Makapuku Forum

Muziki: Nunua Unachohitaji

Ninakusalimia Kapuku mwenzangu na nikwambie tu kitu kimoja ambacho asilani sitakaa niache kukisema. Wewe ni mtu muhimu, ndiyo, wewe unayesoma hapa unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Ninatumaini umekuwa na wakati mzuri, binafsi yangu nimekuwa na wakati mzuri sana, asante kwa kutouliza.

Tumekuwa na kawaida ya kufanya manunuzi, uchumi unakuzwa kutokana na manunuzi hivyo kufanya manunuzi = kukuza uchumi. Changamoto kubwa ni je manunuzi haya tunayofanya tunayahitaji? Wapo baadhi yetu wanashida ya kununua hata wasivyohitaji na si ajabu ndani anakuwa na makorokoro mengi na wala kuyagawa hayahitaji. Hii si sawa, fanya manunuzi kwa kile unachohitaji na kama kuna kitu hukitumii basi kigawe kwa muhitaji angalizo usigawe kilichochakaachakaa sana au ulichojaza viraka.

Muziki sasa, burudika na ninakutakia Ramadhani njema hata wewe ambaye huishiriki.

 
Binamu asante
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…