazi, Ipatikane Kiurahisi

...hakuna ukweli kwamba isipokuwa tu labda umezaliwa kwenye familia ya mabilionea, wengi wetu tunaisaka elimu, iwe ya juu, kati au kawaida kwa ajili ya kupata sifa za kuajiriwa. Ndiyo, utasikia wanasema vinginevyo lakini huu ni ukweli na hata ukiamua kuuzika kwa kusema vinginevyo utafufuka kwa shwangwe na utaona na wengi wala si wachache. Elimu ya juu na kati ni uwekezaji mzuri kwa mtu binafsi, familia na jamii kwa upana wake. Fada za elimu/maarifa haziishii kwa aliyefaidika nayo peke yake, zinasambaa kama tambazi. Tafasiri Unavyoweza.

Ninaandika kuhusu elimu leo sababu kubwa ni kuwa matokeo ya kidato cha sita yametoka, ufaulu umepanda na bahati nzuri shule za umma zimefanya vizuri na nyingi kufanya madudu kama kawaida. Madudu kama kawaida sababu hakuna uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kutoa elimu kwa vijana wa taifa hili. Ndiyo. Waliofanya vizuri kwa sasa wao na walezi wao wanajipanga kusaka vyuo ambavyo bila ubishi vimekuwa ni aghali. Elimu ni gharama lakini kiacha mikopo ya serikali ambayo haitoshi, ni wakati wa serikali kuangalia namna ya kuifanya elimu ya juu kuwa bora na yenye unafuu, isiyomuacha mzazi na mlezi akiogelea kwenye dimbwi la madeni baada ya shule.

Plato alisema maarifa i chakula cha nafsi, elimu inatoa maarifa unayohitaji kuyakabili maisha katika uso na kisogo chake. Kwa sababu chakula ni hitaji la msingi kwa binadamu basi wale wanaotaka kusoma elimu ya juu wasiwe na kikwazo cha ada ndefu za shule na zaidi hatuongelei elimu bure, tunaongelea elimu nafuu na gharaa za elimu ziwe rafiki kwa wingi. Tusitengeneze kundi la watu wanaoshindwa kutimiza ndoto zao za kusaka maarifa sababu tu gharama hata wakinyanyua makwapa na kusimamia vidole hawazifikii. Tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Jumanne Baada ya Jumatatu

...hakuna ubishi kuwa hizi siku zinafuatana sana, hazipishani, yaani ukisikia leo ni Jumanne basi ujue kesho ni Jumatano na jana ilikuwa jumatatu. Ndivyo ilivyo na kama kawaida yangu kukusalimia wewe kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri sitaacha maana ni jambo zuri. Nikushukuru sana Iyegu kwa kulinogesha jukwaa kwa post tofauti, asante mdau na hata kina sisi watembea usiku, asubuhi tunakusoma bila shida.

Muziki sasa, wengi wetu tumeshatoka kwenye vibarua vyetu na kama sio foleni basi tumeshafika nyumbani na ikiwa wewe ni kama anko wangu Lyon Lee basi uko sehemu unachangia pato la taifa kwa kukaa pub ukigonga moja moja pembeni umepakata asiye wako, mjomba wangu huyu aachwe kama alivyo.

Binamu shikamoo asante kwa music

Obe Iyegu Ni Jina La Kijiji Nilipozaliwa, Kukua Na Kusomea.

Kipo Kata Ya Mlali, Wilaya Kongwa Huko Mkoani Dodoma.
 
  • Thanks
Reactions: Obe

Similar Discussions

Back
Top Bottom