Zaburi 145
1 Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2 Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.
3 BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani.
4 Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.
5 Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.
6 Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako.
7 Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako.
8 BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,