Tafasiri Unavyoweza: Jiji la Mafukara, Wekeza Kwengine
Nilipofika jijini kwa mara ya kwanza nikagundua kumbe chipsi ni viazi. Jiji huvutia wengi, wasomi na wasiosoma, matajiri na mafukara. Jiji lina miundombinu rafiki kwa wengi, maji ya uhakika, umeme, barabara nzuri, kazi na waajiri wengi wapo jijini, huduma za hospitali na nyingine za kijamii. Zote hizi hupatikana kwa urahisi jijini.
Kutokana na kuwepo kwa watu wengi jijini, tuseme kwa mfano jiji la DSM, hili linaidadi kubwa ya watu kulinganisha na eneo lake la kijiografia. Unaweza kujiuliza kwanini watu wanakimbilia DSM, yapo mengi, vyuo, shule nzuri, huduma nzuri za kijamii, miundombinu rafiki kwa maisha ya mtu wa karne hii kutaja machache.
Kiukweli kama kuna jiji linalovutia maskini kuishi basi DSM inaongoza, tafasiri unavyoweza. Na ni lazima ujue kuwa jiji haliwafanyi watu kuwa maskini ila watu maskini hukimbilia jijini kwa sababu kuna fursa kulinganisha na sehemu nyinginezo au miji nchini. Fursa za kufanikiwa jijini ni kubwa kulinganisha na ukiwa huko mabonde kuinuka ambako utabaki mwenyewe pekee na jirani yako ambaye mmeachana kwa kilometa saba.
Ipendeze tu kushauri na kukuacha utafasiri unavyoweza kuwa mipango thabiti ya kuendeleza miji yote nchini iwepo na si kila mradi au mpango wa maendeleo basi sehemu inayoangaliwa ni DSM pekee na si sehemu nyingine. Hivi umeshajiuliza kwanini kuna msemo wa watu wa Dar na watu wa mikoani? Kuna tofauti, tafasiri unavyoweza