Muziki: Ninatoa Vyeti
Ninaamini kabisa umekuwa na wikend nzuri na ndiyo maana Jumatatu hii umeainza na tabasamu kuubwa, sikuonei wivu kwa kutabasamu japo mimi nilikuwa na wakati mzuri sana. Yeah, ilikuwa nzuri sana, mnamjua anko wangu, mmh, huyu huyu ambaye huwa ananisaidia masuala ya kiuchumi, basi bhana kwanza kabisa kapewa cheti mapema tu na kala shavu japo haijatangazwa.
Mtashangaa sana maana anko wangu kasomea mambo mengine kabisa lakini hili shavu alilopata ni la masuala mengine kabisa, ilmradi tu potelea mbali, nani anahoji? Ukihoji, hutajibiwa na anayetakiwa kukujibu bali wapo wanaotegemea kuishi kinafki watakufata na kukufanyia mambo yasiyojulikana. Kwa minajili ya kufurahia anko kupewa cheti nami naandaa utaratibu wa kugawa vyeti humu. Ila kukipata ni lazima ukasome na ulete ushahidi wa cheti humu and then ninakupa cheti. Cheti cha kuona cheti chako, na ulete cha ufaulu sio cha mahudhurio.
Muziki sasa, asubuhi anko wangu, sio yul mnayemjua, huyu mwingine kanishawishi na namna alivyowaelezea watoto wa MJ, sio master jay bali mfalme mwenyewe Michael Jackson na sasa nakuletea video yake ninayoipenda nikiamini nawe utaipenda.