Makapuku Forum

Makapuku Forum

Binamu asante
Tafasir Unavyoweza: Msongo Haukimbiwi

Karibu tena hapa, usidhani naishi kwenye dunia ya peke yangu. Unayopitia nami ndo napitia, tunatofautiana kiwango tu. Kuna wakati unakuwa na furaha na wakati mwingine unakuwa na upweke. Sio upweke kwa sababu unakuwa peke yako huna kampani, la ni upweke wa akilini. Huu ndo unaitwa msongo kwa taarifa yako. Msongo ni hali ya kihisia (emotional) ambayo huja kwa sababu ya kunia, kuwaza kulikopitiliza (demanding circmustances). Msongo kwa ufupi hunyong'oza na kumfanya mtu mtupu. Msongo huleta magonjwa na ni hatari kwa afya ya akili.

tunatofautiana sana katika kukabiliana na msongo, hii ni kwa sababu kila mtu ana msongo au misongo yake. Wanaume tunatofautiana sana katika kukabiliana na msongo, wengi wetu huamua kupambana na msongo kwa kujaribu kupambana nao badala ya kuutatua. kupambana na msongo utashindwa wewe, tafiti zinaonesha hivyo. usijidanganye kushindana nao (fight) na ndiyo maana tunaposhindwa huamua kuukimbia (run/flight). Ushahidi unao ulipo, wanaume wengi ndo wa kwanza kukimbia nyumba zao, na wengine kama wasipokimbia basi huwa walevi 'mbwa'.

Kwa wanawake ni tofauti, wao huukabili msongo kwa namna ambayo huushinda msongo mara nyingi, moja, wao hujipa muda kuujua chanzo na kisha hujichanganya na watu wengine, hueleza kinachowasumbua kwa marafiki zao na ndiyo tiba yenyewe. tafasiri unavyoweza.

pambana na msongo kwa kuweka wazi kinachokukabili, kuishi na msongo kunaumiza na kunakufanya kichaa mwenye jina. tafasiri unavyoweza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom