Makapuku Forum

Makapuku Forum

Binamu obe Mungu akupe nini nasikia mvua ilikukuta gest mpaka leo simu haipatikani ...muhimu wababadilishie mashuka

...ha hahah, anko bhana, hii mvua ndo utajua kwanini mke huitwa Jiko, wazee wa zamani bhana ila kwa msio na wake nawasalimia na kuwatakia wakati mzuri mwakani mkiitwa na wakuu wa mikoa yenu.

Anko nasikia RC Maokonda anakutafuta, amekutamia summons iko kwa mama mjumbe yule uliyemzalisha mapacha ukagoma kupima kisa ni Definitely Not Attractive (DNA)
 
Tafasiri Unavyoweza: Jamii Hojaji Haifi Hata Ukinyamaza Wewe

CAG kamaliza uhakiki wake na tuliyoyasikia tumeyasikia. Makusanyo yamekaa vizuri, matumizi yamejaa 'wino damu' (walimu huwa wanatumia kalamu ya wino mwekundu kuonesha kilichowatatiza), matumizi makubwa tu ya serikali hayana vielelezo, kiufupi kama hutaki kujisumbua na utabaki kuwa mkweli ni kuwa mpunga mrefu sana umepigwa na wajanja na siku zote tunamjua mkuu wa serikali ni nani, na kwa maana hiyo mlaji aliyekula hizi hela huhitaji kujifikiria sana au kupoteza muda kuchunguza nani kazipiga hizi hela. Tafasiri unavyoweza.

Ni bahati mbaya sana kama taifa kuna mambo tunayapuuza, kiukweli tumekuwa ni taifa la wapuuzi. Hatuhoji na hata wanaojitokeza kuhoji tunawapuuza na wakati mwingine tunaenda mabli zaidi kwa kuwapa majina ili tupate sababu ya kuwapiga risasi au kuwabambikizia kesi na kuwatesa. Kuhoji ni kutaka kujua, hakuna furaha ya kuwa mjinga au mpuuzi, anayepuuza atapuuziwa na ukikaa kimya usijedhani uko salama.

Tunakoelekea tutafika tu, kujidai kuwa hawa ni bora zaidi ya hawa itatoa majibu muda si mrefu pale watoto wanaozaliwa leo wenye akili za nyoka, wajanja, wanaohoji wanaojua kusoma kabla ya kuingia darasani watakapokaa vifua wazi kuhoji kwanini kuna madhamani tumewaamini kulinda kibubu tunachokichangia lakini wanajiona wao wana haki ya kula na kutudhihaki wote wenye midomo iliyopauka kwa njaa ya kukosa huduma muhimu za msingi tunazostahili kama wana wa nchi hii. Tafasiri unavyoweza
 
Kwani haupo dar

...kakimbia, anasubiri hili joto na mvua la kufuatilia watelekezaji ili watekeleze majukumu yao mahususi liishe. Yaani pale kwa RC kulikuwa na watoto kama idadi timu ya basketiboli. Nilipokuwa nikiwaangalia tu macho yao tu nikajua anko wangu kwanini siku hizi anavaa miwani myeusi
 
Huyu ndo binamu kabisa mtoto wa ndugu yangu
 
...hapa anko ndo unaharibu ujue hii ilikuwa siri yetu sisi ndugu. Sasa mimi nikileta ile picha inayosambaa kwenye whatsaap ikimuonesha yule dada uliyempangishia chumba na bado kaenda kutaka matunzo Ilala boma
Kama mbwai iwe mbwaiii binamu nimejipangaaa...leta nileteeee ulichomfanyia wa tangi bovu
 
...kakimbia, anasubiri hili joto na mvua la kufuatilia watelekezaji ili watekeleze majukumu yao mahususi liishe. Yaani pale kwa RC kulikuwa na watoto kama idadi timu ya basketiboli. Nilipokuwa nikiwaangalia tu macho yao tu nikajua anko wangu kwanini siku hizi anavaa miwani myeusi
Binamu nakusalimia sana na nina mazito yakoo moyonii
 
Back
Top Bottom