Makapuku Forum

Mkuu asante
 
Muziki: Hutaki Kutabasamu, Usifungue Duka

Leo ni Furahi day, inabidi kufurahia kwa sana maana kufurahia huyarahisisha maisha. Ninakusalimia Kapuku mwenzangu kwa tabasamu kubwa kabisa na kwa vile nakuona unasoma muda huu huku ukiwa na tabasamu la nguvu. Hongera sana.

Kutabasamu ni jambo zuri na wikend ukiianza na tabasamu basi tarajia mambo mengi kukaa kwenye mstari. Unapotabasamu kwanza unajihakikishia uso mzuri, pili unaweka mazingira mazuri ya kujenga mahusiano na watu wanaokuzunguka na wageni. Muulize anko wangu Lyon Lee yeye tukiwa bar atasalimia kila mtu na akifika kwa mdada bongebonge ataweka kituo na kuomba namba, kwa kuwa anasmile mara nyingi hupewa namba isipokuwa mara moja tu alipewa email na wakapigas selfie, this is my uncle bhana.

Muziki sasa, ukitabasamu unaupa ubongo wako uweze wa kuchakata taarifa (critical analysis) na zaidi kuyaona maisha katika mwanga bora.
Nakupenda Kapuku mheshimika na unalijua hilo. Furahia wikend yako

 
Muziki wa Mdhamini: Kukazana ni Kusaidiana

Unapoweka juhudi kwenye jambo, huko ndo kukazana na hata Mwinyi aliwahi kutuusia tuzidi kukazana sana kwenye migomba kwani tutafungua fursa za ajira na ongezeko la watu tunalolishuhudia basi litakuwa salama kwa chakula. Endelea kukazana sana kwa kuwa hata mkuu katutaka tufyatue, elimu ni bure.

 
bichwa lako santeee binamu
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…