Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Tafasiri unavyoweza na muziki zitakuja kwa kuchelewa sana.
 
Muziki: Ijumaa na Wikend Njema

Ninakusalimia sana mdau wa ukweli, nikupongeze kwa kuifikia Ijumaa ya leo ambayo ni mwanzo wa weekend. Inawezekana una mipango mingi sana ya kibinafsi, basi ipange ipangike na maisha yaendelee. Binafsi nina mambo yangu ya binafsi tofauti kabisa na yako.

Muziki, sitaongea mengi sana maana wikend ni mwendo wa kinywaji, mishikaki na kukaa kimwili zaidi

Shikamoo binamu,leo ni barukutu day eeeeh
 
Kila la kheri binamu ukumbuke tu kurudi nyumbani ucjetekwa na akina mama muuza

...ha hahha, siwezi kutekwa sema itabidi nikaonane na mama muuza mmoja nikamweleweshe kkuhusu upotevu wa tilioni 1.5, kama nikimaliza mapema basi itakuwa ni jumapili. Nitaenda kufanya ufafanuzi na huku nikidadavua ripoti yote
 
Shikamoo binamu
 
Tafasiri Unavyoweza: Kondoo Mwenye Kengele

Jamii za wafugaji zina kawaida ya kuwa na mifugo mingi na katika mifugo hii, mfugo mmoja huvishwa kengele kama ishara ya kiongozi. Kitendo hiki ni maarufu kwa wale wafugaji wa mbuzi na kondoo. Hapa beberu hili huwa ni kama kiranja, hutangulia mbele na wengine hufuata. Mfugo huu huwa na sifa nyingine ya ziada ukilinganisha na mifugo mingine, huwa na kiburi, akiamua kupita njia fulani basi wengine hawana namna lazima wafuate. Tofauti ya mifugo yenye kiranja wa namna hii na binadamu ni kuwa binadamu ana utashi wa kukubali au kukataa na hasa akiwa amechakata taarifa sahihi na kufanya maamuzi, tafasiri unavyoweza.

Ubabe wa baadhi ya viongozi wetu bila kupindisha maneno unamaana moja tu kubwa, ni wezi. Ndiyo, ni wezi, polisi na wanausalama wanajua lakini kwa kuwa madaraka wanayashikiria kikatiba basi wanausalama hawana jinsi zaidi ya kuendelea kulala kitanda kimoja na wezi. Kiongozi mwizi utamjua tu, yaani kama ilivyo kwa yule kondoo mwenye kengele, kiongozi mwizi utamjua tu kwa ubabe wake, kiburi na kudhani kuwa anajua kuliko mwingine. Ukimshinda kwa hoja atawanyanyua viongozi wa majeshi na kuwaagiza wawakamate 'wakorofi' kwa kutaka kutia kitumbua mchanga.

Tafasiri unavyoweza, Mtanzania ana kichwa na kichwa chake hafugii nywele tu, anakitumia kufikir, kitendo cha kiongozi kujidai wanafikir kuzidi wengine wanajidanganya. Mageti wanayoongeza kwenye makasri yao hayawezi kuzuia wananchi wakiamka, hayawezi kuzuia kelele za mabubu wakiamua kusema, malango hayatazuia vipofu kuona wapi pa kupita. tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Wiki Yenye Tabasamu

Sitaandika kitu kingine nikishamaliza kukusalimia kapuku mwenzangu, nitakuacha uburudike na muziki kama ilivyo kawaida ya kipengele hiki

Back
Top Bottom