Katika dondoo za bbc. ..

Rais Joseph Kabila afanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi. Ateua mkuu mpya wa jeshi hilo.

Marekani yaionya Venezuela kuwa itakabiliwa na hatua za kiuchumi iwapo itaendelea na mipango yake ya kutaka kuandika upya katiba ya nchi hiyo.

Idhaa ya BBC Somali inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza Julai 18 1957.

Hali ya upatikanaji wa mafuta ya petroli na dizeli imeanza kurejea katika baadhi ya miji nchini Tanzania baada ya Mamlaka ya mapato kuvifunga vituo hivyo kwa kushindwa kuweka mashine za kielektroniki kwenye pampu.