Makapuku Forum

Makapuku Forum

Lakini sasa kabla sheby hajataka kuondoka,... Ghafla zaituni alitokea na kusema kuwa
"mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"

ENDELEA........



Kijana sheby aliogopa sana kuhusiana na jambo hilo, kama mwanamke kaweza je huyo mwanaume atashindwa vipi kuliweza jambo kama hilo,.. Kijana huyo alitaka hilo jambo lisiongelewe tena mana huenda kweli likawa zito kwake, hivyo bora asiambiwe mana huenda ni jambo asiloliweza, lakini wakati mama zai anajing'ata ng'ata, mara zaituni katokea huku akiwa anapapasa pakupita,..
"mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"
Aliongea zaituni huku akiwa tayari kwa kuongea,..
"zaituni mwanangu, kakae utulie nitaongea nae tu"
Aliongea mama yake zai huku akimrudisha ndani.. Baada ya hapo mama na sheby walisogea pembeni zaidi ya pale walipokuwa na kuongea

"ukweli ni kwamba, zainabu ndio anaelipa kodi ya hii nyumba, kwa mwezi ni elfu 70, na mimi sina kipato chochote cha kuingiza ili niweze kulipa"
"ina maana ni hilo tu ndilo linalowafanya akae humu ndani"
"ni hilo tu, mana kama ni zaituni akienda kuomba anakuja na hela ya kula tu, na tukifukizwa kwenye hii nyumba je tutaishi wapi, baba yao amefariki miezi kadhaa iliyopita... Hivyo zainabu ndie mlipa kodi ya nyumba hiii na ndio maana siwezi kumfukuza"
"kwani anafanya kazi gani huyo mwanao"
"hhhhmmmm baba,... We acha tu... Sasa hivi anajiuza tu na ndio maana anaweza kuilipa kodi ya nyumba hii"
"kwahio hili ndio jambo uliokuwa unaona uzito kuniambia"
"ni hilo tu baba yangu, siwezi kumgukuza kwa hilo, japo ni katili lakini nitafanyeje sasa"
"ok unaweza kuniunganisha na huyo mwenye nyumba"
 
labda kesho niongee nae mkutane"
Sheby alitaka kumaliza utata juu ya swala hilo, mana wahenga walisema kuwa, ukipenda boga basi penda na uwa lake, na sheby kweli kampenda sana zaituni, kuachilia umbo lake, bali hata heshima anayo yaani sifa zote za kuwa mke anazo, na sheby uwezo wa kumfanya aone tena anawo,...
"sasa... Naomba usimuambie hali yangu,... Narudia tena, sitaki ajue kuwa mimi nina uwezo kifedha, akikuuliza kuhusu mimi mwambie ni kijana mchapakazi tu, anafanya kazi ya kuuza viazi kwa mkokoteni sawa mama"
"sawa baba nimekuelewa.. Lakini kwanini unafanya hivyo"
"utajua baadae mama angu, ila naomba uwe kimya kwa hilo"
"mmmhhh sawa"
Basi sheby na mama zai walielewana kisha akamwachia mama huyo kiasi kidogo cha pesa,..
"sasa mama, utaniagia huyo ila umwambie ukweli kuwa naitaji kuwa nae, na sijali hivyo alivyo"
"sawa baba nitamwambia"
Sheby hakutaka kuooteza muda mana tayari ni saa nne usiku, hivyo kapenda kuwahi zaidi nyumbani.... Akiwa niiani alikuwa akiumiza kichwa sana jinsi ya kuongea kwa wazazi wake,...
Sheby alifika nyumbani na kupaki gari katika paking ya hapo hapo kwao kisha akatoka na briefcase yake mkononi mana anatoka kazini..
"wewe mtoto ulikuwa wapi mwanangu"
Mama alikuwa mlangoni akimsubiri mtoto wake arudi
"mama, gari ilipata pancha, hivyo ikabidi niipeleke kwa fundi mana kesho ningeenda na nini"
 
Sheby aliwadanganya wazazi wake hivyo huku wakiamini hilo..
"oooohhh pole sana baba"
"Ahsante mama... Vp baba yupo ndani"
"ndio, ila anataka kukupa mke.. Mi nasema usikubali"
Sasa sheby kuskia jambo la kuoa,.. Heeeeee alifurahi kinoma
"mamaaaaa, kwanini nisikubali sasa, tena nimefurahi kinoma mama angu, yaani we acha tu, yaani saa zote naumiza kichwa nitaanzaje kisema kumbe nyie mumeshalijua"
"sheby, acha ujinga wewe, umri wako bado ni mdogo, kwanini unataka kujizehesha mwanangu"
Mama anakataa mtoto wake asioe kwasababu mwanamke yenyewe anaetaka kumuoa ni mtu mzima kabisaa, lakini sasa sheby yeye alijua ataoa mtu amtakaye yeye mwenyewe, kumbe keshachaguliwa mke na baba yake... Yaani huu urafiki wa kijinga kuja kusumbua watoto wenu sio mzuri,..
"yaani ungelijua unaozeshwa na mtu kama mama yako wala usingefurahi namna hio"
Sasa sheby kuskia hivyo, hata furaha ilikata,..
"unasemaje mamy"
"utajua mwenyewe... Mi nakwambia kitu cha maana we unaruka ruka tu"
"yaani nyie wazazi mna utani nyie"
Aliongea sheby na kujua swala hilo ni utani, wakati huo mama yake anakwenda kulala,.. Lakini ghafla mzee kaja
"we mwehu ulikuwa wapi mpaka saa hizi"
Aliongea baba yake huku akiwa mkali
"mzee gari ilinisumbua kweli, imepata pancha karibia mara mbili eti"
"sasa kwanini usingesema tuite fundi"
"sasa kama fundi nimemuona mbele ya macho yangu.. Ina haja gani nikupigie simu sasa"
"ok upo salama lakini"
"nipo fresh mzee usiwaze wala nini"
"alafu hicho kihuni chako sikitaki.. Uhuni wako uko uko mtaani sio hapa kwangu"
"basi mzee"
Basi kijana sheby aliingia chumbani kwake kisha kaingia bafuni na kutoka, wala hakuhangaika kula wala nini... Kalala zake mpaka asubuhi...

Baada ya siku hio kupita, na leo ni siku nyingine tena,.. Lakini ghafla tunamuona kijana sheby katika mavazi tofauti kabisa tena alikuwa katika mitaa ya uswahilini,...
 
Alikuwa akitafuta chumba cha kupanga katika nyumba zile za miti,.. Si unajua mambo ya uswahilini yalivyo,.. Kijana sheby alivaa nguo za kimaskini na sijui alikuwa na nia gani,.. Ikiwa ni mida ya saa nne asubuhi hivi, alikuwa akiingia kila kijinyumba akiwa anaulizia chumba, sasa sijui ni chumba cha nini na wakati ana jumba la kifahari huko kwao,.. Uaikute mali za akina sheby ni zile zile za akina binzuluza... Kila anapoingia anaambiwa hakuna chumba, yaani ni vijumba vya miti lakini bimejaza watu balaaa...
"za saa hizi dada"
Alimkuta dada mmoja hivi ambae ni FUNDI CHEREHANI.. Alikuwa ni mzuri sana na mwenye umbo la kuvutia, tena alikuwa kajitanda ushungi wake vizuri,...
"salama habari yako"
"safi tu... Samahani dada, eti mtaa huu naweza kupata chumba dada angu"
Yaani hapo sheby alikuwa kama mtu mshamba mshamba hivi, kama vile kaja mjini juzi tu, kumbe ni mtoto wa boss wa maboss,...
"hhhmm hapo jirani kulikuwa na chumba sasa sijui kilipata mtu"
"kipi hicho"
"nyumba hio hapo"
"jamani dada angu kwanini siniangalizie kama kina mtu au laa"
Jamani huyo mtoto alipoamka, yaani sheby alibakia mdomo wazi, mtoto mzuri, mweupe, shepu ya maana, afu mpole, mbaya zaidi alionekana kuwa mtu wa dini sana, kazi yake ni kushona nguo hapo barani katika nyumba ya jirani alafu kwake ndio hapo hapo anapokwenda kuonyesha chumba,...
Sheby aliomba tu apate chumba maeneo hayo,..
Basi dada huyo alikifungua chumba hicho kisha na kukuta hakikuwa na kitu chochote ila kilikuwa kimebomoka kidogo katika ukuta
"kaka, hakina mtu ila kimebomoka kidogo ukutani"
"ebu nikione.... Ahhhhhh hiki hiki kinafaa, mladi watu wasione ndani.. Sasa mwenye nyumba yupo wapi"
"labda nimpigie simu"
"hebu fanya hivyo basi dada angu"
Basi mtoto wa kike huyo mwenye uzuri wa kila kona, japo alikuwa ni mtu wa kucheka cheka hivyo lakini katulia kiukweli,.. Kavaa hijabu lakini bado umbo limejichora tu,.. Yaani sheby alitoa macho kama mbwa mwizi.... Basi mwenye nyumba alipigiwa simu na kusema kuwa anakuja kuongea na mpangaji huyo mpya... Lakini sheby kaumiza kichwa sana kuhusiana na hio sehemu.. Lakini akapata wazo..
"Samahani dada yangu naomba tuongee kidogo"
 
Sheby alimwita mpaka kwenye chumba hicho hicho lakini mtoto huyo hakuta wakae kwenye hicho chumba ambacho hakikuwa na chochote,...
"karibu ndani, kwani hapo hakuna cha kukalia"
Mdada huyo alimkaribisha sheby ndani kwake,... Lakini sheby baada ya kukaa kwanza kenye kochi, alijikuta anaanza kushangaa mazingira ya hapo ndani yalivyo,.. Makochi yalikuwa yamechakaa, kitanda chenyewe ni tano kwa nne (5×4), alishngaa mrembo kama huyu ataishije kwenye mazingira kama hay, afu mbaya zaidi haoni hata aibu kumkaribusha mtu, kana kwamba kesharidhika na maisha hayo, yaani hapo anahisi ndio kafika na kazi yake ya kushona...
"kaka karibu ukae"
Dada alizidi kumkaribisha bila kujua kuwa sheby kuna jambo analiwaza kichwani mwake na huenda likawa faida kwake.... Lakini sheby ile kupiga jicho katika mguu wa kitanda kuna kitu kaona, kilichomfanya mapigo ya moyo kumwenda mbio.. Sasa dada kumwangalia sheby usoni aligundua alikuwa anaangalia nini... Maskini dada wa watu alijiskia aibu ya mwaka...

Je? Sheby Kaona nini hapo ndani??.... Na je?
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 11
ILIPOISHIA:
Baada ya kumjibu jambo lililonishitua zaidi ni pale aliponiambia kuwa ilibainika Shenazia alikuwa ni mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Amana siku iliyopita na kutoroshwa, hoja ya msingi ilikuwa mimi nilimtoa wapi na utetezi wangu ni upi juu ya kuhusika kwenye tukio lililompata!
SONGA NAYO…

MACHO yalinitoka pima nikimtazama yule askari aliyekuwa amekaa mbele yangu akinihoji maswali mfululizo huku akiwa amenikazia macho. Nilijiuliza niseme nini hata askari huyo anielewe bila kupata majibu, ukweli ni kwamba japo moyoni nilifahamu sikuwa kabisa na hatia katika kila kilichokuwa kinaendelea juu ya Shenaiza lakini ilikuwa ni vigumu kuuelezea ulimwengu hata ukaniamini kuwa nilichosema ndicho kilikuwa kweli.
Moyoni nilizidi kugubikwa na majuto, nilifahamu fika hayo yote yaliyonitokea nilijitakia maana kama si ujinga wangu wa kumuamini msichana ambaye sikuwa ninafahamiana naye zaidi ya kuwa na mawasiliano naye kwenye simu nisingefika hapo nilipokuwa.
Huku hayo yote yakiendelea ndani ya akili yangu yule askari alizidi kunisisitiza kujibu maswali aliyokuwa ananiuliza, machozi yakinitiririka niliamua kufunguka kwa mara nyingine ukweli wote kuhusu mimi na Sheneiza. Kuanzia tulivyoanza kuwasiliana na hata nilivyopata taarifa kuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana na yote yaliyoendelea baada ya hapo.
Askari yule alikuwa ananisikiliza kwa makini huku akiandika kwenye kitabu chake kidogo (diary), nafkiri mambo muhimu kutoka katika maelezo yangu niliyompa. Hakuacha kunihoji maswali kwa ajili ya kupata uhakika kwa yale niliyokuwa ninamuelezea baada ya saa zima la mahojiana alimuita askari polisi aliyekuwa zamu akamtaka kunirudisha nyuma ya nondo.
Siyo siri kila kitu ndani ya maisha yangu niliona kuwa kilikuwa kimebadilika na kuwa kigeni mana hata siku moja sikuwahi kufikiri ningeingia mahabusu hasa kwa sababu kama hiyo iliyonipeleka wakati huo.
Nikiwa katika chumba hicho cha mahabusu machozi yalikuwa yanazidi kunibubujika mfururizo. Tofauti na mawazo niliyokuwa nayo hali halisi ilikuwa inatisha, hakukuwa na hewa ya kutosha maana kidirisha pekee kilichokuwepo katika chumba hicho kilikuwa kidogo na kilikuwa juu, kila mmoja alikuwa anagombania aweze kupata hewa kwa kuwa karibu na dirisha.
“Eee Mungu, naomba uniokoe katika mtihani huu, ni mkubwa sana kwangu, nashindwa kuhimili, onyesha miujiza yako ili maisha yangu yasiishie pabaya,” niliwaza huku machozi yakiendelea kunibubujika.
“Wewe vipi mbona unalialia, humu kiumeni unatakiwa kujikaza,” nilisikia sauti ikiniambia kutoka pembeni yangu.
“Mtoto wa mama huyu, humu ndiyo ubayani, hakuna baba wala mama, suipojikaza utaolewa,” alisema mtu mwingine.
Niligeuza uso wangu na kuwatazama kwa zamu hao waliokuwa wanazungumza, wote walionekana kuwa watu wa miraba minne tena wenye makovu mengi usoni, macho yangu yaliganda kwao kwa sekunde kadhaa kisha nikayatoa bila kujibu neno lolote lile.
Saa zikazidi kusonga mbele kwa tabu sana upande wangu nikiwa ndani ya chumba hicho cha mahabusu, majira ya mchana rafiki yangu Justice na Raya walifika katika kituo hicho cha polisi kufanya mipango ili niweze kuachiwa kwa dhamana.
Lakini suala hilo lilionekana kuwa bado gumu sana, polisi hawakuhitaji kabisa kuwasikiliza maana hata pale walipojaribu kuuzunguka mbuyu kwa kuhonga pesa kwa baadhi ya askari wenye nguvu ili angalau nitoke nje kwa dhamana huku upelelezi ukiendelea waliambiwa wasiwe na haraka kwanza maana ishu yenyewe haikuwa ndogo.
Waliambiwa wapelelezi walikuwa wameivalia njuga kesi hiyo na suala la muhimu kama kweli nilikuwa sihusiki katika mipango ya kumuua Sheneiza ilikuwa ni kusali kwa nguvu zote ili msichana huyo aweze kupata nafuu hata azungumze ukweli mzima wa nini kilimtokea mpaka akawa anaandamwa na watu waliokuwa wanataka kupoteza maisha yake.
Rafiki zangu hawakuwa na namna ya kulazimisha kama walivyokuwa wanataka wao, walichofanya ilikuwa ni kuomba ruhusa ya kuzungumza na mimi japo kwa dakika chache tu. Kwa kuwa kuna chochote walikuwa wamekwishapenyeza kwa askari hao hilo halikuwa suala gumu sana, waliruhusiwa, nikatolewa mahabusu na kwenda kuzungumza nao.
“Haya yote yatakwisha, hutakiwi kujali kabisa baba, jipe moyo kila kitu kitakuwa sawa,” Raya aliniambia huku machozi yanambubujika kwa wingi.
“Asante Raya, ninaamini hivyo pia, Mungu atanisimamia na kila kitu kitakwenda sawa.” Nilimjibu.
“Hapa kaka ni muhimu kuomba kwa nguvu zote huyo mgonjwa maendeleo yake yawe mazuri ili aeleze ukweli mzima wa nini kimetokea, hicho pekee ndicho kinachoweza kukutoa kwenye hii hatia,” Justice aliniambia.
“Ndivyo askari walivyosema?”
“Ndiyo, mimi pia ninaunga mkono suala hilo maana hakuna njia nyingine ya kukunusuru.”
“Dah! Kwani Sheneiza amelazwa wapi?” Nilimuuliza Justice swali lingine.
“Yuko Mwananyamala hospitali lakini sijafahamu amelazwa katika wodi namba ngapi.”
“Fuatilia kaka ufahamu pia na maendeleo yake maana huyo ndiyo kila kitu kwenye hili suala kama unavyosema. Lakini kuna kitu pia nilikuwa ninakifikiria ambacho tunaweza kuzungumza na askari polisi wazidishe ulinzi katika hospitali hiyo kutokana na hali halisi, hao watu wanaotaka kumuua wakigundua kuwa bado ni mzima lazima wataendelea kumuandama.”
“Hilo ni kweli kaka, niachie mimi, nitazungumza na mkuu wa kituo maana ni mtu mzuri, ametupokea vyema mimi na Raya.”
Baada ya kuzungumza mawili matatu na rafiki zangu hao ambao walionekana kuniunga mkono kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kunifariji katika matatizo yangu hayo yaliyokuwa yananisonga, nilirudishwa mahabusu na wao walikwenda kama tulivyozungumza kwa mkuu wa kituo na kumwambia juu ya kuongeza ulinzi kwenye Hospitali ya Mwananyamala.
Hatimaye siku hiyo ilimalizika nikiwa ndani ya kituo hicho cha polisi, siku iliyofuata majira ya asubuhi Raya alikuwa kituoni hapo kwa ajili ya kuniletea kifungua kinywa. Ukweli ni kwamba hakuna wakati niliyomuona Raya kuwa ni mtu wa muhimu kwangu kama wakati huo nilipopata matatizo.
Huko nyuma nilikuwa mtu wa kumchukulia poa sana kwa vitendo vyake vya kuonyesha kuwa ananipenda lakini wakati huo thamani yake niliiona na niliamini kweli mwanamke huyo alikuwa ananipenda kwa dhati.
Baadaye Raya aliondoka na mimi niliendelea kukaa kwenye chumba kile cha mahabusu ambapo mchana nikiwa sina hili wala lile nilishituka baada ya kumuona askari polisi akija kwenye nondo na kuita jina langu, nilipoitika alinichukua mpaka mapokezi nikapewa nguo zangu na kuambiwa nivae, baada ya kuvaa akanitaka nimfuate kuelekea nje, nilifanya hivyo na tulipoanza tu kutoka nje askari wengine watatu walioshika mtutu wa bunduki mkononi walitufuata nyuma tukaenda kuingia pamoja kwenye difenda.
Difenda hilo liliwashwa na kuanza kuelekea mahali ambapo sikuweza kupafahamu kwa mara moja, nilikaa kimya katikati ya askari hao bila kuzungumza neno lolote lile na safari ikazidi kupamba moto. Nilikuja kugundua kuwa huenda tunaelekea Mwananyamala Hospitali baada ya kuumaliza Mtaa wa Makumbusho na kushika barabara ya Mwananyamala, moyoni nilianza kugubikwa na maswali mengi, nilijiuliza kama ni kweli ninapelekwa katika hospitali hiyo ilikuwa ni kufanya nini?
Je, nini kitaendelea kwenye simulizi hii? Usikose next issue!
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 12
ILIPOISHIA:
Nilikuja kugundua kuwa huenda tunaelekea Mwananyamala Hospitali baada ya kuumaliza Mtaa wa Makumbusho na kushika Barabara ya Mwananyamala, moyoni nilianza kugubikwa na maswali mengi, nilijiuliza kama ni kweli nilipelekwa katika Hospitali hiyo ilikuwa ni kufanya nini?
SASA ENDELEA…

“Tumekuleta huku hospitalini kwa sababu kwanza maelezo uliyoyatoa kituoni, kwa kiasi fulani yanapishana na maelezo aliyoyatoa huyu mgonjwa kwa sababu wewe ulisema humfahamu kwa undani zaidi ya kuanza kuwasiliana naye kwenye simu siku chache zilizopita.
“Lakini yeye amesema wewe ni mpenzi wake wa siku nyingi, mna mipango ya kufunga ndoa na tayari ana ujauzito wako,” alisema askari mmoja wa kike, miongoni mwa wale waliokuja kunichukua mahabusu, wakati huo tukiwa tayari tumeshawasili Hospitali ya Mwananyamala.
Akaendelea: “Lakini kingine ni kwamba amekataa kutoa ushirikiano wa kueleza nini kilichotokea mpaka wewe uwepo ndiyo maana tumekufuata, hutakiwi kuzungumza chochote, umenielewa?”
Nilitingisha kichwa kuonesha kukubali kile alichokisema. Mfululizo wa matukio ya kushangaza ulikuwa unaendelea, nilijiuliza iweje tena Shenaiza awaeleze polisi kwamba mimi nilikuwa mpenzi wake na kwamba tulikuwa na mipango ya kufunga ndoa?
Yote tisa, kumi nilijiuliza iweje awaambie kwamba alikuwa na ujauzito wangu wakati hatukuwahi kukutana kimwili hata mara moja? Kama kweli alikuwa mjamzito, mimi nilikuwa nahusikaje? Nilikosa majibu.
“Jamal! Ooh my God! Thanks for coming my dear,” (Jamal! Ooh Mungu wangu, ahsante kwa kuja mpendwa wangu) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini akionesha kwamba yupo kwenye maumivu makali, alizungumza kwa Kiingereza kizuri huku akitanua mikono yake kama ishara ya kunitaka nimkumbatie.
Sikuwahi kumsikia akizungumza Kiingereza, nikabaki na swali jingine lakini sikutaka kumuonesha chochote, nikalilazimisha tabasamu usoni kwangu, nikamuinamia pale kitandani alipokuwa amelala, dripu ikiendelea kutiririka kwa kasi kuingia mishipani mwake, nikamkumbatia, akanibusu shavuni na kuning’ang’ania kifuani kwake, tukiwa kwenye hali hiyo alinibusu mdomoni na kunifanya nijisikie aibu ndani ya moyo wangu.
Kwa jinsi alivyokuwa akinidekea, mtu yeyote angeweza kuamini kwamba kweli sisi ni wapenzi wa muda mrefu, nikageuka na kumtazama yule askari ambaye moyoni ni kama alikuwa anasema ‘unabisha nini sasa? Kama siyo mpenzi wako angekubusu mdomoni?’.
“Please help me Jamal, they want to kill me! You are my only savior,” (Tafadhali nisaidie Jamal, wanataka kuniua! Wewe ndiyo mkombozi wangu wa pekee) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini akiwa bado amenikumbatia. Japokuwa yule askari alikuwa mita chache tu kutoka pale kitandani, hakuweza kusikia chochote.
Kwa kuwa nilishaambiwa sitakiwi kuzungumza chochote, sikumjibu chochote zaidi ya kumtazama usoni huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua hao anaosema wanataka kumuua ni akina nani na ilikuwaje mpaka watake kumuua?
“Inatosha sasa, hebu kaa pembeni. Binti, naamini sasa utatoa ushirikiano maana uliyekuwa unamtaka tumeshamleta,” alisema yule askari huku akinielekeza kukaa pembeni ya kitanda cha mgonjwa, akarudi kinyumenyume na kufungua mlango, askari wengine watatu, akiwemo yule aliyenihoji mimi wakaingia na kusimama kwa kutuzunguka.
Yule askari wa kike akawaeleza jambo kwa sauti ya chini ambayo mimi na Shenaiza hatukusikia kisha tukawaona wote wakitoka, akabaki yule mmoja aliyenihoji mimi siku iliyopita, mkononi akiwa na ‘diary’, akavuta kiti na kukisogeza karibu na pale Shenaiza alipokuwa amelala.
“Si umeshaambiwa maelezo yote kwamba hutakiwi kuzungumza chochote?” yule askari ambaye nilishamtambua kwamba ni mpelelezi, aliniambia.
“Ndiyo.”
“Oke vizuri, binti unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri,” alijibu Shenaiza, akamwambia anataka kuanza upya kumhoji na anaamini atatoa ushirikiano kwa sababu mimi nilikuwepo.
“Jina lako kamili unaitwa nani?”
Shenaiza alinitazama kabla ya kuanza kujibu, akanionesha ishara ambayo sikuielewa, nikabaki kumtazama tu huku na mimi nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia maelezo yake maana kiukweli hata mimi sikuwa namfahamu kwa undani.
“Shenaiza Petras Loris,” alijibu Shenaiza. Nilishangazwa na jina lake, sikuwahi kusikia Mtanzania yeyote akiwa na jina hilo, akilini nikaanza kupata majibu kwamba kile nilichokuwa nakihisi awali kwamba msichana huyo hakuwa Mtanzania kutokana na mwonekano wake kilikuwa kweli.
Yule askari aliendelea kumhoji maswali kama polisi wote wanavyofanya, akafikia swali la kabila na utaifa wake, Shenaiza akanitazama tena na kushusha pumzi ndefu kisha akamjibu:
“Kabila langu ni Aethikes,” alijibu, yule askari akapigwa na butwaa na kuacha kuandika, akamtazama Shenaiza kwa muda kisha akanigeukia na mimi, mshangao aliokuwa nao ulikuwa sawa na niliokuwa nao mimi.
‘Bini, hebu kuwa ‘serious’, hilo ndiyo kabila gani? Tangu nianze kufanya kazi huu mwaka wa kumi sasa sijawahi kusikia kabila kama hilo hapa Tanzania, hebu taja kabila lako,” alisema yule askari kwa sauti iliyoonesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
“Mimi siyo Mtanzania, natokea Greece (Ugiriki), asili yetu ni Attica, baba yangu amezaliwa na kukulia kwenye Jiji la Athens lakini mama yangu ni mpare wa Mtae, Lushoto mkoani Tanga ndiyo maana unaona naweza kuzungumza Kiswahili vizuri,” alisema msichana huyo huku akionesha kujiamini mno.
Nilimuona yule askari akiandika maelezo hayo kwenye ‘diary’ yake, akaendelea kumhoji maswali mengine ambapo niligundua kwamba msichana huyo, alikuwepo nchini kisheria na kubwa zaidi, kumbe alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mahojiano yaliendelea, kikafikia kipengele cha muhimu ambacho ndiyo hasa nilichokuwa nakisubiri kwa shauku kubwa, cha kutaka kujua nini kilitokea mpaka msichana huyo mrembo akajeruhiwa vibaya na kwenda kulazwa Hospitali ya Amana kabla ya mimi kumsaidia kutoroka mpaka nyumbani kwangu, na kile kilichokuwa kimetokea nyumbani kwangu usiku.
Shenaiza alivuta pumzi ndefu baada ya kuulizwa swali hilo, akazishusha kisha akatulia, ukimya mkubwa ukapita kati yetu mle wodini. Ilibidi yule askari avunje ukimya na kurudia tena kumuuliza swali lile lakini badala ya kutoa majibu kama alivyokuwa akifanya kwa maswali yote, alikaa kimya huku machozi mengi yakimtoka na kulowanisha uso wake.
‘Kijana hebu naomba utupishe mara moja, toka nje nitakuita,” alisema yule askari, ikabidi nitii, nikawaacha wenyewe wawili mle wodini.
