Makapuku Forum

Makapuku Forum

71a86ff68fc53f5083f00d425862438d.jpg
Aiseee
 
THE DOM

Sehemu Ya 25

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

hallo mama yangu mzazi shkamoo"
Aliipokea kwa furaha kubwa sana lakini ghafla anasikia
"sheby mwanangu, usije huku na usilete hicho kitu wanachokitaka... Baba yako kaniteka huku ananitesa sana... Usije tafadhali sana baba"
Ilikuwa ni sauti ya mama yake,.. Lakini ukweli wa mama wa sahi ni mke wa rais GU, hivyo huyu ndio ndio mama wa Joseph...
Mara ghafla sauti ikabadilika
"kama unampenda mama yako, utaileta hio dom,.. Nadhani unanijua mimi baba yako, siangalii huyu ni mke wangu au laaa,... Naua kama usipoleta hio dom hapa... "
Aliongea general Nyange lakini kwa mbali sahi akasikia sauti ya mama yake ikisema
"mwanangu usijeeeeee, acha nife tu"

ENDELEA.......

Sahi aliisikia hio sauti,... Lakini sasa kumbe ile simu ya siri ambayo ni simu ya sikioni, ina uwezo wa kuvuta sauti ya simu nyingine ya upande wq sikio lingie, hivyo mheshimiwa rais GU kasikia kila kitu,.... Sahi alipotaka kukata simu ghafla General akasikika akisema kuwa
"na kama unakuja, njoo katika msitu wa sentago mbele ya kambi ya TMA haraka sana laa sivyo mama yako hutomwona tena"
Sahi alikataka simu, kisha akapanda gari mpaka Airport,... Sahi hawezi kuacha mama yake afe kwasababu ya dom,.... Huezi amini sahi anaipeleka dom kwa general Nyange ili mama yake aachiwe...

Huku msituni,... Huezi amini Joseph ndio wa kwanza kumwazibu mama yake sahi, lakini bila kujua anamwazibu mama yake mzazi,..
"Joseph mwangu, leo wewe ni wa kunipiga kibao mimi... Ahsante sana baba"
Aliongea mama huyo ambae ndio mama Joseph originally,...
"mimi nataka kupiga pesa, sasa nitaonaje haya kukupiga makofi... Tena usinisemeshe (tasi)"
Joseph alikuwa ni katili wa kimya kimya,... Mama alikuwa akilia sana na yupo tayari kufa lakini mtoto wake asije...

Sasa je mama kajuaje kama yule alikuwa ni sheby wake... Kama unakumbuka siku ile sahi alipokuwa katangulizana na Joseph kwenda Airport kubadilishana dom, walikutana na mama huyo njiani.. Sasa sahi alipoingia ndani ya gari ya yule mama alimwambia kila kitu, kiwa yeye ni sheby, ila hapo alipo amefanyiwa plastic surgery katika uso wake, lakini baada ya kazi atavuliwa sura hio na kubaki na sura yake originally,... Hivyo kumbe kweli Joseph alichokisema kuwa sahi ni sheby ila kafanyiwa plastic surgery katika uso wake na ndio mana hafanani na mtu ispokuwa sauti na mwendo ndio mana wengi walimdhania kuwa sheby, ila ni kweli ni Sharbiny Rashidy,...

Usafiri wa ndege sio wa mchezo mchezo,.. Kwani alichukuwa muda??.. Dakika kadhaa tu tayari yupo ndani ya eneo alilo agizwa,... Sasa tunamjua kama sheby na sio sahi,.. Alipofika kwanza alichungulia katika hio kambi mpya,.. Aliona mama yake anateseka sana ila hajui kama huyo sio mama yake,...

Sahi alijitokeza huku akiwa kanyoosha mikono juu,... General alipoona dom imefika, alimchapa mkewe kibao cha mwisho mwisho... Hajakaa vizuri Joseph nae akamchapa mama sahi kibao cha mwisho mwisho, hio sahi aliiona,..
"haaaa Joseph, yaani hata wewe unadiliki kumpiga kibao mama... Joseph tumelelewa na huyu mama leo unampiga kofi"
"haikuhusu we fara nini, tupatie dom hio"
"mfungulieni mama kwanza.. Laa sivyo naipigiza chini tuikose wote"
General anakijua kichwa cha mtoto wake, hashindwi kweli kuipasua hapo chini,.. Basi mama akafunguliwa na kumkimbilia mtoto wake na kukumbatiana,... Sasa kumbe walishapanga sahi auwawe baada ya kutoa dom,... Sahi akawarushia dom yao,... Sasa nyuma ya dom kuna target imemlenga,.. Mama si kaiona, akamgeuza sahi ile risasi ikampata mama, sasa kile kitendo cha General kuzubaa, sahi saa mingi sana keshachukuwa bastola ya baba yake, kitu cha kwanza alianza na wapambe waliozunguka eneo hilo, utamu ni kwamba kila risasi alioitoa haikuwa ya hasara... Wakati huo. Mama yupo. Chini,... Mara bastola ikaisha risasi General anacheka tu kwa kuiona dom, sasa sahi mikono juu kwa kuguswa na ubaridi wa bunduki katika shingo yake,.... Sahi hakuwa mjinga mjinga, alionyesha umahiri wake juu ya uwezo wake,... Aliinama chini huku mguu akiuzungusha kwa nyuma kana kwamba alikuwa akimpiga mtama huyu aliekuwa nyuma yake,... Sasa jamaa aliposhangaa mtama chini, kumbe juu anapokonywa silaha yake,.. Na si mwingine bali ni Joseph,.. Sahi alipoimiliki silaha ile, cha kwanza alivunja miguu, sahi hajakaa sawa mara nae kapigwa za miguu, kuangalia ni nani, ni mwaju.. Kumbe mwaju aliungana na mr general,...sahi akawa hana ujanja tena, dom inakwenda na kutekwa katekwa...

Lakini mungu sio asumani, gharama kunatua helikopta kubwa sana ilioshusha makomando wapatao 15 ndani yake dokta alikuwepo, sasa hatuji dokta ni wa nini.... Sasa kumbe mr gu alikuwa akiifuatilia ile simu, mana alisikia mazungumzo,.... Viwanajeshi vyote vilivyodanganywa na generally Nyange vilipukutishwa vyote, sasa wamebaki watatu tu General nyange, General Deo, na Joseph ambae kavunjwa miguu na sahi,,.. Mara ghafla dokta anashuka na mke waraisi,.. Dokta kitu cha kwanza alimpa huduma ya kwanza mama yake sahi, uzuri ni kwamba risasi haikupiga sehemu mbaya,.. Hivo huduma alipatiwa... Sasa mke wa raisi alipofika tu, aliita
"mwanangu sheby umzima"
Mr Nyange anashangaa, mwanae sheby,... Kivipi... Sasa Nyange hakushangaa mwenyewe tu hata mama yake sheby pia alishangaa,... Na sio mama sheby tu hata sheby mwenyewe alishangaa,...
"unashangaa nini sasa jipu mkubwa wewe"
Aliongea rais GU kwa kumwambia General nyange,...
"ivi nikuulize mr President... Kijana wangu imekuwaje mpaka sasa yupo hai"
"kijana wako?? Kijana wako ni huyo hapo chini, huyo ndio mtoto wenu"
"unasemaje mheshimiwa rais"
Mama sheby alipata hata nguvu ya kuongea
"huyu hapa chini ndio mtoto wenu"
"kivipi"
"siku ile tunaingia hospitalini na mabunduki, tumesababisha wake zetu kuchukuwa mtoto wa mwenzie... Mke wako akachukuwa mtoto wangu na mke wangu akachukuwa mtoto wako... Sasa hivi ndio tunajua hili swala, mtoto wako yule pale chini"
Aliongea raisi GU, huku akinyoosha kidole kwa Joseph,...
"afu kwanini hafanani na sura ya mwanzo"
Aliuliza generally Nyange huku akimuangalia sahi,... Sasa yule dokta aliokuja na mr GU, kumbe alikuja kwa ajili ya sahi, kwani sahi ana nini.... Dokta alimtaka sahi au sheby aje karibu yake,...
"vua shati kijana"
Dokta alimtaka sahi avue shati lake,.. Sasa kumbe sahi alishonwa nyuzi maalum katika shingo yake, na ukiangalia kwa umakini utaona kuna kiungio ila usipokuwa makini huoni kitu,.. Sasa dokta alianza kumpaka sahi mafuta fulani katika kile kiungo,.. Dakika 5 mbele, ile sehemu ilionekana kuvimba na nyuzi zilionekana, dokta ndio anajua zinatolewaje nyuzi hizo..... Dakika 10 mbele, damu zilianza kutoka katika shingo ya sahi,... Mama sasa wamama wote wanamlilia sahi, kila mtu
"jamani mwanangu unamfanyaje"
Hata mke wa rais hamtaki tena Joseph, yaani baada ya kujua huyo ndio sheby wake, hataki kusikia neno Joseph tena,... Sasa sahi ana wamama wawili...
"tulieni nyie wanawake, mnalia lia nini"
Aliongea dokta, wakati huo sahi damu zinamtoka baada ya nyuzi hizo kutolewa...

Sahi alianza kulivuta lile lingozi alilovalishwa nchini Korea, wakati alipokwenda kusoma,... Plastic surgery zipo aina tatu, kuna ya kuvaa kama likofia tu hilo halina haja ya dokta, na kuna ya kushonwa nyuzi maana yake hio sio ya kutolewa mara kwa mara na ndio hii ya sahi, afu kuna ya kufanyiwa operesheni ya usoni yaani sura yako ndio ifanyiwe operesheni ili ije sura nyingine, hio ni ya milele kabisa.... Sahi alifanikiwa kulivua lile likofia, kila mmoja haamini kama kweli alikuwa ni sheby, na ni kweli ni Sharbiny aliosadikika amekufa,.. Mwaju aliokuwa taabani kwa kuchakazwa risasi za mbavu leo anashuhudia kumwona mpenzi wake kwa mara ya pili,.. Haamini macho yake, lakini wakati huo hali yake inazidi kuwa mbaya,... Na yeye ndie aliempiga mama sahi risahi ya mgongoni....
"amaizing boy, siamini kama ni mtoto wangu aiseee"
Aliongea generally nyange ila wakati huo wapo chini ya makomando, hivyo hawakuwa na ujanja hapo walipo.. Mama sheby anajua kuwa ni mtoto wake mana alishampa taarifa kiwa hapo yupo kazini na sura nyingine...
"haya niambie, kwanini ulimfanya mtoto wangu mfu kumbe ni mzima"
Mr Nyange alimuuliza raisi GU, kuwa ilikuwaje mpaka sahi akaonekana mfu,....
"kwanza nimeshakwambia huyu sio mtoto wako, huyu ni mtoto wa Tanzania"
Aliongea rais GU huku akitoa kumbu kumbu juu ya kifo sa sheby miaka mitatu iliyopita,...

SASA HAPA NI MIAKA MITATU ILIOPITA....

Kipindi cha uchaguzi mkuu Tanzania, marais walikuwa wengi sana waliogombea nafasi hizo,.. Katika hoteli moja ya kifahari walikutana viongozi wawili, ila wakati huo hawakuwa viongozi wakubwa... Ila mheshimiwa rais alikuwa ni Waziri wa ujenzi,.. Na huyu mwingine sijui alikuwa nani lakini kwa sasa ni Waziri mkuu,..

"niambie bwana mzee wa kujaaliwa na mwenyezi mungu"
Aliongea waziri wa ujenzi, ambae kwa sasa ni rais,...
"safi tu ndugu yangu,.. Naona umeshachukuwa fomu ya kuwania urais mwaka huu"
"ni kweli... Ila nahitaji nipate vijana kama wawili watatu hivi, niwasomeshe ili nikipata urais wanisaidie kazi ya kuniletea majipu"
"aaahhh yaani unaandaa vijana kabla hujapata"
"ndio"
"ukikosa je?"
"nikikosa urais nitamuuzia mtu aliofanikiwa kupita"
"ok.. Sasa mi naona tuangalie kule jeshini, kule hatutokosa vijana"
"enheeee, umetoa wazo zuri sana... Sasa tunachukuaje kijana pale, mana sihitaji serikali ijue mipango yangu"
Aliongea waziri GU, huku mwenzie akitafakari jinsi ya kufanya,...
"mi naona tuanze na kijana mmoja kwanza"
"sawa, je ni yupi pale jeshini"
"yule mtoto wa General nyange hafai yule... Mana atakuwa na mazoezi mazuri kwasababu namuonaga sana baba yake anampa mazoezi ya private sana"
"mmmhhhh nyange ataua mtu,.. Ataua mtu nakwambia"
"sikiliza bwana mr GU,.. Hatumchukui kama tunachukuwa kuku"
"tutafanyeje sasa"
"sikiliza... Hata sisi ni wanajeshi wa kale, na unamjua vizuri General nyange ni rafiki yako... Tumchukue mtoto wake"
"sawa sikatai, ila tutamchukuaje yule"

Itaendelea.......

ITAENDELEA.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom