Makapuku Forum

Muziki: Upekee, Kuiga na Kuboresha

Tuzo za Grammy zimeisha jana na wakali wengi wamepata tuzo, Bruno Mars na Kendric Lamar wamejizoela tuzo kibao, hongera kwao. Nikusalimie Kapuku mheshimika na kukutakia juma zuri nikijiaminisha ulikuwa na wikend nzuri. Mimi sijambo na wikend ilikuwa poa sana, asante kwa kutouliza ila nimependa ufahamu.

Muziki huelezea mengi, hisia, ukweli, kiujumla falsafa nyingi huelezewa kwenye muziki unaoupenda. Kama ilivyo kwenye kusoma kitabu (BTW, wikend hii nimeanza kusoma kitabu kipya, ni cha hadithi ya kubuni yenye kufuata matukio halisi- unamkumbuka Black Widow, ndo nachokisoma sasa). Mwandishi kafuatilia matukio ya kweli, akatengeneza hadithi nzuri ya kuvutia, hii ndo tunahitaji wasanii wetu wafanye, upekee na kama ukishindwa iga uboreshe uoneshe utofauti.
Muziki sasa, nimeanza kuongelea tuzo za Garmmy 2018 na nikasahau kukwambia Ladysmith Black Mambazo wamejitwalia tuzo ya album bora. Wasanii wetu wana kitu cha kufanya mojawapo ni kusambaza kazi zao kimataifa, muulizeni bingwa wa Mchiriku Jagwa, nakomea hapa. Namsalimia mjomba wangu Lyon Lee msidhani nimesahau kuwaandikia yale tunayofanya kiukoo

 
Naomba unipatie softcopy ya hcho kitabu...
 
Asante Obe muziki mzuri ,nawapenda hawa ndugu wanaimba kwa hisia sana na Ujumbe haupotei
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…