Muziki: Ukimya Unaopiga Kelele
Kuna kuwa kimya na kukaa kimya, haya yanatofautiana. Ngoja kwanza, usiharakie kusema mbona yote yanafanana, nani kasema. Kuwa kimya ni dhana nzima ya kujitafakari, unajitafakari tembea yako, unatafakari ufanye nini, huzungushi ulimi. yeah, huzungushi ulimi maana hata ukimpa ulimi unayempenda ulimi utaongea na huku ndo kukaa kimya na kuwa kimya ni kelele zenye sauti ya nyangumi. Huelewi, well, hatushindani kufikiri maana leo ni furahiday na always I take this delicious day very easy, and hate those making obnoxious noise na kuusumbua ukimya wangu.
Napita tu, kimya kimya, napekua usisikie kelele zangu nikiwasalimia
shululu ambaye sichoki kusoma magazeti, unanianzishia siku kwa uzuri kabisa. Nakushushukuru
Jimena kwa historia na wine ya Ximena bila kusahau Chi seeds (nikajua ni 'kai square'), asante
Shunie kwa sala, sijakusahau
Madame S , picha zinaongea sana na ndizo zimenivuta kuandika ninachoandika leo.
Asante
Bitoz kwa kutia chachandu, sijakusahau
husna muba sichoki kukukumbuka,
Tumosa ujue safari yangu nakutegemea,
Sakayo ujue
Transcend leo kabamba Jukwaa kwa picha nzuri. Na
Clkey ,
mzeewakungoa ,
Nyagei ,
Mondray ,
shedede ,
koncho77 ,
Mkushi wa kusi Mndali ndanyelakakomu lee empire , na wewe msomaji mnajijua kabisa bila nyinyi jukwaa hili linabaki kuwa kama majukwaa mengine tu ya kawaida. Uwepo wenu hapa unaifanya KF iwe hot na wengine kupiga miayo ya njaa kama wapishi wa hotel.
Muziki sasa; hey, sijarudi bado sema hii furahiday nimekaa naangusha mbuyu hapa kwa taratibu maana asubuhi inaanza kama jumatatu