Makapuku Forum

Kivuruge anavuruga sana
 
ZABURI 121

1.Nitayainua macho yangu,msaada wangu utatoka wapi.

2.Msaada wangu ni katika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi.

3.Asiuache mguu wako usogezwe;asinzie akulindaye

4.Naam ,hatasinzia wala hatalala usingizi,Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5.BWANA ndiye mlinzi wako,BWANA ndiye mlinzi wako BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.

6.Jua halitakupiga mchana ,wala mwezi wakati wa usiku.

7.BWANA atakulinda na mabaya yote Atakulinda nafsi yako .

8.BWANA atakulinda utokapo na uingiapo Tangu sasa na hata milele.

SIKU NJEMA
 
 
TUOMBE:


Baba yetu na Mungu wetu tunakushukuru sana kwa wema wako na Ulinzi wako hata kutufikisha siku hii ya leo JUMAMOSI 23 DESEMBA 2017 wako watu wengi walitamani kuiona siku ya leo,wakiwa na mipango mingi , haijawezekana. Baba Sifa Shukurani Heshima Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.
Tunakuomba utusamehe makosa yetu yote tuliyotenda kwa mawazo maneno matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali
Utulinde siku ya leo Utukinge na ajali na hatari zote Ukawatume Malaika Walinzi Kila tunapokuwa Baba na Utupe nguvu ya kukutumikia wewe.
Wabariki watu wote katika Familia zetu Wasaidizi wetu wanandoa Watoto Ndugu Jamaa na Marafiki Damu ya Yesu itufunike.
Walinde wenye mahitaji na shida mbalimbali Ponya Wagonjwa Fariji Wafiwa ,Wajane, Wagane, Yatima, Wafungwa na wote Walioumizwa na kukata tamaa wape Tumaini Baba.
Walinde Wasafiri wote Majini Nchi kavu Angani uwe Dereva Utufunike kwa Damu yako ya Thamani Tutokako na Tuendako Tuwe salama,tuepushe na ajali za aina yoyote.
Bariki kazi zote za mikono yetu Ukaonekane kwetu katika Ajira Ujasiriamali Biashara tupate riziki halali na tukutumikie vyema.
Mungu wetu na Baba yetu tunakuomba utusaidie tuwe na Upendo wa kweli tukawe msaada kwa wenzetu kimwili na kiroho na tusipungukiwe Baba tuitende kazi yako bila kuchoka.
Asante Baba kwakuwa Unatupenda na Utatutendea sawasawa na Mapenzi yako Tunaomba haya yote kwa Jina la takatifu la Yesu Kristo tukiamini na kushukuru Amen.Nawatakia siku njema yenye Baraka Damu ya Yesu itufunike Amen
 
Amen mama mchungaji Asante kwa neno
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…