Makapuku Forum

Habari za asubuhi mabibi na mabwana
Wake kwa waume
Wakubwa kwa wadogo

Nafikiri mmeamka salama na harakati za kutafuta mawe zinaendelea fresh
Niwatakie Jumanne Njema
.....
 
Ahsante mdau
Kwa facts & dondoo
.
.
.
.
Tofauti ya Tz na Kenya
Kenya wanaouawa maiti zao zinapatikana wakati Bongo wanaouawa maiti zao hazipatikani
Sijui wanakula maiti ?
.....
 
Habari za asubuhi mabibi na mabwana
Wake kwa waume
Wakubwa kwa wadogo

Nafikiri mmeamka salama na harakati za kutafuta mawe zinaendelea fresh
Niwatakie Jumanne Njema
.....
Nzuri mdau

Nawe pia
 
Leo katika Historia

1876 - Jimbo la Colorado latambulika rasmi kama jimbo la 38 huko nchini Marekani.


Sehemu ya kusini mwa Colorado kuna safu za milima maarufu duniani za Rocky Mountains yaani ni kama Milima ya Usambara kule Lushoto

Kati ya majimbo 50 ya Marekani Colorado inakamata # 21 kwa idadi ya watu ikiwa na watu takribani 5,600,000
......
 
Leo katika Historia

1914 - Ujerumani yatangaza rasmi vita dhidi ya Urusi na hivyo kupelekea Vita kuu ya kwanza ya Dunia kuanza.


Ilijulikanakama Eastern Theater pia Eastern Front

Kando ya Mjerumani na Mrusi walikuwepo pia Ottoman Empire,Austro--Hungarian Empire na Romania Empire & Bulgaria
Ilikuwa ni vita ya wababe
Wapiganapo mafahari wawili nyasi huumia
......
 
Leo katika Historia

1960 - Nchi ya Dahomey yajitangazia Uhuru wake toka kwa Ufaransa.
Dahomey ilikuja kufahamika baadae kama Benin.

Dohamey ilianzishwa mwaka 1600
Wakoloni wa Kifaransa waliingia mwaka 1894 baada ya kumshinda Mfalme wao wa mwisho aittwaye King Behanzin
Pamoja na kupata uhuru waliendelea kutumia bendera ileile hadi miaka ya 1970's walipobadili jina
....
 
Leo katika Historia

1961 - Waziri wa Ulinzi wa Marekani anashauri kuanzishwa kwa Shirika la Ujasusi la Jeshi la Marekani na kufanya Marekani kuwa nchi ya kwanza yenye kutumia ujasusi wa Kijeshi.

Ikaja kuanzishwa rasmi 1 Oktoba 1951 ikijulikana kama Defense Intelligence Agency
.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…