Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Miaka Miwili Twajikongoja

...kuna wakati huwa najiuliza kuhusu Tanzania yetu ilivyokubwa na maswali yanazidi nikija hapa na kukuta wewe kapuku mhesimika ambaye nachukua nafasi hii kukusalimia sana na usijesema sikumbuki kuwa kwa siku mbili sijakusalimia na sina hakika ninaweza kukusalimia mara mbili kufidia siku ambazo sikukusalimia wewe unayelifanya Jukwaa hili kuwa bora zaidi ya majukwaa mengi humu. Ujue nini, wengine wakipita Jukwaa hili hawaachi kujikwaa na hii ni kwasababu wewe uko humu. Asante sana.

Leo nitaiangalia zamani, si zamani sana maana muda unakwenda hata jana inaweza kuwa zamani na ukitaka kuijua nguvu ya zamani basi kumbuka yote yaliyokufanya unyongee moyo na kama hujaamua kuamka na kuendelea kwa kuyafanya somo basi zamani itakuumiza sana kila wakati. Rais wetu katimiza miaka miwili mjengoni na anaendelea, hapa kazi tu. Kusheherekea miaka miwili ya urais, anko wangu akaandaa sherehe bhana, ujue anko wangu yeye kila tukio lazima alitafutie sababu ya kufurahia. Maisha ni kufurahia, kwani nani hapendi kufurahia. Anko akaniambia nisiache kuja kwenye sherehe kutakuwa na ugeni. Nikapiga mahesabu kama ugeni basi sherehe itakuwa kubwa maana aunt yangu kwa kuandaa madikodiko hajawahi kutuangusha. Kufika eneo la tukio namuona anko na mrembo wa kimanga, kutizama simuoni aunt. Nikajiongeza akili zangu maana haya mambo ya ukoo, nikatambulishwa na kasi ya vinywaji ilivyokuwa inakuja sikupenda hata kujua aunt yangu mnayemjua yuko wapi.

Muziki, hebu tujikongoje na tufurahie maana maisha yafaa nini kama hatufurahi na kuwafanya wanaotuzunguka wafurahi

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom