Tafasiri Unavyoweza: Ushawishi, Jiongeze
Jiongeze, hili ni neno/kitenzi kinachomaanisha upe kazi ubongo wako. Na kazi ya ubongo ni kufikiria, kupambanua na kukusaidia ufanye maamuzi.
Tunashawishiwa kila siku, kila saa, ukitizama luninga, ukisikiza radio, ukisoma magazeti yote haya yapo sio kukuhabarisha tu bali kukushawishi juu ya jambo fulani. Unakutana na mmachinga, afisa masoko na mwanasiasa would wanapanga kukushawishi ufanye wanachotaka. Mwanaume au mwanamke akikutaka kimapenzi ya muda mrefu au mfupi, atakushawishi. Tafasiri Unavyoweza.
Zipo njia kadhaa za kushawishi, angalia matangazo ya sigara na pombe. Unashawishiwa. Angalia matangazo ya forex/kamari/kubet, unashawishiwa maana wewe ni fursa, Jiongeze.
Tafasiri Unavyoweza, ushawishi una sababu na wewe timamu Jiongeze, kipe kichwa chako kazi ya kufanya, kufikiri. Ukifanywa fursa hakikisha kuna hamsini kwako hamsini kwake, usiwe 0-100