Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,324
- 35,833
Tafasiri Unavyoweza! Akili Ni Kuhoji Sio Kunyamaa
Hakuna ubishi kuwa zama zinabadilika sana, hata walio ndani ya boksi wanapata nafasi ya kunyanyua vichwa vyao kuona ndani ya boksi kuna nini maana kila siku wanaambiwa kutazama nje ya boksi. Ukweli ni kuwa huwezi kuona kilicho nje ya boksi kama kilichomo ndani ya boksi ulimokaa hukijui. watu sasa wanahoji maana wanauelewa wa mengi, huwezi kukaa unawadanganya maana huwezi kuwadanganya watu wote muda wote. Tafasiri Unavyoweza.
Kuna viongozi kila wakifungua vinywa vyao baada ya kula mapochopocho kwenye majumba tunayowalipia kukaa hawaishi kusema yanayowafurahisha na kulinda maslahi yao pekee na si vinginevyo. Wanaenda mbali zaidi na kutaka kutufundisha namna ya kufikiri. Hawataki tusome na tuhoji, wanatamani kuongoza malaika ili watufanye sisis kondoo, ttusioweza kuinua vichwa na kuangalia mbele kuna nini ikiwa wao wametangulia.
Wanatumia pesa kwa utashi wao bila kuleta mrejesho na mbaya zaidi wanatumia pesa hizi kwa manufaa yao binafsi na kutuletea viswahili vingi tukitaka kujua matumizi mapato yaliyofanya. Tukatae ukondoo, tuwe na shauku ya kuhoji maana kuhoji ndo akili vinginevyo ukimya wako ndo hasara yako na kiama ya kizazi chako maana kizazi cha kiongozi kinafundishwa kuendeleea kukuibia na kukuongoza.