Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Harufu ya Mvua

...nawakumbusha tu Makapuku, msipuuzie taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa, zitasaidia kuwaunganisha walioachana.

Muziki sasa, burudika mdau mwenzangu wa jukwaa hili adhimu

Tfasiri Unavyoweza: Hoja Hujibiwa Kwa Hoja Si Vioja

...ni Jumatano leo, ndiyo, nakukumbusha tu kama mambo yaliyotokea wiki hii tunayoigawa kati leo yamekuchanganya. Kuna mengi yametokea, mazuri na yapo baadhi ya kukarahisha ambayo kama tusipoyasema maana yanafanywa na wale tuliowapa dhamani ya kutuongoza kama taifa. Uteuzi wa majaji kwa mfano, chapuo limepigwa kwamba ni kwa ajili ya kuharakisha kesi, hili ni jambo zuri na uwingi wa majaji unaweza usiwe unawakilisha ubora wa majaji. Siwezi kuwa jaji wa jaji, kama unanielewa lakini inakuwa ni tatizo pale unapoteua jaji kwa misingi ambayo inaonesha kabisa kuna namna fulani ya upendeleo kwa misingi ya kikanda, udugu, udini na hata mahusiano baini ya mteua na mteuliwa. Nafasi ya Ujaji si nafasi ya mtu kulipa fadhila, chezea yote lakini nafasi ya jaji na elimu ni vitu usivyopaswa kuviangalia kijuujuu. Tafasiri unavyoweza.

Hoja ijibiwe kwa hoja na sio kujibu hoja kwa nguvu au kwa vioja. Mbunge Zitto katoa uchambuzi wake wa taarifa ya CAG, taarifa iko wazi, kama taifa madhamana wametupiga 1,500 billion na hawataki tuhoji, mwenezi wa CCM anaenda mbali zaidi na kutaka mbunge akamatwe kwa kutoa taarifa za serikali ya kutumbua tilioni za umma bila maelezo. Tabia hii ndiyo inashamiri sasa, tumekuwa na serikali inayojihami kwa nguvu za dola isivyo kawaida, haijapata kutokea. Je, awamu hii haina watu serikalini wenye uwezo wa kujenga hoja za ukweli na zenye kuaminika? Mbona ndiyo serikali inayoongoza kwa kuwa na teuzi nyingi za wasomi viwango vya uzamivu?

Vioja vya mawaziri na wasemaji wengine wa serikali na hasa vikianza kuwapa wanaohoji majina ni upungufu wa akili, dalili za mwanzo kabisa za kuwa na viongozi wapumbavu, viongozi wazima shingoni kushuka chini na wafu shingoni kupanda juu. Hoja ijibiwe kwa hoja, tuambiwe hii serkali inayojinasibu kupambaa na ufisadi, ndani ya mwaka mmoja tu imetupiga wananchi tilioni za kutosha, hizi pesa ziko wapi?
 
Muziki: Mapuuza Yasiyo Puuzwa

Ninakusalimia Kapuku mwenzangu, nikikupa pole ya mihangaiko ya siku nzima ya leo, kwa wale ambao giza limeshaingia na kwa wale wote ambao ndo kwanza ni saa nne asubuhi basi nikutakie kazi njema. JF ni bahari, wengine leo ni alhamisi ni mwaka 1439. Uzuri ni kuwa wote tupo humu na tunaifurahia JF na hasa makapuku forum, forum bora kabisa kwa sababu wewe upo.

Muziki sasa, usipuuze yasiyopaswa kupuuza, chukulia kila kitu kwa umakini unaotakiwa. Kuna puuza nyingine huzaa tatizo au shida kubwa usipochukua hatua. Nakupenda mdau mwenzengu na kukutakia wakati mzuri.

Shikamoo binamu
 
Back
Top Bottom