Makapuku Forum

Muziki: Heko ya Kuzaliwa shululu

Nafurahi hujaandamana barabarani leo, ni jambo zuri kufanya kilicho sahihi kwako na ndiyo maana Tumosa aka mama JJ kaamua kumtunuku shululu wimbo mzuri siku ya kukumbuka kuzaliwa kwake. nami ninakusalimia kapuku na kukutakia wakati mzuri wakati ukitafakari siku ya Ijumaa itakavyokuwa.

Burudika na muziki na tumtakia Shululu heko ya kuzaliwa

Asante binamu naamini baba wawili na makapuku wote wataburudika kwa wimbo huu mzuri
 
Happy birthday to u mzee mwenzangu, mhenga mwenzangu, mshika bunduki mwenzangu, jirani yangu, swahiba wangu, ndugu yangu, kaka yangu...

Allah akupe kila lenye kheri kaka, akutie imani, akuongoze njia ya wale aliowaongoa, afanikishe ndoto na malengo yako, akupe afya madhubuti, baraka zake na rehema zake zisizo na mipaka ziwe juu yako kiongozi..
 
...falsafa hii. Asante.

Ravalomanana alikuwa na jeshi lililomlinda, akawazuia wananchi kufanya haki yao aliingia topeni
Ndio tatizo la kujikuta ww ni mjuvi wa kila jambo unahisi utaleta mambo ambayo yaishawahi kutimia katika mtindo mpya.. Jambo ambalo halipo na halitoweza kuwepo

Kama mwenzio alichafuka kwa tope, usitegemee ww utasafishika kwa tope.
 
Tafasiri Unavyoweza: Maandamano Yamelipa

Hakuna ubishi kuwa leo maandamano yamefanyika, ndiyo yamefanyika tena kwa kiwango kikubwa sana. Maandamano haya unaweza kuyatafasiri unavyoweza nami nitakueleza kuwa wakati wewe ulikaa ndani leo polisi wengi kwa karibu wiki nzima hii walikuwa wakiandamana (wenyewe wakiita mazoezi) kumuunga mkono dada jasiri (hata kama hukubaliani na baadhi ya mbinu zake za kuwasilisha ujumbe) Mange Kimambi. Ukiwaacha polisi walioandamana kwa wingi sana, raia wengi walikuwa na ufahamu wa tukio la maandamano ya leo na kwa kuunga mkono maandamano haya waliandamana kifikra. Tafasiri unavyoweza.

Ujumbe umetumwa na umefika kikamilifu, ni bahati mbaya sana kuona rais na serikali inayojinasibu kufanya mambo mazuri inakuwa katika nafasi ya kujihami zaidi kuliko kujitokeza nje na kusikiliza yale ambayo yanasemwa kuwa haifanyi. Haki ya kujieleza kama ilivyo haki ya kuandamano na mikutano ni kitu kilichokubaliwa ndani ya katiba, si hisani ya rais, au chama kilichoko madarakani. Ni ushamba mkubwa kudhani kuwa mtu mmoja au kikundi cha kisiasa kinaweza kuamua tofauti na katiba. Ni suala la muda tu, bubu atasema kwa kupaza sauti na hapo ndo walioshika madaraka watapazwa kwa kasi ya kobe, waugulie maumivu kwa kila hatua. Sio utabiri huu ninaoandika, naandika utafasiri unavyoweza.

Asanteni sana jeshi la polisi kwa kuandamano na kumfanya Mange na hoja zake ziwe na mashiko, bahati mbaya sana wakati mnaandamana hakukuwa na chombo kingine cha kuwazuia kuandamana
:D :D :D :D haya binamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom