Makapuku Forum

Makapuku Forum

THE DOM

Sehemu Ya 11

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

Sasa sahi alipokuwa barabarani, kuna gari aliiona, na anaijua hio gari, wakati huo Joseph yupo nyuma ya sahi, na sahi yupo mbele, sasa sahi kaona gari ya mama mmoja hivi anamjua vizuri,... Sasa ile gari ya yule mama ikapaki pembeni,... Sahi alishindwa kuvumilia kumpita huyo mama,.... Sasa hata Joseph pia anaijua hio gari ya huyo mama,... Lakini yeye hakutaka kusimama... Ila hofu ilimjia mr Joseph, kwanini sahi kasimama kwa ajili ya huyo mama... Mama huyo ni mke mkubwa wa General Nyange, yaani mama wa yule marehemu itwae Sharbiny,... Sasa Joseph anashangaa, huyu sahi amemjuaje huyu mama.... Sasa sahi anaharibu kila kitu,.... Lakini sasa huyu mama ndio yule alie onekana kwenye simu ya sahi, ndio huyu hapa
"shkamoo"
Sahi alimsalimia mama huyo, mama kwa mshtuko wa sauti ya mtu huyo alijikuta akilia mwenyewe,... Sasa swali linakuja hivi, kwanini sahi anafanana sauti na huyo kijana... Sasa je, hata huyu mama pia hamjui sahi??....
"huyu sahi, anajuana vipi na huyu mama,... Hapana lazima nimtaarifu General Nyange, je huyu ni nani?"
Aliongea Joseph huku akichukuwa simu yake na kutafuta jina la mr Nyange,...... Sasa sahi keshaharibu swala la kwenda kuchukuwa dom original....

ENDELEA..........

Hatimaye Dom original yapatika kirahisi sana, kumbe ile dom tuliokuwa tukiiona kwa sahi ile dom feki,.. Hivyo kwakuwa sahi ni mpelelezi japo kajiunga na watu hao sasa katika hali ya kwenda kuchukuwa dom original, wakiwa barabarani na askari mwenzie aitwaye Joseph John (JJ) sahi kina gari aliiona kitu kilichomfanya nae asimamishe gari baada ya gari hio alio iona kusimama katima sehemu za paking... Sasa kumbe hata Joseph anamjua mama huyo ambae sahi kasimamisha gari kwa ajili yake,

Joseph aliona hili nalo ni tatizo, hivyo alichukuwa simu na kumpigia mr Nyange wa kule kambini, na mama huyo ni mke wa mr Nyange, ambae ni mkuu wa jeshi
"haloo mkuu"
"Enheee vp umeshaipata hio dom"
"hapana, ndio tunaelekea huko... Lakini tupo hapa njiani tumemwona mama, ila kinachonishangaza ni kwamba mbona huyu kijana anafahamiana na mkeo ambae ni mama yake sheby"
"ni kweli... Ila huyo pia alikuwa ni rafiki wa sheby, hata mimi huku niliona picha ya mke wangu kwenye simu yake, nikamuuliza ndio akanipa huo ukweli"
Aliongea mr Nyange na ni kweli hata kule kambini sahi aliulizwa kuhusiana na hio picha katika simu yake, je wana mahusiano gani na mama huyo, na sahi alijibu vizuri tu.. Basi Joseph akawa kaupata ukweli kuwa kumbe nae huyu alikuwa rafiki yake, lakini Joseph bado haamini amini kwasababu yeye ndie rafiki mkubwa wa sahi, na anamjua sahi hakuwa na rafiki mwingine zaifi yake, sasa iweje leo ana rafiki mwingine...

Sasa huku kwa mama sheby akiwa na sahi, mama alitokwa na machozi baada ya kusikia sauti ya sahi, yaani sahi na sheby wamefanana sauti mpaka vitendo, yaani kasoro sura tu ndio tofauti, lakini laiti kama sura nazo zingeendana hata kidogo tu, ni lazima General aseme ni mtoto wake
"mama, sasa unalia nini"
Aliuliza sahi kwa heshima tu mana ni mama warafiki yake na hata yeye ni kama kalelewa na mama huyo mana saa zingine wanalala huko huko
"kijana angu, umenirudisha katika machungu ya kumpoteza mtoto wangu... Yaani mumefanana sauti kuliko kitu chochote kile"
Aliongea mama huyu, huku sahi nae akitokwa na machozi, sasa swali ni hivi, je? Familia ya akina sahi ni ipi, na mbona familia ya akina mr Nyange inamhisi kuwa kama mtoto wake,...
"shkamoo mama"
Alisalimia Joseph huku akimtaka sahi waondoke
"marahaba Joseph, hujambo mwanangu"
"sijambo"
"sahi twende bwana"
aliongea sahi huku kweli sahi akiachana na mama huyo kisha kufuata kazi iliomleta mjini

Airport kama kawaida mzigo ukiwa bado haujafika, hivyo lazima wachukiwe times ya kuusubiria mzigo huo,.. Walikaa takribani robo saa kisha wanaliona lihelikopta la jeshi likiwa linataka kutua Airport, wakati huo sahi ana ile dom feki, na hio helikopta ina dom original, hivyo ni kitendo cha kufanya mabadilishano tu kila mtu apite na kazi zake,...
"chukuwa na hii CD ni programu yake"
Sahi aliwapa na cd inayosemekana ni programu ya hio dom original, na wao waliamini kweli hio ni original, mana feki na original hawawezi kujua na hata sahi mwenyewe hapo hajui dom original ilivyo mana zote zimefanana... Sasa baada ya makabiziano sahi haamini kama kweli anamiliki dom original, na hio alio wapa ni dom feki, sasa Joseph anapiga simu kwa mkuu wake
"mkuu, kazi yako ulionituma nimeshaimaliza"
"safi sana... Ngoja ije kisha tumpigie yule mzungu"
"sawa... Natumaini pesa nono"
Sasa hapo kila mmoja akawa na furaha tena yakiwa ni majira ya jioni hivi, Joseph na sahi tayari ni marafiki wazuri, mana wamefanya jambo zuri sana kwa ushirikiano,...

Sasa katika kurudi, Joseph na sahi waliona wapitie sehemu fulani kupata moja moto moja baridi, sahi hua hatumiagi vinywaji vya kemikali, huq anatumia juice,.... Basi walipofika kila mmoja aliagiza kile akipendacho na kuanza kujiburudisha wakati huo watembea walikuwa wakipita kila mahala wakitaka wanaume..
"sahi, unaonaje tukaenda shiva"
"ati nini"
"twende zetu shiva tikajibebee watoto"
"aisee yaani afisa mzima uende ukanunue mwanamke danguro"
"acha ushamba wewe, sasa tabu ya lutongoza ya nini"
"tena wewe ni mtoto wa raisi GU, leo uende shiva jamaa angu... Twende zetu nyumbani bwana"
"acha zako sahi, wewe ni mwanaume rijali, kwanini ziishie kiunoni tu... Utakufa nazo.. Kule kuna warembo clasic, kuna watoto sio mchezo twende ukajionee"
Aliongea Joseph ambae yeye keshazoea tabia hio ya kununua wanawake shiva,... Wakati huo sahi na kirasketi chake (kibegi) alichowekea ile dom original,.. Na anayo bado hapo alipo sema uzuruni kwamba sahi sio mlevi hivyo kupotea kwa dom ni ngumu,...

Baada ya kushawishiwa sana sahi na Joseph kweli walisogea mahala husika yaani shivaz amako ndipo wasichana hujiuza kwa bei tofauti tofauti, wakati huo yapata majira ya saa moja za usiku, ukumhuke pale kwenye baa walipokuwa wanakunywa, walitumia muda mwingi sana kuwepo pale hivyo huku shivaz walifika times za saa moja za jioni japo kila mmoja kuwa na usafiri wake,...

Kama tunavyo wajua madada wanaojiuza wakiona magari tu yakipaki maeneo yao basi wanajua ni wateja, hivyo kuwakimbilia, lakini sahi yeye alikuwa ni mgeni kwenye tabia hii, hajui aanze vipi japo wanajileta wenyewe ni yeye tu kuchagua,
"kaka, ona kitu mnato kaka... Kaka nichukue mimi sina ghara kubwa sana"
Walikuwa wakijinadi wadada hao ili wapate kipato cha kuwakidhi mahitaji yao,... Sahi kila mschana aliomtazama alikuwa na uzuri wa kipekee, yaani haamini kama watoto wazuti namna hii wanakuja kufanya ufuska kama huu,... Sahi alishindwa amchukuwe yupi, wakati huo Joseph alikuwa akiwatomasa makalio, yaani yeye anachagua kwa kuwaminya makalio yao, eti anaangalia kama kuna mwenye kalio la kichina, mana kalio la kichina ni gumu...
Joseph alizungukwa na wasichana wengi huku wakisema
"kila siku nakuonye unaniminya minya tu afu unaniacha"
Aliongea dada mmoja aliekuwa akikaguliwa na Joseph kila siku lakini hamchukui, wakati huo sahi kaachana na wale wasichana wengine, sasa kabaki kumwangalia Joseph anavyo gombaniwa na wasichana hao, binafsi alihisi kucheka tu, mana anawaonea huruma wadada hao na anaamini kweli hawakuwa wakitaka kuifanya kazi hio ispokuwa shida ya kimaisha ndio chanzo cha kazi hio kuzaliwa, tena haswa kwa ukosefu wa ajira kwa wingi,..
"hili swala ni la kumfikishia raisi GU, hawa ni watu wa kuwasaidia hawa"
Sasa sahi akiwa anaendelea kujiuliza na wakayi huo hakuwa na mschana hata mmoja, wote walishamuacha mana amekaa kama mshamba mshamba hajui hata kuchagua....
Sasa alishtuliwa na sauti nzuuri, iliokuwa nyuma yake......
"shkamoo"
Ilikuwa ni sauti ya kike nzuri mno, kwanza kitendo cha kusalimiwa SHIKAMOO katika eneo hilo, ni sawa na kuokota embe dodo katika shamba la minazi... Sasa sahi anageuka na kuangalia nani katoa salamu ya aina hio,... Laaaaaa haulaaa alikuwa ni mschana mzuri tena mpole kupita kiasi,.. Hata sahi haamini kama na uzuri wote huu kakosa mwanaume wa kummiliki kimapenzi,...
"safi tu hali yako dada"
Sahi alijibu, lakini dada alionekana kuangalia huku na kule kana kwamba anaogopa mno na alionekana kuwa mgeni wa jambo hilo, mana hata zile mbwembwe za KAKA ONA KITU MNATO, sijui KAKA MI YANGU HAINA MAJI... Mara ooohhh KAKA JAMANI MIMI NAHIMILI USIKU KUCHA... Huyu alikuwa hana bali alikuwa kama vile anaogopa... Tena alikuwa kaumbika kuliko hata wale alio waona awali waliokuja kumzunguka, kisura chake jamani mtoto alikuwa mzuri....
"Samahani, nikusaidie nini dada angu"
Aliongea sahi huku akimuangalia jinsi anavyo hangaika kulishusha lile gauni alilovaa lililoishia mapajani, sasa anaona aibu kwa jinsi lilivyo fupi,... Mtoto wa kike alikuwa akiona aibu mno, zake ni kung'ata vidole tu
Sahi alijua nae ni mmoja wao,... Huyo hakumchelewesha
"twende basi"
Aliongea sahi tena kwa kujikaza mno,
Na dada kweli alikubali mana ndio kazi yake sema alionekana mgeni katika kazi hio,... Wakati huo Joseph hata hajulikani kaingilia mlango gani na kaenda na wasichana wangapi...

Chumbani dada kawa mgumu kuvua nguo,...

Lakini Baada ya masaa matatu kupita, dada huyo akiwa analia lia kitandani mwenyewe, wakati huo sahi ndio ananyanyuka kwenda kuoga,... Sasa huku chumbani, yule dada hakutaka kumsubiri sahi, lakini haijulikani kama kalipwa au laa,... Kwanza alichukuwa suruali ya sahi na kuisachi vizuri.. Kachukuwa waleti kisha kaangalia... Kakutana na vitambulisho vya uanajeshi.. Kaweka suruali pembeni kisha mana kakosa cha kuchukuwa mana hajazoea kuiba, lakini wakati huo dada alikuwa akichechemea, sasa hatujui kioi kimemkuta dada huyo mana hapo alikuwa na hasira ya hali ya juu,...
Sasa alipoangalia kwenye ile misumari ya mlangoni ya kuwekea vitu kama shati au suruali, na vingine vingi, sasa kwenye huo mlango kuna kile kibegi ambacho kina dom original, saa ngapi hajakichukuwa na kukisachi... Aliikuta dom original ikiwa imejaa katika kibegi hicho.. Kulikuwa na vitu vingi sana, ikiwemo laptop, na External hard drive na pia kulikuwepo na internal hard drive, na hio dom original, sasa dom na internal hard drive vinafanana na pia vinaendana kwa ukubwa.. Japo dom kubwa kidogo,...
"hii kubwa kubwa hii.. Itakuwa ina bei kubwa kidogo, wacha niondoke na hii kubwa"
Aliongea yule dada huku akiichukuwa dom Originally

Itaendelea.....

ITAENDELEA.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom