MKE JEURI
(The Wife's Tyrant)
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
"heeeeeeee shadi umependeza"
Aliongea zai huku akimuonea wivu mwenzie
"yes, ni mambo ya kujiachia tu.. Nitajibana mpaka lini na wakati najitambua"
Shadya kumbe hakuwa mschana mzuri, kumbe alivaa ngozi ya kondoo na wakati kumbe ni chui,.. Huezi amini kumbe shadya ni mschana anaejiuza, na kutudanganya ni fundi cherehani kumbe ni malaya,.. Kwani hata nguo alioivaa ilikuwa ni fupi na hata yeye mwenyewe alikuwa akiivuta vuta ili isiwe fupi sana...
"kujiachia Kivipi tena"
"mi nakushangaa unakaa na kijidume kichaafu hakina mbele wala nyuma, pesa ya kuendea kule india yenyewe kakopa sasa hivi anadaiwa weeee, utakufa njaaa"
"lakini shadi mbona sikuelewi shost"
"ona pesa hizi hapa"
"Haaaaaaaaaaaaaaa umetoa wapi pesa zote hizo"
"una sura, una umbo zuri.. Una kila kitu kwanini usipate pesa mtoto wa kike"
Huezi amini shadi kaanza kumharibu mdada wa watu, maskini zai anatamani mavazi aliovaa shadi, anatamani pesa alizonazo shadi
"nitapate sasa"
"sikia... Kuna kijidume kinakuoenda kina pesa chafu.. Vipi sema nikupeleke"
"mmhhhhh lakini shadi"
"lakini nini acha ujinga... Mimi nawagereshea tu hapa lakini nina nyumba yangu mjini"
Mara ghafla simu ya shadi ikaita, sijui nani aliokuwa akipiga
"enheee tena mwanaume mwenyewe huyu hapa anapiga... Sema nimuambieje sasa kuhusu wewe"
Zaituni alianza kujing'ata ng'ata vidole huku akiziangalia zile pesa za
Kweli wahenga walisema mtu mpole ndio mbaya kuliko mcharuko, huezi kuamini shadi yule mpole sana huku akijifanya ni mshona nguo, kumbe ni mschana wa kujiuza,.. Na huwezi amini anataka kumwambukiza na zaitini wa watu,
Maisha wanayoishi ni maisha magumu sana hivyo kushawishiana ni rahisi sana tena pale unapoona ushawishi unakuja na pesa juu lazima ukubali
Sasa wakiwa wanazidi kuongea mara simu ya shadi ukaita, kuangalia jina hakutaka kusema ila alimwambia zai kuwa
"enheee tena mwanaume mwenyewe huyu hapa anapiga... Sema nimuambieje sasa kuhusu wewe"
Zaituni alianza kujing'ata ng'ata vidole huku akiziangalia zile pesa za shadi,
"mmmhhh shadi hapana, hapana... Siwezi kufanya hivyo, nampenda sana sheby siwezi.. Kama ni pesa wacha nizikose tu"
Aliongea zaituni huku akiingia zake ndani na kumwacha shadi akiongea na simu,... Na hata hivyo hatukujua aliokuwa akiongea nae,
Sasa tukija huku kwa akina rose wakiwa wana furaha sana ya kwenda kwenye harusi ya rafiki yao mwai,.. Kwa furaha kubwa walishonesha sale zao,...
"nakwambia mary mi nataka nikamwone tu huyo mpenzi wake, mana alisema hataki wazee"
Aliongea rose huku wakiendelea kujipara vipodozi vyao katika kioo...
Sasa tukija huku kwa baba yake sheby akiwa kaketi sebuleni, ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni mr sadiki, mfanyabiashara mwenzake ndio aliompigia
"haloo mr sadiki vipi"
"safi tu mr rashidi... Sasa bwana ile kazi yangu vipi"
"oooohhhhh unajua bado sijaiandikia kabisa, ila natarajia kuiandikia kesho"
"ayaaaaaaaa mr rashidiiii... Nilikwambia leo ndio naonfoka naenda Sweden, na siwezi kuondoka bila Documents husika za kazi ile"
"aaahhhhh sasa tufanyeje mr sadiki"
"hebu fanya fanya hata leo... Nisaidie bwana"
Mzee sadiki alikuwa na haraka na kazi zake, mana kuchelewa kwa documents hizo kutasababisha asisafiri,
"unajua leo nina harusi ya mtoto wangu"
"kwani huna wafanyakazi mr Rashidy... Hebu nisaidie niondoke leo hiii"
Muda wa mabwana harusi kutoka ulikuwa unakaribia, wakati huo akina mary na rose wako nje ya nyumba yao wakiita tax ili waweze kupelekwa harusini, lakini wahenga walisema mpania maji hua hayanywi, na akiyanywa basi hua sio mengi kama alivyopania,... Simu ya rose iliita
"heeeeeee boss"
Aliongea Rose huku wakishtuka kwa kuiona simu ya boss wao,... Rose aliipokea simu hio na kuongea kwa heshima
"halooo boss"
"rose,.. Samahanini watoto wangu, naombeni kuna kazi mkaifanye kule ofisini, naombeni sana wanangu, nawatumia pesa ya siku ya leo.. Kila mmoja atapata elfu 50 kwa kuifanya hio kazi..."
Akina rose walikasirika sana lakini waliposikia kuna posho ya elfu 50 mbali na mshahara.... Walifurahi
"ni kazi gani boss"
"ile ya mr sadiki, anataka kwenda Sweden leo jioni sasa kazi zake bado hazijaguswa"
"sawa boss... Tunakwenda"
"sawa, nawatumieni laki moja sasa hivi"
Mzee huyo alizamiria kuwalipa akina rose,..
Basi simu ilikata na safari ya kwenda harusini ikafia hapo...
"mary, chagua moja uende harusini au ule elfu 50...kama hutaki wacha nile laki moja peke yangu"
"nyoooooo, ulifikiri nimekuja mjini kuzungusha sketi hapa? Twende kazini woteee, kwani harusi kitu gani bwana"
Aliongea mary huku gari ikielekea kazini,.. Na siku hio haikuwa siku ya kazi, licha ya kuwa kuna harusi lakini pia haikuwa siku ya kazi...
Sasa huku kwenye harusi ikiwa imepamba moto, yaani hakusemeki ni full shangwe katika hoteli ya kitajiri jijini hapo,.. Yaani hoteli ya maana haswa tena inalipiwa kwa lisaa, ulishawahi kulipa hoteli kwa lisaa... Sasa hio inalipiwa kwa lisaa shilingi laki mija kwa lisaa limoja,.. Wakati huo mama sheby kaketi katika vile viti vya watu maalum (VIP) kiufupi wazazi wote wamekaa viti maalum
Muda nao ulisogea na sasa ni wakati wa kuvishana pete baina ya mwai na kijana sheby,.... Kwa shinikizo la wazazi ndoa ikawa imefungwa lakini kati yao hakuna aliompenda mwenzie,
"kwa sisi wazazi tunashukuru sana watoto wetu kufunga ndoa"
Waalikwa walipiga vigelegele huku wengine wakisema kuwa wanandoa hao hawaendani kabisa hata kiumri,
"Namshukuru sana mwanangu mwanaheri kwa kupata mume,.. Kiukweli kapata kijana hensamu, mchapa kazi, mcheshi.. Kiukweli nashukuru sana"
Aliongea mama yake mwai huku akimpa mama sheby maiki nae atoe sifa zake, lakini baba sheby akajua mke wake ni mtu wa kuropoka hua hafichi kitu...
"mke wangu kuwa mpole"
Alimwambia mkewe kwa sauti ya chini chini
Mama sheby alikasirika sana kitendo cha mtoto wake kuoa jitu zima mtu mwenye umri mkubwa hata mtoto wake wa kwanza hawalingani kabisaa..
"hata mimi nina furaha kwa mwanangu sheby kupata jiko,.. Mimi na mume wangu tumewazawadia nyumba ya kifahari ilio mpya.. Tunawaombea katika ndoa yao na maisha mazuri"
Aliongea mama yake sheby huku akitoa hatimiliki ya jumba hilo la kifahari, ambalo ndio wataishi sheby na mke wake mwai...
BAADA YA MIEZI MITATU KUOITA
Siku, wiki, miezi kadhaa ilipita na leo ni siku nyingine kijana sheby akiwa ofisini kwake, lakini mawazo ni yale yale, hakuwa na raha kabisa...
"boss kuna kazi hiii hapa ya mr kifesi"
Alikuwa ni mary akiwa kaleta kazi fulani ambayo ilistahiki aifanye kijana huyo,.. Sheby akiwa katika mawazo mengi sana hata kazi zilikuwa haziwezi.... Na wakati huo muda wa kutoka kazini ulishafika lakini sheby yeye hatamani hata kurudi nyumbani, japokuwa ana mke lakini bado hana raha,... Wafanyakazi wote waliondoka baada ya saa 11 kamili kufika, sheby alibaki ofisini akiwa mpole sana...
"rose, unajua boss tumemwacha ndani"
"weeeeee ina maana bafo hajatoka"
"ndio, gari yake si ile pale"
"mungu wangu weee, amina atakuwa keshafunga mlango"
"lakini boss ana ufunguo"
"aaahhh basi kama anao.... Lakini mary, boss mdogo kapatwa na nini"
"mi ata sijui"
"mana ni muda sasa, hana raha kama mwanzo"
"mi nakwambia kama ndio tungelikuja kuomba kazi kipindi hiki, ingekula kwetu"
"kweli.. Mana asingetuelewa"
"mungu amlinde tu, mana anakosa raha"
Unajua hata akina rose hawajui kama sheby kaoa, yaani harusi ilikuwa ni kubwa kila mtu anaju lakini hawa wawili hawajui, ila wafanyakazi wengine wanalijua hilo kasoro hawa, mana siku ile ndoa inafungwa rose na mary waliingia kazini, na hata ile siku waliotaka kwenda kwenye harusi sio kuwa walitaka kwenda kwasababu ya sheby, Hapana bali walitaka kwenda kwasababu ya rafiki yao mwai, na pia hawajui kama huyo huyo mwai ndio kaolewa na sheby, unaona kamchezo hako...
Wakati huo mke wa mtu, mwanadada mwai, akiwa ndani ya gari yake kuelekea kwa marafiki zake ambao ni akina rose.... Gari anayotembelea ni gari ya maana tena mpyaaaaaaaaa
Ana nyodo mwanzo mwisho, na vile uso wake ni mpana heeeee kweli hapo sheby ana kazi ya ziada... Basi mwai kafika katoka boma la akina rose walipopangisha akachukuwa simu yake na kuanza kuwapigia, lakini kabla haijapokelewa ghafla akina rose haoooo
"waoooooo jamani mwai, umekuja saa ngapi hapa"
"heeeeeee siku hizi mnapendezaje"
Aliongea mwai mana kipindi cha nyuma alikuwa akiwapa wavae nguo zake, mana walikuwa hawajapata kazi bado, sasa hivi wana kazi wanang'aaa tu...
"we acha tu mwai, lakini si tulikwambiaga tumepata kazi"
"ndio, mliniambiaga.... Lakini nyie wabaya sana nyie"
Aliongea mwai huku wakiingia ndani
"heeeeeeee ubaya wetu ni upi we mwai"
Alijibu rose huku wakikaa katika sofa, na wakati huo mary alikuwa akiandaa juisi baridi...
"kwanza kwenye harusi yangu hamkuja na niliwaalika... Pili hata nyumbani kwangu hamji, au kuolewa kwangu imekuwa kero kwenu eti ee"
"hapana bwana mwai... Unajua siku ile tuliingia kazini... Na huezi amini tulijiandaa kwa ajili ya kuja harusini, lakini tukapigiwa simu na boss tuende kazini kuna kazi ya kufanya haraka haraka... Ikabidi twende"
"ok haya, na kwangu je mbona hamji"
"kweli apo utusamehe, ila nadhani unajua pilika pilika ya hapa kazi tu"
"na ni kweli hapa kazi tu"
Basi hakukuwa na ugomvi wowote ule zaidi ya kufurahi,
"lakini mwai, sisi tunajua kwenu tu, lakini huko ulipoolewa hatukujui ng'ooo"
"msijali nitakuja siku kuwachukuwa.. Mana kuna kaumbali kidogo"
"enheee tupe habari za mumeo.. Nakumbuka ulisema hutaki mume mzee"
"we acha tu, nina mume mtoto.. Yaani kama ningelikuwa malaya toka nikiwa shule ya msingi, ningemzaa mimi"
Aliongea mke wa sheby kuwa kama angelikuwa malaya kipindi hicho basi angelikuwa na mtoto lika la kijana sheby
"weeeee mwai... Ina maana ni mdogo"
"yaani kitoto kimo hiki, sema urefu umemseidia"
"lakini ulisema mwenyewe"
"ndio ila huyo kazini afu istoshe sijampenda yaani namchukia"
"wewe mwai, wenzio wanazitafuta ndoa kama hizo hawazipati"
"I know but huyo mume wangu bwege tu"
Mwai alikuwa akimsema kijana sheby huku wakicheka sana
"kwahio ni jinga jinga tu"
"yaani halina hata akili, lipo lipo lipoleee halipendi kutoka out, yaani ni yeye na kazi tu muda wote"
"heheheeeeeeeee halooooooo bibie unalo ilooo"
Rose alicheka huku wakigongesheana mikono kwa umbea, wakati huo mary yupo bize na laptop yake, alikuwa anachati
"sasa hivi shost una laptop ni kuchat mwanzo mwisho"
"we acha tu... Hapa kuchati tuu"
"weweeeeee.... Halooooo"
"mary, umesikia mwai anavyosema kuhusu mumewe"
"nimesikia... "
"mmmhhhh lakini mwai, uyo mi mumeo tu usimfanyie hivyo"
Aliongea rose huku akicheka kwa unafiki wa hali ya juu tena wakati huo mikono inagongana haswa kwa umbea
"tena hilo ni dogo, sasa nakwambia kuna kitendo namfanyia mpaka leo hana hata raha yani"
Aliongea mwai huku rose akitega skio kujua hicho kitendo...
"Enheeee umemfanyia nini tena"
Aliuliza rose huku akitamani sana kujua, na mwai bila hiana akaanza kuropoka siri za ndoa yake..
"huezi amini rose,.. Yule mtoto wa kiume....
Je? Mtoto wa kiume kafanya nini au kamfanya tendo gani....