Makapuku Forum

Makapuku Forum

Binamu unashkuru vipii jioni jamani mda wote ulikuwa wapi shikamoo kwanza

...sikuwa na data, ndo nimeweka bando muda huu nikaona nipitie kwanza MF nijue na bahati nzuri nikakuta umeweka magazeti ndo nikaona hakuna ubaya kusema asante, si unajua ndugu yako mimi sio mchoyo, wa asante.

Marhaba, ngoja nijiandae niandike kitu kifupi tu.
 
Sawa binamu
 
Obe..

Hebu nitafutie huu uzi mkuu.
20180524_184403.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafasiri Unavyoweza: Kutegemeana Si Utegemezi

Kila mtu na mteja wake. Usidhani ninaongelea masuala ya huduma na biashara hapa kwa kusema kila mtu na mteja wake. Mteja kiurahisirahisi inaweza kuwa inahusiana zaidi na masuala ya kibiashara au huduma kama za kisheria, mahakama, polisi, elimu kifupi mteja inahusiana na malipo ya huduma. Sasa liangalie neno mteja kwa jicho jingine, jicho la kutegemeana baini ya watu wawili au zaidi/kikundi. Mfanyakazi anategemea mwajiri wake atimize wajibu wake kwake na mwajiri vile vile anategemea mfanyakazi atimize majukumu yake. Maisha ya leo ni ya ya nipe nikupe na ukiyafanya ya upande mmoja tegemea kuwa peke yako. Tafasiri unavyoweza.

Kuna kanuni kubwa na muhimu sana ya mahusiano, iwe ni ya kifamilia au kijamii. Kanuni hii inasema kuwa watu/mtu hutegemea malipo kwa kile wanachofanya (law of reciprocity-people expect to get paid back for whatever they do for others). Mpiga kura anapopiga kura na kumchagua kiongozi anamtegemea kiongozi awezeshe miondombinu ambayo itamsaidia mwananchi kujikwamua na umaskini. Hategemei baada ya kupiga kura na kiongozi kuchaguliwa basi kiongozi anabaki kutoa amri na kuzidi kubomoa daraja kati yake na mwananchi.

Kama ilivyo kwenye mahusiano baini ya watu wanaoishi pamoja ambapo hujengwa kwa wawili kila mmoja kutoa asilimia mia ya alichonacho kwa mwenzake basi wanasiasa nao wanapaswa kupunguza umimi (ubinafsi) na kujitoa kwa wananchi na wasiwalazimishe wananchi kujitoa kwao bila wao watawala kujitoa kwa wananchi. Usitegemee kupata haki kwa kiongozi ambaye kila kukicha anajiongezea ulinzi nyumbani kwake, mageti makubwa, askari wenye silaha za moto na mbwa wakali, huyu ni tegemezi kwako, anakuibia na maneno yake usiyaamini hata kama anaongea kuhusu kutegemeana. Tafasiri unavyoweza.

Hadi wiki ijayo tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom