Makapuku Forum

Makapuku Forum

2b3850bfca62ae92dd8a468477119744.jpg
 
Baba yetu na Mungu wetu tunakushukuru sana kwa wema wako ,fadhili zako na Ulinzi wako hata kutufikisha siku hii njema sana ya leo JUMATATU , 20 NOVEMBA ,2017 Baba Sifa Shukurani Heshima Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.
Tunakuomba, utusamehe makosa yetu yote tuliyotenda kwa mawazo maneno matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali
Tunaomba Utulinde siku ya leo na wiki nzima Utukinge na ajali na hatari zote za mwili na za roho Ukawatume Malaika Walinzi Kila tunapokuwa Baba na Utupe nguvu ya kukutumikia wewe.
Wabariki watu wote katika Familia zetu, Wasaidizi wetu, wanandoa ,Watoto, Ndugu Jamaa ,majirani na Marafiki Damu ya Yesu itufunike.
Walinde wenye mahitaji na shida mbalimbali Ponya Wagonjwa Fariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wafungwa na wote Walioumizwa na kukata tamaa wape Tumaini Baba.
Walinde Wasafiri wote Majini ,Nchi kavu, Angani uwe Dereva Utufunike kwa Damu yako ya Thamani Tutokako na Tuendako
Bariki kazi zote za mikono yetu Ukaonekane kwetu katika Ajira ,Ujasiriamali Biashara tupate riziki halali na tukutumikie vyema.
Mungu wetu na Baba yetu tunakuomba utusaidie tuwe na Upendo wa kweli tukawe msaada kwa wenzetu kimwili na kiroho na tusipungukiwe Baba tuitende kazi yako bila kuchoka wala kukatishwa tamaa..Tunayo mipango mingi mbele yetu Baba tunaomba UKATUFANIKISHE ,kila jambo tulilopanga lifanyike kwa utukufu wa jina lako takatifu
Asante Baba kwakuwa Unatupenda na Utatutendea sawasawa na Mapenzi yako.

Tunaomba haya yote kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu amen.Damu Takatifu ya Yesu ikanene mema wiki nzima kuanzia leo. Amen.

SIKU NJEMA,WIKI NJEMA YENYE BARAKA TELE
 
Kumekucha swalama wakuu japo anko mpendwa Obe bado hayuko sawa maumivu kiukweli kipigo kilikuwa kitamu kitakatifu ...ila nimejifunza kwake

Maumivu yake hayawezi kusababisha etu ashindwe kunipa udhamini na mm bila hiyana kapuku muheshimika nakusalimia kwa niaba ya anko...


....anko, sasa hivi maumivu yamepungua, nimekula madiclopar kama kichaa, kumbe yanasaidia bhana! wikend nimeshinda nasikiza gospel tu wala sijaweza kufanya kitu kingine.

Ila anko siku nyingine misala yako siji hata ukiniita vipi, haya maumivu ni kwa sababu nilikuja kuingilia ugomvi wakati unagombana na mchumba wa Perepetua, jamaa anapiga balaa, vipi mbavu zako
 
....anko, sasa hivi maumivu yamepungua, nimekula madiclopar kama kichaa, kumbe yanasaidia bhana! wikend nimeshinda nasikiza gospel tu wala sijaweza kufanya kitu kingine.

Ila anko siku nyingine misala yako siji hata ukiniita vipi, haya maumivu ni kwa sababu nilikuja kuingilia ugomvi wakati unagombana na mchumba wa Perepetua, jamaa anapiga balaa, vipi mbavu zako
Naona harakati zako za kunigombanisha na mpenzi wangu ABJ hujakomaa ila utashindwa make katulia tuliii kwangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom