Makapuku Forum

Muziki: Likizo

...inawezekana mpo wadau humu mko likizo, namaanisha mapumziko yaani ile ruhusa anayoipata mwanafunzi au mwajiriwa. Hongera kwa wote mlio likizo sasa na wale ambao likizo huwa tunazikimbia basi sio mbaya tukajitahidi angalau kupata mapumziko marefu kidogo kwa kile ambacho tunakuwa tunafanya kwa mwaka mzima.
Ila likizo ya kipindi hiki huwa ina mengi, siwaongelei wanafunzi (watoto wa shule) ambao likizo maana yake utumie kujifunza yale utakayosoma mwakani na si ndo ujikalie tu ukibet kama unasubiri ubwabwa msibani hata kuzika hukwenda. Nawaongelea watu wazima kama mimi ambao hiki kipindi cha likizo ndo wanakazana kutafuta sababu ya kuomba likizo ya uzazi mwakani na mvua hizi zinavyonyesha sasa.

Muziki sasa, najiaminisha ulikuwa na wikend nzuri, nami upande wangu ilikuwa poa sana. Muda niliutumia kwa kusoma kitabu kipya nimepewa zawadi ya krismasi, na nikawapigia simu wazee wangu na kuwaahidi wiki moja kabla ya Krismasi nitawapatia sikukuu, maisha mzunguko na upendo ndo muhimu

 
Waooooo...speechless...asante Obe
 
Asante binamu obee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…