MKE JEURI
(The Wife's Tyrant)
Sehemu Ya 35
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
Sasa sheby ikabidi apige jicho vizuri kwa nyuma ili akiendesha gari asije kudondoka mana hapo alipo kajikunja sana kwa baridi... Lakini sasa ile sheby kupiga jicho nyuma, kakutana na paja lilionona haswa, akapanda na paja hilo hilo mpaka alipokutana na chupi ya pinki... Balaa la Sheby ni kuona hio nguo, yaani hio ndio shida yake kuu... Sheby akatikisa kichwa ili kujitoa ufahamu, akamfunika vizuri lakini bado akili inawaza tu kumfinya... Alipiga moyo konde, aliwasha gari kisha huyooo.. Mpaka kwao rose katoka nje baada ya kusikia muungurumo wa gari,...
"ebu mchukiwe rafiki yako"
Rose alitoka na kumshika mkono, kiukweli mary alikuwa wabaridi sana kutoka AC ya kule ndani
"mbona ana baridi hivi"
"nilisahau nikajikuta nimemfungia kule ndani"
"mungu wangu sasa si ataugua huyu"
Rose alimkokota rafiki yake mpaka ndani kisha akarudi kwa sheby...
"boy nina maongezi na wewe"
Aliongea rose huku akimsogele kijana huyo.......... Dakika chache mbele sheby alitoa gari na kurudi nyumbani kwake, hata mke wake sikuhizi hakasiriki hovyo wala hamkasirikii mumewe, anampokea kwa shangwe sana... Lakini leo alishangaa mkewe kawa kimya afu mbaya zaidi alikuwa akimwangalia,..
"haya niambie.. Naona makiss ya mdomoni na mashavuni hayajakutosha,.. Ila ukaona uje unidhibitishie kwa kupigwa mabusu mpaka kwenye mashati"
Sasa sheby kuangalia kwenye kifua chake katika shati, laaaaa haulaaaaa shati limejaa rangi ya mdomo, (lipstick)
ENDELEA........
Sasa kabla hatujaanzia hapo naomba tuanze nyuma kidogo wakati amemmbeba mary,... Mary akiwa kule ndani alijipara mdomo yaani alijipaka rqngi za mdomoni huku akisema
"kama nitashindwa kukuambia basi we gundua upendo wangu kwa rangi"
Aliongea hivyo mary kisha akajifanya kulegea lege lege... Sheby alipokuja aligundua mary aliathiliwa na air condition za humo ndani hivyo kakosa nguvu ya kutembea,.. Na hapo ndipo sheby alipochukuwa jukumu la kumbeba mpaka kwenye gari, sasa hicho kitendo cha kubebwa hapo ndipo alipompaka sheby rangi ya mdomo katika kifua chake, tena vile sheby akitembea huku mary alikuwa akimkiss kijana huyo katika kifua chake, bila kujua hio ni hatari sana katika ndoa yake... Kijana yalimpakia mary vizuri kisha akaondoka zake, alipofika nyumbani kwao rose alitoka na kuja kumpokea rafiki yake, japo wana kabifu ka kimapenzi wenyewe ni siri yao... Rose alimpeleka mary ndani kumlaza lakini ukumbuke kuwa mary hakuchoka kivile bali aliweza kuongea na kutembea pia, lakini kulegea kule alifanya makusudi kwa yule ampendae... Lakini kabla sheby hajaondoka rose alimwita sheby
"Boy, nina maongezi na wewe"
Aliongea rose baada ya kumpeleka mary ndani, lakini mary yeye hakulala aliamka na kuchungulia dirishani, kana kwamba wivu ulikuwa ukimsumbua mtoto wa kike... Sasa ukumbuke sehemu iliopita hatukujua walichoongea hawa watu wawili, na dhumuni la kuianzia stori huku nyuma kabisa, ni ili tuyajue yale maongezi baina ya rose na sheby..
"unajua nachelewa"
Aliongea kijana huyo huku akiangalia saa yake ya mkononi,
"i Know, but nipe dakika tano tu"
Rose alisogea karibu na sheby, lakini sasa rose kuangalia vizuri kifuani kwa sheby aligundua shati lake lilichafuliwa na makiss ya mary,.. Rose akajua basi mary keshamaliza kila kitu, kama mpaka mabusu wamepigana basi keshamaliza kazi yake... Lakini rose alipoangalia vizuri, makiss yenyewe yalionekana kama kuiba iba hivi ndipo alipogundua kuwa bado hajafanya lolote lile...
"boss.... Kwanza kabisa naomba unisamehe mimi, sisi ni wafanyakazi wako, lakini kibaya zaidi ni kwamba wote tumejikuta tukikupenda weww peke yako... Mpaka sasa hivi hapo ndani hapatokalika tena, mary anataka kuhama kwa kile nilichomfanyia"
Aliongea rose huku akiwa anafikicha vidole vyake kana kwamba anaanza kumseidia mary
"sasa kwanini umfanyie mwenzio kitu ambacho hapendi"
"kitu ambacho hapendi, ni kufanya mapenzi na wewe"
"Ati nini"
Wakati huo mary anasikiliza kupitia dirishani,
"kiukweli Mary alikuwa akinituma mimi kama dada yake kwako kukudhihirishia kuwa anakupenda, lakini badala yake nikawa naitumia nafasi hio kujielezea badala yake... Nakumbuka hata siku ile mary alilazimika kwenda bafuni kuoga ili kunipa nafasi ya mimi na wewe nikuelezee ni jinsi gani anakupenda... Lakini nikawa najitengenezea mimi kwa tamaa zangu za mwili"
"kwaio point ni ipi"
Aliongea kijana huyo huku akitaka kuondoka mana hakuna kilichokuwa kikimuingia akilini,
"najua nimeshaharibu sana, na mpaka sasa hatuna raha tena baada kugundua tumefanya mapenzi mimi na wewe... Na hata ile chupi yangu yeye ndio alichukuwa"
"kwasababu gani afanye hivyo"
"aliniambia kuwa alileta documents fulani, ndipo akakuta nguo yangu juu ya meza, anavyosema yeye aliondoka lakini kufika mbele akakutana na baba yako anakuja ofisini kwako,.. Ikabidi arudi mbio na kuichukuwa ile nguo ili baba yako asije kuiona... Hivyo ndivyo ilivyokuwa na kwa kitendo hicho tu nimegundua mary ananipenda sana na hakutaka nifukuzwe kazi japo niliekuwa nafanya nae mapenzi ni mtu anaempenda kwa dhati.... Boss, ndio maana nikatanguliza Samahani, kwasababu tumejikuta tunakupenda tu, ila najijua mimi ni tamaa zangu tu, lakini mary, anakupenda kutoka moyoni... Mfikirie tu, kama ni mimi niache mana ilikuwa ni nafasi yake"
Rose alimaliza kuongea kihivyo huku akitaka kuondoka
"mshanifanya mi malaya eee?.. Yeye leo si kafanya na mtu ofisini"
Rose kashangaa kuskia mary alikuwa na mtu kazini,.. Hata mary nae akawa makini kuskia hapo
"alikuwa na mpenzi ndani"
Aliuliza rose huku akiwa katoa macho
"ina maana we hujaona kondom zile"
Rose kuskia hivyo akapumua kwa nguvu, mana alikuwa anamjengea rafiki yake japo keshaharibu lakini ivo ivo tu
"afu boss Samahani, sijakuelezea kuhusu zile kondom... Zile mimi ndio niliziweka tukiwa ndani ili tukutwe na hatia wote, kwasababu muda nilioweka zile kondom kwenye begi lake, alikuwa bado hajanipa chupi, hivyo nikajua nikikutwa sina chupi nitafukuzwa kazi, sasa nikaona tuingie wote nitoke peke yangu haiwezekani ndipo nikamuekea kondom kwenye begi lake... Lakini Nilitamani kuzitoa baada ya kunipa nguo yangu ila nilikosa nafasi hiyo, nikaacha tu ndio akakutwa nazo"
Sheby aliona ni kama anaimba tu, aliingia kwenye gari yake kisha huyoo kaondoka zake, rose kaingia ndani na kumpa taarifa mary
"haya sasa kazi yako nimeshamaliza"
Aliongea rose huku akikaa kitandani
"sina shida"
Mary alijibu kwa nyodo kali, na anajua kweli kamwambia, lakini haiseidii kitu mana hata akimkubali, atakuwa keshatembea na shemeji yake,...
"sasa mbona unakusanya nguo jamani"
"niache niondoke zangu... Kisa unalipa chumba wewe ndio uninyanya kwenye mapenzi"
"mary jamani, nimeshasema yote"
"sina shida na ukuadi wako.. Naondoka"
"mary please kumbuka tumetoka mbali eti"
"staki kujua"
Mary kweli alikuwa akikusanya mabegi yake tayari kwa kuondoka,.. Rose alichukuwa simu na kumpigia rafiki yao mkubwa ambae ni mwai
"halooo shost mwai"
"vp saa hizi"
"mary anataka kuondoka jamani eti kisa nimeshindwa kumtongozea boss wetu"
"ivi nyie mna akili nyie... Ebu mpe simu niongee nae"
Mary alipewa simu na rose, hakusita kuichukuwa mana mwai ndio rafiki aliewapokea hapa mjini
"we mary, unakwenda wapi usiku huu.. Utakuja ubakwe bure na kibikra chako kiozee mbele, tuliza miguu hapo"
"siwezi kuishi na hasidi mimi"
"ebu ngoja kwanza, naomba kesho Jumapili mje nyumbani kwangu tulizungumze vizuri"
"sawa lakini staki kukaa kwake tena"
"mary nisikilize mimi kama dada yako.. Usinidharau.. Kama ni huyo mwanaume hata mimi naweza kukuseidia"
"ok sawa... Lakini naomba mwisho wa kuishi na huyu mtu iwe leo, kesho natafuta chumba changu"
"sawa hakuna shida"
Wakati mwai anaongea na simu ghafla honi ya gari inapigwa hapo getini, kana kwamba sheby ndio alikuwa anaingia kwa wakati huo,
"sawa basi kesho muje wote"
Mwai alikata simu kisha kasimama mlangoni ili kumpokea mume wake, siku hizi habebi bebi vipocho pocho vingi mana si anapika, mwanzo alikuwa akibeba kwasababu kulikuwa hakupikwi,... Sasa mwai kabaki mdomo wazi baada ya kuona shati la mume wake limejaa rangi ya mdomo
"haya niambie.. Naona makiss ya mdomoni na mashavuni hayajakutosha,.. Ila ukaona uje unidhibitishie kwa kupigwa mabusu mpaka kwenye mashati"
Sheby kucheki Ayaaaaaa... Kweli imekaa mabusu sio mabusu.. Lakini sasa huyu ni mtoto wa kiume na anajua kuikwepa mitego kama hio
"ayaaaaaaa ina maana yule bibi kizee anapakaga huu ujinga"
Aliongea hivyo huku mwai akiuliza kuwa
"ina maana siku hizi unatembea na watu wazima"
Sasa sheby kuskia hivyo nae Kukasirika na kusema
"kwani ata wewe ni lika langu, si mtu mzima kabisa wewe, muone vile"
Mwai roho ilimuuma mana kwa sasa ana vichembe chembe vya upendo kwa mumewe...
Sheby alimsukuma na kuingia zake ndani,
"lakini bado nina haki ya kujua huu upumbavu wa kwenye shati umeutoa wapi, laa sivyo hapalaliki hapa"
Mwai kaamua sasa mana kupenda penda kijinga imekuwa kero..
"kuna bibi aligongwa na gari ndio nikamseidia, ndio maana mwanzo nikasema ina maana mpaka bibi kizee anapa huo ujinga.. Umeridhika"
"basi nenda zako kalale uko"
Sheby aliingia chumbani kwake na kulala bila hata ya kuvua viatu kwa kuchoka...
Kesho yake ikiwa ni siku ya Jumapili sheby akiwa katika gari kuelekea kwa akina zai,... Leo kwa mara ya kwanza toka waachane na zai ndio anakanyaga kwao,... Lakini sasa ile anakata tu kona ya kuingilia kwenye boma ya akina zai, aliona gari ya saidi kwa mbali, sheby alitamani kukata na kurudi lakini hapakuwa na nafasi ya kugeuzia, ni mpaka ufike pale ndipo ugeuze,.. Saidi akiwa ndani na mke wake mtarajiwa alisikia sauti ya gari ya boss wake,...
"heeeeeeeee kwa mfano boss kapajuaje hapa"
Saidi aliongea kimoyomoyo huku akiwaza boss wake kapajuaje hapo, mana anakumbuka alimwomba gari tu sasa vipi leo kaja,.. Ukumbuke saifi hajui kama sheby na zaituni walikuwa ni wachumba waliokuwa wakisubiri ndoa...
"karibu baba"
Mama zai alimkaribisha, wakati huo ndani zaituni anaogopa kuwa saidi akijua kuwa mimi nilishawahi kuwa mpenzi wa boss wake, atamuacha na mwishowe atakuwa kakosa bara na pwani,...
"Ahsante mama shkamoo"
"Marahaba ujambo baba"
"sijambo mama angu"
Sheby kaingia mpaka ndani na kuwakuta zai na saidi wamekaa kochi moja ili kuonyesha upendo wa hali ya juu,...
"za saa izi jamani"
Sheby alitoa salamu kwa wawili hao,
"safi tu boss, vp umejuaje kuwa nipo huku"
"aaahhh nimekuja kumsalimia mama hapa"
"aaahhh kumbe unafahamiana na hii familia"
"ndio, tena kwa kiasi kikubwa sana"
"aaaaahh duuu nimeshangaa kuskia upo hapa na sijawahi kukuleta"
"ahahahaha mi mbona mwenyeji hapa"
Lakini sasa mama ni mtu mzima alishaanza kuona kitakachotokea mbele baada ya saidi kujua boss wake alishapita hapo... Mama alimwangalia sheby kisha akatikisa kichwa, kana kwamba kama sheby kuna kitu alitaka kufanya asifanye tena, mana ataharibu uchumba wa mtoto wake... Sasa kwakua sheby yeye hana nia ya kuharibu hivyo alimsikiliza mama kisha akajifanya kamfuata Zainabu mana kuna zainabu na zaituni...
"aaahhh zainabu yupo wapi"
Zaituni alishangaa kumsikia sheby anamuulizia ndugu yake, na sheby anajua fika kuwa zainabu ni malaya wa kutupwa
"yupo nje hapa baba"
Mama alitoka na sheby kisha akawa anamwangalia zainabu... Kwa bahati nzuri hakuwepo mana ilikuwa ni gia ya kutokea pale ndani.. Mama hakutaka kuuliza kilichotokea baina yao na zaituni, mana kitendo cha zaituni kuleta mwanaume mwingine ni dhahiri kuwa alishindwa kuvumilia hali ya kijana huyo... Sheby aliwasha gari yake bila hata ya kuaga kule ndani....
Ikiwa ni mida ya jioni huku nyumbani kwa kijana sheby kulikuwa na ugeni wa wasichana wawili... Mary na rose
"karibuni jamani mashost zangu"
Mwai aliwakaribisha wageni zake, kama unakumbuka aliwaalika waje wale chakula cha jioni,.. Wakati huo kijana sheby yupo njiani kuelekea nyumbani kwake, asijue hili wala lile huko nyumbani kwake
"jamani nimewamis nyie, toka siku ileee ya sherehe mpaka leo"
"mmmhh mbona sie tupo, sema bize"
"bize ya hao wachumba zenu mnaowagombea kila siku.. Oleweni mtulie kama mimi mwenzenu"
"enheee hapo mwai umeongea kitu, ebu mwambie mary, nimemuomba msamaha mimi lakini hataki kusikia sijui ana nini huyu"
"lakini nawe rose, kwanini utembee na mtu wa watu eee, Kama we umejua anampenda kwanini usimfanyie mpango yeye"
"lakini mwai si unajua shetani tu"
"kwahio huyo mtu mnafanya nae kazi ofisini kwenu"
"ndio tena ni boss wetu mdogo mdogo hivi"
Waliongea bila hata ya kumeza mate, kama unavyojua mashostito wanapokutana mahali, na wakati huo kijana sheby yupo mlangoni tayari kiganja chake kimetua kwenye honi
"piii, piiii"
Mlinzi kama kawaida yake kuchakalika kwa hapa na pale kutokana na kazi yake
"mmeo nini huyo"
Aliuliza rose huku kama wanaogopa ogopa hivi mana kwenda kubwata umbea kwenye nyumba za watu ni kitendo kibaya sana tena kwa sisi wanaume hua hatukipendi kabisa yani, mwanamke utoke kwako uje huku kuleta umbea tu, ndio uharibifu wa ndoa sema hawajui tu wenyewe.. Sasa kama kawaida ya mke wa sheby kukaa mlangoni ili tu ampokee na maneno,
"leo hujaleta hata chochote, yaani mwanaume wewe"
Mwanaheri aliongea hivyo huku sheby akishuka kwenye gari na msunyo mkubwaaa,...
"nipishe mimi"
"lakini si nimekuuliza tu"
"unaniuliza mie baba ako"
"Wwhaaaaaat"
Sasa mwai anasema What, sheby nae ndio anawaona akina mary...
"ooohhh leo kuna ugeni leo"
Sasa mary na rose ndio wanashangaa, ina maana kumbe rafiki yao ndio kaolewa na boss wao,. Sasa mwai nae anataka kutambulisha anakuta watu wanajuana siku nyingi tu,.. Mwai anashanga hawa wakina rose na mume wake wamejuana wapi...
"nyi... Nyie... Nyie mnajuana"
Mwai au mke wa sheby Aliuliza, na sheby pale pale akajibu kwa uchangamfu wa hali ya juu..
"ndio... Ni wafanyakazi wenzangu hawa.. Sasa kwanini umekuja usiku jamani"
Sasa sheby yeye anajua katembelewa yeye,...
"rose na mary, anachokisema mme wangu ni kweli mnafanya nae kazi"
"ndio.. Tena ni boss wetu huyu"
Sasa mwai kuskia hivyo akagundua jambo
"ina maana siku zoote hizo kumbe mnamgombania mume wangu rose??... Hapana kitaeleweka tu hapa"
Mwai alianza kufunga kanga kiunoni, wakati huo sheby nae anashangaa kumbe mkewe na akina rose wanajuana.....
Je? Nini kitaendelea hapo???... Watajitetea vipi?.....