Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Kusikia Sio Kusikiliza

...juzi nilikuwa nabisha na anko wangu, eeh huyu huyu mnayemjua sio huyu mdogo. Anko mdogo yeye uongo mbaya ni mtu makini huwa anasikiliza sana na kuelewa mambo wakati akiwa hajalewa. Ila huyu anko wangu mnayemjua yeye atasikia kitu na atafanya maamuzi hapo hapo, yaani huwa namlinganisha na yule jamaa tuliyempigia kura mtawala lakini kila siku ni frustration tu akifurahia umaskini na kudhani kuwa tajiri ni dhambi. Hivi nimeanza tu bila kukusalimia wewe Kapuku mheshimika, basi nakusalimia na kukuambia ninakupenda sana, unalijua hilo.

Mabishano yangu na anko ni kuhusu kusikia na kusikiliza, ujue tupo wengi sana ambao huwa tunajidai kuelewa kwa kusikia na sio kusikiliza. Kuna tofauti kubwa kati ya kusikia na kusikiliza, kusikia ni kama unasikia mawimbi ya sauti na ubongo unapata taarifa. Kusikiliza ni mchakato, a mental process , unasikia, unafikiri na kuelewa ujumbe. Sasa anko kashangaa sana mbunge kujiuzulu kisa anaunga mkono sijui juhudi gani ambazo wengine hatuzioni na bado tunaunga mkono.

Muziki sasa, tusibishane kuhusu siasa, dini, mapenzi na mengine mengi, muhimu tusikilize ili tupate ujumbe, tunaweza kubishana usiku kucha humu kuhusu siasa kwa mfano, lakini je vyama tunavyobishania vinatupa meseji gani au ndo mambo ya potelea mbali ilmradi tu tunaunga juhudi ya kitu ambacho hatukielewi.

Asante binamu hii nyimbo imfikie bae wangu mie jamani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom