Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Usiaibishe Mkono Unaokulisha

Nimeianza siku yangu leo kwa namna ya kipekee kabisa, yes, upekee unaotofautiana na namna ulivyoianza siku yako. Kwangu kumekuwa kutulivu na kama kawaida unapofanya kazi ya kuajiriwa serikalini unakuwa hauko salama kivile hasa kwa awamu hii. Ni bahati mbaya sina unapokuwa na watu wengi wanaoshangilia tabia za kinyampara kisa tu nyampara ni mwenzetu na tunahusiana naye. Siku zote huwezi kuudhalilisha mkono unaoutegemea kukulisha. Mkono una vidole na ukiudhalilisha mkono navyo haviko salama.

Siongelei siasa hapa, kwangu maisha ni kuishi na tafsiri ya kuishi si tu kuwa hai bali kutambua tofauti zetu na kuheshimiana bila kujali cheo, jinsi, umri, uwezo, unakotokea na makandokando mengine. Wait a bit, maisha ni siasa, si ndiyo, na sijakosea kusema siongelei siasa wakati maisha ni siasa. Hata sijui naandika nini maana kila nachotaka kuandika vidole vinapata kigugumizi bora tu nimwandike anko wangu maana sina namna sasa. Kumwongelea kiongozi mwenye ile kitu tunaiita Dunning-kruger effect where an incompetent person is too incompetent to understand his incompetence inahitaji ujasiri hasa katika zama hizi za 'watu wasiojulikana'.

Muziki sasa, nikwambie kitu, hata mjomba wangu pamoja na mapungufu yake, mfano alipotekwa kule Moshi juzi aliamua kukimbia na kumpiga chini mateka wake, pamoja na kumpiga chini alitumia ustaarabu wa kutomwaibisha 'nyumba ndogo' kwa nyumba ndogo nyingine (hii ni nyumba ndogo mpya na aunt yangu haijui so msiseme) ya pale jirani na mimi ninapofikiaga nikija mjini. Huna sababu ya kumwaibisha uliyemwamini maana ukimwaibisha sisi tunaoangalia kwa macho ya malyenge tutajua mwenye tatizo si uliyemtumbua bali wewe unayetumbua huku ukidhani uko kwenye kipindi cha kampeni.

Asante Obe
 
Zaburi 143

7 Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni

8 Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.

9 Ee BWANA, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho wako mwema aniongoze kwenye nchi sawa. Amina
 
202f5e9a8716d83b95cff0599cb037f8.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom