Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, ameamua kuondoka katika klabu hiyo huku Real Madrid, Manchester City na Paris Saint-Germain zikipambana kumsajili (L'Equipe)
Ligi ya Uhispania haitokubali kupokea malipo ya kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar kutoka PSG kwa sababu ya mzozo wa malipo ya uzalendo kati ya Neymar na Barca na pia wasiwasi kuhusu PSG kukiuka kanuni za fedha za UEFA. (Sport
Wakala wa zamani wa Neymar Wagner Ribeiro amesema "PSG watalipa kitita cha kutengua kifungu cha usajili" wa mchezaji huyo wa Brazil na kuwa "Neymar atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wiki hii". (Marca)