Makapuku Forum

USIKU UINGIAPO

1.Usiku uingiapo,umwaze Mungu Mkuu,aendeshaye dunia kwa mwendo mtulivu.

2.Kwanini wahangaika Usiku na Mchana?Umtwike huzuni yako aliyekuumba.

3.Kwake haujapungua uwezo na msaada.Atayatimiza yote aliyoyaanza.

4.Ukamwachie kutenda atakalo kwako!Kwa hiyo ulale raha na kufurahiwa.


TUOMBE BABA Asante kwa ulinzi wako mchana kutwa umekuwa mwema sana kwetu umetuepusha na hatari zote za mwili na roho ,ajali ,mafuriko na hata kukata tamaa..tunasema asante Baba wewe ni Alfa na Omega wastahili sifa heshima shukurani utukufu.sasa tunapumzika,tunaomba toba kwa yote tuliyotenda kwa mawazo maneno matendo uturehemu twakusihi,ponya wagonjwa,wenye tabu,dhiki,wafiwa wakumbatie , tunaomba malaika walinzi waweke vituo katika malalo yetu utuamshe tena salama asubuhi ni katika jina la Yesu jina lipitalo majina yote amina.


USIKU MWEMA WAPENDWA MBARIKIWE
 
Asante Obe Ubarikiwe
 
Amina mama mchuchu, uwe na usiku mwema.
 
Zaburi 139

7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?

8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.

11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.

13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
 
Masada
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…