[emoji524]TUOMBE
Baba MUNGU Wa mbinguni katika jina la YESU KRISTO , tunazileta shukrani zetu kwako eee Baba ,, tunasema ahsante kwa kutuamsha salama ,leo ALHAMIS tarehe 1 MACHI 2018, Mungu umetulinda usiku mzima na mwezi mzima wa pili.
Umetuponya na kutuokoa na kazi za adui yetu ibilisi ,,zaidi ya yote BWANA YESU umetupatia ushindi juu ya maadui zetu ,
Ahsante BWANA YESU , kwa Neema yako , kwa upendo wako , na rehema zako
MUNGU WETU UISHIE MAHALA PA JUU KABISA KATIKA JINA LA YESU tunaomba Mungu utusamehe dhambi na maovu yetu , utupe Neema ya kuwasamehe wale walio tukosea sisi pia ,
Tunaomba utuongoze katika njia zako eee Bwana , tusaidie tupate kuyatimiza mapenzi yako Mungu ,
Tutangulie maofsini na katika njia zetu BWANA YESU ,
Neno lako likawe ni mwanga na Nuru ya miguu yetu ,, tunaomba BWANA YESU ukafanyike Baraka kwetu , ibariki siku hii ya Leo BWANA ukaifanye itutumikie ,
Bwana Yesu tunaomba utuponye katika kila jambo ,damu yako itufunike na kutulinda ,, ROHO MTAKATIFU TUFUNDISHE KATIKA KWELI YOTE NA HUO UKAMILIFU ,
Tumeomba yote na kuamini katika jina la YESU KRISTO ,,Amen[emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji1374]
NAWATAKIA MWEZI WA BARAKA WA MACHI KWETU SOTE.