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 13
ILIPOISHIA:
Ilibidi yule askari avunje ukimya na kurudia tena kumuuliza swali lile lakini badala ya kutoa majibu kama alivyokuwa akifanya kwa maswali yote, alikaa kimya huku machozi mengi yakimtoka na kulowanisha uso wake.
“Kijana hebu naomba utupishe mara moja, toka nje nitakuita,” alisema yule askari, ikabidi nitii, nikawaacha wenyewe wawili mle wodini.
SASA ENDELEA…

Nilihisi kichwa changu kikipata moto, nilikuwa na shauku kubwa mno ya kutaka kuufahamu ukweli wa kilichokuwa kimemtokea Shenaiza. Lile swali la awali kwamba yeye ni nani, tayari nilishapata majibu kwa kiasi fulani lakini bado nilitaka kujua nini hasa kilichomtokea.
Mazungumzo kati ya Shenaiza na yule mpelelezi kule ndani yaliendelea kwa muda na baada ya kama dakika kumi na tano kupita, mlango ulifunguliwa na yule mpelelezi akatoka, akanionesha ishara kwamba niingie ndani.
Nikaenda ambapo nilimkuta Shenaiza akiwa anajifuta machozi, macho yake yakiwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu sana.
“Come to me Jamal, you are my comfort,” (Njoo Jamal, wewe ndiyo faraja yangu) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini, nikamsogelea pale kitandani na kumkumbatia, akanibusu shavuni na kuniomba radhi kwa kilichotokea.
“Unaniomba radhi kwa nini Shenaiza?”
“Najua hujajisikia vizuri kwa mimi kuzungumza kilichonitokea wakati wewe ukiwa nje, nilitamani na wewe usikie lakini naona kwa sasa siyo muda muafaka lakini nakuahidi kwamba muda mfupi ujao nitakueleza wala usijali,” alisema Shenaiza huku akiendelea kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.
Nilimtoa wasiwasi na kumtaka awe huru na mimi, akaniachia kisha nikakaa pembeni ya kitanda chake.
“Walitaka kuniua jana, yaani ni Mungu tu na naamini hata wao wanajua kwamba nimekufa, wamenipiga sana,” alisema Shenaiza na kuniambia anajisikia vibaya sana kuniingiza kwenye matatizo ambayo wala hayakuwa yakinihusu.
“Nakuomba sana nikishapata nafuu kidogo tu tuondoke, hata ikibidi kwenda kuishi hotelini mimi nitagharamia kila kitu maana wanaweza kurudi tena kule nyumbani kwako kwa sababu wanaamini kwamba nimeshakwambia kila kitu kinachoendelea.”
“Kwa hiyo unataka kusema wanaweza tena kurudi nyumbani kwangu?”
“Ndiyo! Wanaweza kurudi na kukudhuru bure wakati hauna hatia yoyote,” alisema Shenaiza, kauli ambayo ilinishangaza na kunijaza hofu kubwa moyoni. Kuna wakati nilikuwa najuta sana kwa kujiingiza kwenye mdomo wa mamba bila kujua.
Shenaiza aliendelea kuniongelesha mambo mbalimbali lakini wala akili yangu haikuwa pale, nilikuwa nikiwaza mambo tofauti kabisa. Baadaye nesi aliingia na kunieleza kwamba mgonjwa alikuwa anahitaji kupumzika kwa hiyo nitoke na kumuacha peke yake.
Shenaiza alikuwa mbishi kidogo lakini baadaye alikubali, akaomba kabla sijatoka nimbusu, nikamuinamia pale kitandani kwa lengo la kumbusu kwenye shavu lake lakini alinishika shingoni na kunivutia kwake, ndimi zetu zikagusana na kunifanya nipigwe na ganzi kwa sekunde kadhaa, aliponiachia, nilibaki nimeganda vilevile mpaka nesi aliponishtua.
“Inabidi uende nje kaka ili tumhudumie mkeo kisha apate muda wa kupumzika,” alisema yule nesi, nikashtuka kama mtu aliyekuwa usingizini, nikageuka na kumtazama Shenaiza pale kitandani, akanifinyia jicho lake moja na kunibusu kwa mbali, nikatoka mpaka nje huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu.
“Jamal! Uko salama mpenzi wangu? Nakupigia simu lakini sikupati mpaka imebidi nije huku,” alisema Raya ambaye aliponiona tu nikitoka wodini, alikuja na kunikumbatia kwa nguvu, akionesha kuwa na hofu kubwa na ukimya wangu.
Hata hivyo sikumtilia sana maanani, japokuwa nilitoka nikiwa natabasamu, nilipomuona nilikunja sura, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa simu, nikagundua kuwa kumbe kweli ilikuwa imejizima bila mimi kufahamu, nikaiwasha na kusogea mpaka pembeni kulikokuwa na mabenchi, nikakaa. Raya naye akaja na kukaa pembeni yangu, akawa na shauku kubwa ya kutaka kusikia chochote kutoka kwangu.
“Niache kidogo Raya, akili yangu haijatulia kabisa, tutazungumza baadaye,” nilimjibu msichana huyo kwa kifupi, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kutulia kimya. Maskini Raya! Alionesha kuwa na hisia nzito juu yangu lakini kwa bahati mbaya mwenzake nilikuwa namchukulia kawaida sana.
Sote tukiwa kimya kabisa, nilikumbuka kilichotokea kati yangu na Raya usiku na kujikuta nikishindwa kumeza chakula nilichotafuniwa, nikageuka na kumtazama usoni, naye akanitazama, nikagundua kwamba alikuwa akilengwalengwa na machozi.
“Najua hunipendi Jamal lakini hiyo isiwe sababu ya kuninyanyasa, nakupenda sana mwenzio kuliko mtu yeyote chini ya jua, naamini ipo siku utaujua ukweli,” alisema msichana huyo, nikarudia kumsisitiza kwamba aniache kidogo hayo mambo tutayajadili baadaye, safari hii nilizungumza kwa sauti ya chini nikiwa kama nambembeleza f’lani, nikamuona ametulia.
Nikiwa nimekaa pale, nilimuona yule askari mpelelezi akiwa na wenzake, nikamuomba Raya anisubiri hapohapo, nikainuka na kumfuata huku bado nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua alizungumza nini na Shenaiza.
Hata hivyo, licha ya kumfuata askari huyo na kumuomba anidokeze alichoelezwa na Samantha, alikataa katakata kwa maelezo kwamba atavuruga upelelezi, nikakosa cha kufanya. Nilirudi hadi pale nilipokuwa nimemuacha Raya, nikakaa pembeni yake huku nikiwa kimya kabisa.
“Nakushuru kwa jinsi ulivyojitoa kunisaidia katika haya matatizo yanayonikabili,” nilivunja ukimya na kumsemesha Raya, nikamuona akiinua uso wake ambao muda wote alikuwa ameuinamisha chini, akanitazama huku tabasamu hafifu likichanua kwenye uso wake.
“Usijali Jamal, nipo kwa ajili yako na kamwe sitakuacha peke yako hata iweje.”
“Yaani japokuwa ulikuwa unalia lakini macho yako yamezidi kuwa mazuri,” nilimtania Raya, akashindwa kujizua na kucheka kwa nguvu. Hakuna kitu alichokuwa anakipenda Raya kama kusikia kauli yoyote ya kumsifia kutoka kwangu. Ile huzuni aliyokuwa nayo, iliyeyuka kama theluji juani, akachangamka kabisa.
“Na leo si tutaenda kulala pamoja nyumbani kwetu?”
“Kwani wazazi wako bado hawajarudi?”
“Bado!”
“Ok, tutaangalia itakavyokuwa,” niliamua kumjibu hivyo Raya ili kumridhisha ingawa ukweli ni kwamba kauli hiyo haikuwa imetoka ndani ya moyo wangu. Wakati tukiendelea kuzungumza, niligundua jambo lisilo la kawaida.
Mita chache kutoka pale tulipokuwa tumekaa, kulikuwa na maegesho ya magari. Magari mengi yalikuwa yameegeshwa lakini miongoni mwa magari hayo, ndani ya gari moja kulionekana kuwa na watu zaidi ya mmoja ambao baadaye nilikuja kushtukia kwamba walikuwa wakitutazama sana mimi na Raya pale tulipokuwa tumekaa na zaidi walikuwa wakiniangalia mimi.
Nilipogeuka haraka na kuwatazama, macho yangu na yao yaligongana lakini wakazuga kwamba hawakuwa wakinitazama, wakawa wanaendelea na mazungumzo yao.
“Kwani nini wananitazama mimi?” nilijikuta nikizungumza kwa sauti, Raya akashtuka na kuniuliza nilikuwa namaanisha nini? Nikataka kumzuga lakini haikuwa rahisi, akafanikiwa kugundua kuwa nilikuwa nawatazama watu gani.
“Hata mimi nimewaona muda mrefu tu, tangu unatoka wodini walikuwa wakikutazama lakini sikuwatilia maanani.”
“Tuondoke!” nilisema huku nikiinuka pale nilipokuwa nimekaa kwani tayari kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu, Raya naye akainuka, tukaanza kuelekea kwenye lango la kutokea nje ya hospitali hiyo lakini cha ajabu zaidi, tukiwa getini tunataka kutoka, nililiona lile gari nalo likija kule tulipokuwepo.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom